Kufukuzwa kwa Waziri wa Ulinzi wa Ukraine ndio kutasababisha Urusi ishinde?
Mmemuua Prigozhin na Utkin ambao ndio wapiganaji wakubwa pale Urusi na Wagner yao na wana medani za kutosha. Mmemuondoa General Surovikin ambaye ndiye the most competent jeshi zima la Urusi mmebaki na wazee watupu.
Waziri ajaye hapo Ukraine ana miaka 41. Jumlisha na kina Zelensky, Kuleba, Budanov, Zaluzhnyi na wakubwa wengine mnapigana na 40s hapo, nyie mna wazee wa enzi za Soviet Union hawana mbinu mpya na wamekariri nguvu wasizokuwa nazo kwa sasa.
Hicho anachofanya Zelensky kafanya mara nyingi tangu awe Rais na kabla ya vita. Hapati shida kumuondoa kiongozi akamteua mwingine anayefaa zaidi, the next anayeweza kuondoka ni Foreign Minister. Putin yeye labda aue au awafiche, hatoi vigogo mara kwa mara.