barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Hali si shwari mara baada ya uchaguzi wa SM Jimboni Isimani,baada ya ngome ya Chama cha Mapinduzi iliyopo kijiji cha Migoli kutikiswa.Chadema imechukuwa kijiji na baadhi ya vitongoji katika kata ya Migoli ambapo ndio ngome ya CCM.Hii imewastua sana CCM na Lukuvi,kwamba "usultani" wake ndani ya Jimbo hilo umetikiswa.
Ikumbukwe kuwa toka 1995 ktk uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi,Jimbo la Isimani halikuwahi kuwa na upinzani,ndio jimbo pekee toka 1995 ambapo mbunge wake William Vangimembe Lukuvi alikuwa anapita bila kupingwa,yaani wakati wananchi wengine sehemu nyingine Tz walipokuwa wanapiga kura,Isimani hawakuwa wanapiga kura,maana madiwani,wabunge na Raisi kupitia chama cha Mapinduzi hawakuwa na mpinzani.
Hali imekuwa tofauti kwa sasa,katika maeneo mengi upinzani umechukua viti katika serikali za mitaa,hizi ni salamu za mwakani kwenye uchaguzi mkuu,siku kadhaa kabla ya uchaguzi wa SM;Mwenyekiti wa CCM-Mkoa Mama Jesca na Mh.Lukuvi walipiga kambi kwenye ngome yao ya kata ya Migoli,wakimwaga hela na vitisho kwa vijana wa upinzani..katikati ya dhiki na taabu,umaskini na hongo Wananchi wa Isimani wametoa kura kwa upinzani na kupata kata moja,wajumbe kadhaa na vitongoji..na ushindi wa CCM ni wa tofauti ya Kura 4 hadi 5.
Ushindi huu umesababisha Lukuvi kuwabambikia kesi wafuasi wa Chadema kwa visingizio vya kumtishia Mwenyekiti wa CCM aliyeangushwa na Chadema ambaye ameongoza kijiji 2009-2014,toka usiku wa kuamkia J3 vijana waliokuwa team ya kampeni wamekamatwa na kupelekwa mjini Iringa kisirisiri wakati Migoli kuna polisi na Mahakama ya kuwahukumu kama wana hatia.
Vijana,wanaume wawili na mwanadada mmoja ambaye alikuwa muhamasishaji kwa upande wa kina Mama wapo lupango kwa kesi za kutungwa,Polisi katika kijiji cha Migoli wanadai wanatekeleza maagizo kutoka juu,Mwenyekiti wa CCM Bw.Mwengwa aliyeangushwa na CDM anasema yeye haijui hiyo kesi na hana uwezo wa kuhamishia kesi mjini,Afisa Mtendaji wa Kata ambaye hana hata miezi 6 toka aletwe hapo kimkakati ili kucahakachua uchaguzi amekimbia kituo cha kazi baada ya kuona hali ni ngumu na analalamikiwa na CCM kushindwa kuibakiza Kata mikononi mwa CCM.
Katika mkutano wa kampeni uchaguzi SM Kata ya Migoli,uliofanyika katika viwanja vya Maakama,Mh.Lukuvi aliuambia mkutano wa hadhara kuwa katika watu watano viongozi wakubwa nchi hii yeye yumo,na kwamba MTU wa kulichukua Jimbo la Isimani hajaonekana bado kwa sasa.
Vijana hawa wamewekwa ndani kwa makosa ya kutengenezwa,mpaka sasa haikulikani kosa Lao,Watu wanawaomba CCM mkoa wa Iringa na Jimbo la Isimini kutotumia vibaya vyombo vya dola,wakubaliane na mabadiliko.Viongozi wa Chadema mkoa wa Iringa wawasaidie kisheria vijana hawa ili haki itendeke.CCM kubalini mabadiliko na muwe wavumilivu wa siasa za ushindani.....Vangimembe Lukuvi William,Ubunge si usultani,kubali mabadiliko na usitumie ubunge na cheo chako cha uwaziri kuwashurutisha polisi kuonea watu.
Msaada wa kisheria toka kwa Viongozi wa CHADEMA unahitajika kwa vijana hawa.