Baada ya CHADEMA kutikisa Jimbo la Isimani,Lukuvi aanza kubambikia Vijana kesi Polisi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
Hali si shwari mara baada ya uchaguzi wa SM Jimboni Isimani,baada ya ngome ya Chama cha Mapinduzi iliyopo kijiji cha Migoli kutikiswa.Chadema imechukuwa kijiji na baadhi ya vitongoji katika kata ya Migoli ambapo ndio ngome ya CCM.Hii imewastua sana CCM na Lukuvi,kwamba "usultani" wake ndani ya Jimbo hilo umetikiswa.

Ikumbukwe kuwa toka 1995 ktk uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi,Jimbo la Isimani halikuwahi kuwa na upinzani,ndio jimbo pekee toka 1995 ambapo mbunge wake William Vangimembe Lukuvi alikuwa anapita bila kupingwa,yaani wakati wananchi wengine sehemu nyingine Tz walipokuwa wanapiga kura,Isimani hawakuwa wanapiga kura,maana madiwani,wabunge na Raisi kupitia chama cha Mapinduzi hawakuwa na mpinzani.

Hali imekuwa tofauti kwa sasa,katika maeneo mengi upinzani umechukua viti katika serikali za mitaa,hizi ni salamu za mwakani kwenye uchaguzi mkuu,siku kadhaa kabla ya uchaguzi wa SM;Mwenyekiti wa CCM-Mkoa Mama Jesca na Mh.Lukuvi walipiga kambi kwenye ngome yao ya kata ya Migoli,wakimwaga hela na vitisho kwa vijana wa upinzani..katikati ya dhiki na taabu,umaskini na hongo Wananchi wa Isimani wametoa kura kwa upinzani na kupata kata moja,wajumbe kadhaa na vitongoji..na ushindi wa CCM ni wa tofauti ya Kura 4 hadi 5.

Ushindi huu umesababisha Lukuvi kuwabambikia kesi wafuasi wa Chadema kwa visingizio vya kumtishia Mwenyekiti wa CCM aliyeangushwa na Chadema ambaye ameongoza kijiji 2009-2014,toka usiku wa kuamkia J3 vijana waliokuwa team ya kampeni wamekamatwa na kupelekwa mjini Iringa kisirisiri wakati Migoli kuna polisi na Mahakama ya kuwahukumu kama wana hatia.

Vijana,wanaume wawili na mwanadada mmoja ambaye alikuwa muhamasishaji kwa upande wa kina Mama wapo lupango kwa kesi za kutungwa,Polisi katika kijiji cha Migoli wanadai wanatekeleza maagizo kutoka juu,Mwenyekiti wa CCM Bw.Mwengwa aliyeangushwa na CDM anasema yeye haijui hiyo kesi na hana uwezo wa kuhamishia kesi mjini,Afisa Mtendaji wa Kata ambaye hana hata miezi 6 toka aletwe hapo kimkakati ili kucahakachua uchaguzi amekimbia kituo cha kazi baada ya kuona hali ni ngumu na analalamikiwa na CCM kushindwa kuibakiza Kata mikononi mwa CCM.

Katika mkutano wa kampeni uchaguzi SM Kata ya Migoli,uliofanyika katika viwanja vya Maakama,Mh.Lukuvi aliuambia mkutano wa hadhara kuwa katika watu watano viongozi wakubwa nchi hii yeye yumo,na kwamba MTU wa kulichukua Jimbo la Isimani hajaonekana bado kwa sasa.

Vijana hawa wamewekwa ndani kwa makosa ya kutengenezwa,mpaka sasa haikulikani kosa Lao,Watu wanawaomba CCM mkoa wa Iringa na Jimbo la Isimini kutotumia vibaya vyombo vya dola,wakubaliane na mabadiliko.Viongozi wa Chadema mkoa wa Iringa wawasaidie kisheria vijana hawa ili haki itendeke.CCM kubalini mabadiliko na muwe wavumilivu wa siasa za ushindani.....Vangimembe Lukuvi William,Ubunge si usultani,kubali mabadiliko na usitumie ubunge na cheo chako cha uwaziri kuwashurutisha polisi kuonea watu.

Msaada wa kisheria toka kwa Viongozi wa CHADEMA unahitajika kwa vijana hawa.
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
Safi sana Wana wa Isimani,Lukuvi alifanya hilo jimbo kama mali yake binafsi....Pigeni kazi,Viongozi Chadema wasaidieni hawa vijana kisheria...CCM wamezoea kubambikizia kesi
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,464
2,000
Maneno yasiyo na elimu wala njozi ya wakati. Sasa imetokea na atakuwa chini ya mfalme asiyempenda, atahama jimbo?

