CHADEMA wachukua Fomu za Kugombea Ubunge Majimbo Mawili. Salum Mwalim Juma (Kinondoni) na Elvis Christopher (Siha)

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,157
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amechukua fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Kinondoni

Habari zaidi zinakuja.....

=======

TAARIFA KWA UMMA, KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA KINONDONI NA SIHA.

Kamati Kuu ya Chama imemaliza Vikao vyake Leo tarehe 19 Januari, 2018 na imefanya uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018.

Baada ya uamuzi huu kufanyika , Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo kama ifuatavyo;

1. Jimbo la Kinondoni ameteuliwa Mhe. Salum Mwalim Juma

2. Jimbo la Siha ameteuliwa Bwana Elvis Christopher Mosi

Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika na watazirejesha kesho Jumamosi tarehe 20 Januari 2018 , kwa ajili ya uteuzi.

Imetolewa Leo tarehe 19 Januari, 2018.

John Mrema - Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amechukua fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Kinondoni

Habari zaidi zinakuja.....
Huyu anahangaika bure,kama ameshindwa kuchaguliwa mchambawima,kura 3,000 tu umechukua jimbo ataweza kinondoni?
Ni vizuri chadema wanavyowafanya wafuasi wao wajinga.Singida kaskazini na songea mjini wamewakataza wasishiriki,lakini bila ya walichosusa kutekelezwa,kigogo ameshajitwalia fomu kinondoni.Hii ndio chadema ya mazuzu
 
Dar es salaam ndio Jiji,
Na Makao Makuu ya CDM hayawezi kua under CCM
 
Kumbe ile kususa ilikuwa geresha haa haa au zile kasoro walizosema tume imezifanyia kazi kweee kwee kweee Watu wa namarumango wanatusaidia sana
Wasiwasi wanini? Mmepata fundisho. Halafu muache ugaidi wakupiga watu mapanga na kuteka wapinzani.
 
Mgombea wa ccm. ambaye ndie alikuwa mbunge wa kinondoni kabla ya kujiuzuru atatangazwa mshindi.

(atatangazwa mshindi..... mnielewe hapo) sio kwa sababu anapendwa na wengi au ndie atapata kura nyingi..
Tayari ushaanza kujitisha
 
Huyu anahangaika bure,kama ameshindwa kuchaguliwa mchambawima,kura 3,000 tu umechukua jimbo ataweza kinondoni?
Ni vizuri chadema wanavyowafanya wafuasi wao wajinga.Singida kaskazini na songea mjini wamewakataza wasishiriki,lakini bila ya walichosusa kutekelezwa,kigogo ameshajitwalia fomu kinondoni.Hii ndio chadema ya mazuzu
Mlizoea vya kunyonga mlifikiri safari hii nayo mtazoa mizoga kama singida na songea, safari hii hakuna cha kumuachia fisi bucha lazima muusotee au muue kabisa kama mlivyozoea.
 
Back
Top Bottom