Ngoja nitoke kidogo nje ya maada husika; kuna kitu hua kinanipa shida sana kukielewa ndani ya ccm; hivi hua haiwezekani kua kiongozi ndani ya hiki chama na ukadumisha hali yako ya kiucha Mungu? Nasema hivyo kwasababu zifuatazo, nina orodha kubwa ya viongozi ndani ya chama hiki ambao kabla hawajawa viongozi walikua watu wenye hofu ya Mungu sana but leo wanafanya mambo ya kishetani balaa; Jesca anaetajwa humu, ninamfahamu sana tu, nimesoma nae Mkwawa high school, nakumbuka wakati huo alikua bonge la mlokole though alikua dada mmoja mcheshi sana tu, ole wako umuombe papuchi, she was very smart na alikua kiongozi wa bweni na kwenye kikundi chake cha maombi pale shule, ninapomtazama Jesca wa Mkwawa na Jesca wa ccm kimatendo akili inakataa kabisa; Jesca wa kuongoza utoaji wa rushwa? Jesca wa kuongoza vijana kubaka manamke mwenzie? refer lile saga la uchaguzi wa ubunge pale Tosamaganga na kile walichomfanyia aliyekua mke wa Dr. Slaa (uzi huo umo humu ndani)
Namtazamaga mama Rwakatare na uchungaji wake, mara tukasikia kachakachua umeme na kujenga nyumba mahali pasipo sahihi na akiwa anajua, how?
Mama wa wale mabinti wa J sisters, the way alivyokua akiongea bungeni juzi kwenye ESCROW A/C ni full unafiki na hiyo ni miongoni mwa dhambi mbaya sana kwa mujibu wa walokole, mara uzi ukabandikwa humu kwamba through mhe. Suleman Nchambi, mbunge wa kishapu huyu mama alikula mgao na akalishwa maneno!
Nape Moses Nnauye, ujana wake wote alikua mlokole, kapiga magitaa kwenye mikutano yao ya injili, hadi anagombea ubunge Ubungo, dogo alikua bado mlokole, sina hakika na alipoupata ukuu wa wilaya kama aliendelea au laa, ninapo mtazama na kumsikiliza Nape wa ccm, naziona chembe chembe za namna ya uongeaji wake kwenye mikutano ya ccm na za wahubiri wa kilokole, ndani ya maneno yake kumejaa uongo, unafiki na chuki dhidi ya wasiokua wafuasi wa chama chake, inakuaje? List ni ndefu, kama kina Juliana Shonza n.k, swali langu ni hili, hivi hiki chama kinafuata miiko ya kishetani au nini? Sina maana kwamba viongozi wa kisiasa wawe wachaa Mungu laa, maana ndani ya ccm, CDM, CUF n.k wapo pia wasio amini katika Mungu,point yangu ni hi, kwanini wakifika huko wanaacha? Hata Jesca Msavatavangu?
Back to the topic, viongozi wa CDM mmesikia, kuna vijana wenzetu huko Iringa wamebambikiziwa case na Lukuvi na Jesca, please hu ndio wakati wa kuonesha chama kina jali wafuasi wao, nendeni Iringa mkawaokoe hawa. Mara baada ha hi scandle, timu ya M4C pamoja na operation delete ccm walitenge Iringa vijijini hadi Lukuvi aachie ngazi.