…Katika mkutano wa kampeni uchaguzi SM Kata ya Migoli,uliofanyika katika viwanja vya Maakama,Mh.Lukuvi aliuambia mkutano wa hadhara kuwa katika watu watano viongozi wakubwa nchi hii yeye yumo,na kwamba MTU wa kulichukua Jimbo la Isimani hajaonekana bado kwa sasa.…
 
suleym

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,918
2,000
tatizo viongozi aina ya lukuvi wanatengeneza chuki kwa wananchi zisizo namsingi hawajui kuwa hao wanaowaweka ndani wana ndugu wanaoweza kuambukiza chuki hiyo kwa wananchi wengine ikaleta madhara kwenye ubunge wake, tena ajue kwa vijijjini wananchi wanaishi km ndugu, mmoja akipata janga jamii nzima inaguswa aendelee tu na ubabe wake atajuta!
 
timbilimu

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
4,813
2,000
Lukuvi anaharibu mpaka kwao?! Hapa Dsm Mbezi beach anakoishi ni mtu mpweke hasiye kuwa karibu na majirani. Madaraka na pesa vimemwondelea utu,anaishi kwa wasiwasi!
 
Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Anaogopa kikiota nyasi atarudi kufundisha shule ya msingi kijijini kwao.
Ka certificate ka TTC ndo kanamfanya aseme hakuna wakuongoza jimbo lake?
Mbona anawaogopa wasomi wenye PhD toka Isimani na huwa mpole kweli akisikia wanataka kuchukua form? Hiiii:becky:
Anadhani hatujui hili?
Lukuvu acha matusi ya nguoni gwaride la chipukizi lilikupa ulaji, gwaride limeisha miaka nenda rudi kwa nini ulaji wako uendelee???.
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
10,018

Huyu Lukuvi ndo aliye ratibu uchakachuaji wa maoni ya wananchi ya katiba mpya
 
Kundelungu

Member
Oct 2, 2011
87
70
Anaogopa kikiota nyasi atarudi kufundisha shule ya msingi kijijini kwao.
Ka certificate ka TTC ndo kanamfanya aseme hakuna wakuongoza jimbo lake?
Mbona anawaogopa wasomi wenye PhD toka Isimani na huwa mpole kweli akisikia wanataka kuchukua form? Hiiii:becky:
Anadhani hatujui hili?
Lukuvu acha matusi ya nguoni gwaride la chipukizi lilikupa ulaji, gwaride limeisha miaka nenda rudi kwa nini ulaji wako uendelee???.
Ni kale ka TTC Tabora?
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,177
2,000
Ngoja nitoke kidogo nje ya maada husika; kuna kitu hua kinanipa shida sana kukielewa ndani ya ccm; hivi hua haiwezekani kua kiongozi ndani ya hiki chama na ukadumisha hali yako ya kiucha Mungu? Nasema hivyo kwasababu zifuatazo, nina orodha kubwa ya viongozi ndani ya chama hiki ambao kabla hawajawa viongozi walikua watu wenye hofu ya Mungu sana but leo wanafanya mambo ya kishetani balaa; Jesca anaetajwa humu, ninamfahamu sana tu, nimesoma nae Mkwawa high school, nakumbuka wakati huo alikua bonge la mlokole though alikua dada mmoja mcheshi sana tu, ole wako umuombe papuchi, she was very smart na alikua kiongozi wa bweni na kwenye kikundi chake cha maombi pale shule, ninapomtazama Jesca wa Mkwawa na Jesca wa ccm kimatendo akili inakataa kabisa; Jesca wa kuongoza utoaji wa rushwa? Jesca wa kuongoza vijana kubaka manamke mwenzie? refer lile saga la uchaguzi wa ubunge pale Tosamaganga na kile walichomfanyia aliyekua mke wa Dr. Slaa (uzi huo umo humu ndani)

Namtazamaga mama Rwakatare na uchungaji wake, mara tukasikia kachakachua umeme na kujenga nyumba mahali pasipo sahihi na akiwa anajua, how?

Mama wa wale mabinti wa J sisters, the way alivyokua akiongea bungeni juzi kwenye ESCROW A/C ni full unafiki na hiyo ni miongoni mwa dhambi mbaya sana kwa mujibu wa walokole, mara uzi ukabandikwa humu kwamba through mhe. Suleman Nchambi, mbunge wa kishapu huyu mama alikula mgao na akalishwa maneno!

Nape Moses Nnauye, ujana wake wote alikua mlokole, kapiga magitaa kwenye mikutano yao ya injili, hadi anagombea ubunge Ubungo, dogo alikua bado mlokole, sina hakika na alipoupata ukuu wa wilaya kama aliendelea au laa, ninapo mtazama na kumsikiliza Nape wa ccm, naziona chembe chembe za namna ya uongeaji wake kwenye mikutano ya ccm na za wahubiri wa kilokole, ndani ya maneno yake kumejaa uongo, unafiki na chuki dhidi ya wasiokua wafuasi wa chama chake, inakuaje? List ni ndefu, kama kina Juliana Shonza n.k, swali langu ni hili, hivi hiki chama kinafuata miiko ya kishetani au nini? Sina maana kwamba viongozi wa kisiasa wawe wachaa Mungu laa, maana ndani ya ccm, CDM, CUF n.k wapo pia wasio amini katika Mungu,point yangu ni hi, kwanini wakifika huko wanaacha? Hata Jesca Msavatavangu?

