Baada ya crimea kujiunga na Russia, wengine nao wanataka kujiunga

Baada ya crimea kujiunga na Russia, wengine nao wanataka kujiunga

JustDoItNow

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,967
Reaction score
1,513
140409111126_ukraine_512x288_bbc_nocredit.jpg

Majengo yaliyotekwa mashariki ya Ukraine
Waukraine wanaoishi mashariki mwa taifa hilo wanatakriban saa 48 kuamua mustakabal wao la sivyo wakabiliane na vyombo vya usalama vya dola.
Taarifa zinazohusiana
Siasa
Waziri wa masuala ya ndani nchin Ukrain Arsen Avakov amewaambia waandishi wa habari mjini Kiev kuwa hali iliyo mashariki mwa nchi itatatuliwa kstika masaa 48 yajayo aidha kwa mazungumzo au kwa
kutumia nguvu.

Wanaharakati wanaoiunga mkono Urusi bado wameyateka majengo ya serikali kwenye miji miwili iliyo mashariki mwa Ukrain
Duru zinaarifa kuwa baadhi ya waandamani ambao walikuwa wameteka majengo ya serikali katika mji wa Luhansk wameondoka .

Mapema juma hili utawala nchini Ukrain uliendesha kile ulichokiita kampeni dhidi ya ugaidi ukilenga makundi yaliyotenga.
Ukrain inaishutumu Urusi kwa kuchochea ghasia.
Maafisa wa ngazi za juu kutoka Urusi, Marekani , Ukrain na Jumuiya ya Ulaya wamekubalina kufanya mazunguzmo juma lijalo.
140409101929_ukraine_donetsk_512x288_ap.jpg

Majengo yaliyotekwa Donetsk
Mazungumzo hayo yanalenga kuleta uwiano baada ya Urusi kuteka eneo la Crimea mwezi February .
Majeshi ya Urusi yangali karibu na mpaka wa Ukraine .
Taharuki imetanda mijini Luhansk, Donetsk na Kharkiv tangu watu wanaounga mkono hatua ya Urusi kuchukua Crimea kudai wanataka Urusi itawale miji hiyo iliyoko mashariki mwa Ukraine.

Serikali ya Kiev tayari imewataja kuwa magaidi na kuwa inapanga operesheni dhidi ya magaidi hao katika kipindi cha siku mbili zijazo.
Bwana Avakov amesema kuwa afua ni mbili mazungumzo ya amani ama vita.
Kiongozi wa waandamani mjini Luhansk amemuaomba rais wa Urusi Vladimir Putin kuwasaidia wasidhulumiwe na Kiev.

Wakati huohuo serikali ya Kiev imetangaza kuwa imewaachia watu 56 waliokuwa wamekamatwa kwa kuvamia majengo ya Umma.
Huko Kharkiv viongozi wa maandamano wamelaumu serikali ya Kiev kwa matatizo mengi yanayowakumba na wakaitisha kura ya maoni ya kuamua iwapo wangependa kusalia Ukraine ama kujiunga na Urusi.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa kiev imetwaa majengo yaliyokuwa yametekwa na waandamanji ingawaji hali ingali tata katika mji ulioko karibu wa Donetsk.


Chanzo:BBC
 
Any war with Russia will be nuclear.Na outcome ya nuclear war Russia itashinda

Russia land mass ni the largest na ina span 7 time zones.Marekani na Europe ni ndogo compared to Russia.

Sasa wakianza kulipuana idadi kubwa ya survivours itakuwa upande wa Russia kwa ajili ya ukubwa wake.Na kuna wadau wanadai S-500 ina uwezo wa ku counter kombola lolote litokee Germany(American nuclear silo) au marekani kwenyewe

Balaa tupu.
 
ngoja tuone mchezo utavyokua,kwani hii dunia haitokua na amani hadi vita ya tatu itokee na super power ajulikane tena ndio kutakua na kueshimiana,
 
Back
Top Bottom