Kweli waliosema ukishangaa ya MUSA utashuhudia ya Firauni hawakukosea.! Chama cha Mapinduzi baaada ya kuona kuwa Mbinu zote za kuichafua CHADEMA hapa Arusha Mjini zimeshindwa haswa kwa ile mbinu ya kuiita ni chama cha Wachagga leo nimeshuhudia kituko kingine.
Ikumbukwe kwamba CHADEMA walikuwa wakitumia uwanja wa NMC kama uwanja wao wa Mikutano mikubwa na midogo.
Lakini mwishoni mwa mwaka jana Mkuu wa mkoa na mkurugenzi walihalalisha uwanja huo wa NMC kufanywa Soko.
Baada ya hapo CHADEMA wakawa wanautumia uwanja wa shule ya Ngarenaro ambao mara zingine ulishindikana kutumiwa kwa ajili ya wanafunzi ambao wanakuwa shuleni siku za kazi.
Viwanja vya Soweto vipo chini ya AICC na na miaka yote vimekuwa vikutumika na watu kwa michezo mbalimbali bila masharti yeyote. Lakini cha kushangaza leo nikiwa napita maeneo yale nilifanikiwa kuona VIBAO VYA MATANGAZO vikiwa vimewekwa kuzunguka uwanja wote maneno yenyewe ni haya; ILANI. HAIRUHUSIWI KUFANYA MICHEZO AINA YEYOTE AU "SHUGHULI NYINGINE YEYOTE" KATIKA VIWANJA HIVI BILA IDHINI YA UONGOZI. BY UTAWALA WA AICC.
Hii yote ni mbinu inayofanywa na Ccm kuhakikisha kuwa CHADEMA hawapati eneo la karibu mjini hapa kufanya mikutano. Sasa uwanja wa shule ya Ngarenaro nao unazungushiwa uzio na manispaa ktk kilekile cha kuhakikisha kuwa CHADEMA wakitaks kufanya Mkutano wao basi either waende viwanja vya Suye au Kimandolu nje kabisa ya mji.
CHADEMA kwa Arusha ipo Mioyoni mwa watu na sio viwanjani. Kitendo cha Ccm na washirika wake kuzuia viwanja vyote kutotumika na CHADEMA hakutasababisha watu na wapenzi wa CHADEMA kuacha kuiunga Mkono.
Hii ni sawa na kujaza maji kwenye gunia wakati unajuwa kuwa huwezi kujaza hata ukitumia water pump!!