Back to the topic, viongozi wa CDM mmesikia, kuna vijana wenzetu huko Iringa wamebambikiziwa case na Lukuvi na Jesca, please hu ndio wakati wa kuonesha chama kina jali wafuasi wao, nendeni Iringa mkawaokoe hawa. Mara baada ha hi scandle, timu ya M4C pamoja na operation delete ccm walitenge Iringa vijijini hadi Lukuvi aachie ngazi.
 
afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Maneno yasiyo na elimu wala njozi ya wakati. Sasa imetokea na atakuwa chini ya mfalme asiyempenda, atahama jimbo?

…Katika mkutano wa kampeni uchaguzi SM Kata ya Migoli,uliofanyika katika viwanja vya Maakama,Mh.Lukuvi aliuambia mkutano wa hadhara kuwa katika watu watano viongozi wakubwa nchi hii yeye yumo,na kwamba MTU wa kulichukua Jimbo la Isimani hajaonekana bado kwa sasa.…
Hivi huwa hamjui kuwa Lukuvi ana kasoro kwenye network kichwani? sasa maneno gani hayo kama siyo mgonjwa wa akili
 
lustaki

Senior Member
Sep 24, 2014
176
195
CDM na wadau au mdau yeyote anaeweza kuwasaidia hawa makamanda wenzetu kisheria plz n plz jamani nendeni haraka mkawasaidie... huu ndo mtaji wa kupata kura mwakani,,, plz jamani ccm hawajui kuwa ndo wanazid kuharibu. Maskini lukuvi huyuuuu mweeeee! Makamanda plz wasaidieni hao
 
respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,535
2,000
Ngoja nitoke kidogo nje ya maada husika; kuna kitu hua kinanipa shida sana kukielewa ndani ya ccm; hivi hua haiwezekani kua kiongozi ndani ya hiki chama na ukadumisha hali yako ya kiucha Mungu? Nasema hivyo kwasababu zifuatazo, nina orodha kubwa ya viongozi ndani ya chama hiki ambao kabla hawajawa viongozi walikua watu wenye hofu ya Mungu sana but leo wanafanya mambo ya kishetani balaa; Jesca anaetajwa humu, ninamfahamu sana tu, nimesoma nae Mkwawa high school, nakumbuka wakati huo alikua bonge la mlokole though alikua dada mmoja mcheshi sana tu, ole wako umuombe papuchi, she was very smart na alikua kiongozi wa bweni na kwenye kikundi chake cha maombi pale shule, ninapomtazama Jesca wa Mkwawa na Jesca wa ccm kimatendo akili inakataa kabisa; Jesca wa kuongoza utoaji wa rushwa? Jesca wa kuongoza vijana kubaka manamke mwenzie? refer lile saga la uchaguzi wa ubunge pale Tosamaganga na kile walichomfanyia aliyekua mke wa Dr. Slaa (uzi huo umo humu ndani)

Namtazamaga mama Rwakatare na uchungaji wake, mara tukasikia kachakachua umeme na kujenga nyumba mahali pasipo sahihi na akiwa anajua, how?

Mama wa wale mabinti wa J sisters, the way alivyokua akiongea bungeni juzi kwenye ESCROW A/C ni full unafiki na hiyo ni miongoni mwa dhambi mbaya sana kwa mujibu wa walokole, mara uzi ukabandikwa humu kwamba through mhe. Suleman Nchambi, mbunge wa kishapu huyu mama alikula mgao na akalishwa maneno!

Nape Moses Nnauye, ujana wake wote alikua mlokole, kapiga magitaa kwenye mikutano yao ya injili, hadi anagombea ubunge Ubungo, dogo alikua bado mlokole, sina hakika na alipoupata ukuu wa wilaya kama aliendelea au laa, ninapo mtazama na kumsikiliza Nape wa ccm, naziona chembe chembe za namna ya uongeaji wake kwenye mikutano ya ccm na za wahubiri wa kilokole, ndani ya maneno yake kumejaa uongo, unafiki na chuki dhidi ya wasiokua wafuasi wa chama chake, inakuaje? List ni ndefu, kama kina Juliana Shonza n.k, swali langu ni hili, hivi hiki chama kinafuata miiko ya kishetani au nini? Sina maana kwamba viongozi wa kisiasa wawe wachaa Mungu laa, maana ndani ya ccm, CDM, CUF n.k wapo pia wasio amini katika Mungu,point yangu ni hi, kwanini wakifika huko wanaacha? Hata Jesca Msavatavangu?

Back to the topic, viongozi wa CDM mmesikia, kuna vijana wenzetu huko Iringa wamebambikiziwa case na Lukuvi na Jesca, please hu ndio wakati wa kuonesha chama kina jali wafuasi wao, nendeni Iringa mkawaokoe hawa. Mara baada ha hi scandle, timu ya M4C pamoja na operation delete ccm walitenge Iringa vijijini hadi Lukuvi aachie ngazi.
Heshima zote kwa post hii

BACK TANGANYIKA
 
Kikuyumbo

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
391
170
Miongoni mwa watu watano wa juu ambao ni WEZI wa mali za umma na wala Rushwa, Lukuvi yumo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom