Baa za Tabata kwa misosi bado sana

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,436
17,080
Nimekua nikisikia kua Tabata ndio kuna bata, basi siku za hivi karbuni nikawa na mambo yangu maeneo hayo.

Pia nikaamua kufanya utafiti usio rasmi kuhusu ubora wa misosi ya hizo bar. Kwa mfano 4040 pub, misosi ya hovyo sana.

Siku ya kwanza niliagiza ugali na makange ya kuku wa kienyeji. Msosi ulipokuja nyama ikawa na ladha chachu, nikauliza kama ni ya jana yake, nikaambiwa hapana ni ya siku hiyo.

Siku ya pili nikaagiza makange ya mbuzi, nikaletewa, nyama ina ladha ya uchachu, nikamuita mhudumu akashindwa kunipa majibu, nikaita mpishi akasema nyama haina tatizo labda tatizo liko kwenye nyanya, maana wanatumia nyanya za kopo.

Baada ya kuniambia kua wanatumia nyanya za kopo hata ham ya kula ikaniishia, nikalipa nikaendelea na mambo yangu. Binafsi hapa Bongo siwezi kula vitu vya kopo, bado tuna vitu fresh vingi sana. Nyanya fresh zinaoza Buguruni au Kariakoo sokoni alafu mtu unapikia nyanya za kopo?

Binafsi nikahitimisha kua Bar za Tabata kwa ubora wa misosi bado sana, bado hawajafikia misosi tunayokula Bar za mwenge au Kinondoni.

Kwa upande mwingine hata yale mambo yetu, watoto ni wa kawaida sana. Mimi nikienda bar naangalia misosi na totozi mara moja moja tu maana sinyi pombe na sijawahi kunywa na sina mpango wa kunywa.
 
Pole sana kwa kutokunywa pombe mkuu. Hapo ndio unapokosa uhondo wa Ulimwengu. Kunywa pombe sio lazima uwe mlevi. Kuna tofauti kubwa kati ya mnywa pombe na mlevi.
Takwimu zinaonyesha watu wasiotumia kilevi huwa wanaangamia sana kwenye ngono uzembe.
 
Ukiona mpishi anazidisha ndimu au limau ujue anajaribu kupoteza ladha halisi ya nyama/samaki iliyoharibika mkuu. Tunakula matakataka sana huku mabarabarani.
Sio kweli, recipe ya makange ina ndimu ndani yake mkuu.
 
Hasty generalization

Is an informal fallacyof faulty generalization by reaching an inductive generalization based on insufficient evidence—essentially making a rushed conclusion without considering all of the variables.
 
Sio kweli, recipe ya makange ina ndimu ndani yake mkuu.
Hapa tutabishana kama misukule mkuu.
Mimi ni mlaji na naomba niweke wazi huwa napenda kupika tokea enzi za ujana wangu. Mara nyingi nimekuwa nikikutana na Makange ya kuku walioharibika yamejazwa ndimu/limao kupita kiasi. Kuna Bar fulani (jina kapuni) maeneo ya Ubungo niliwahi kula Makange ya kuku nyama ilikuwa inateleza kama mlenda, ikiwa imejazwa ndimu na tangawizi kupunguza harufu. Anachoeleza mleta mada kinafanyika sana kwenye mabaa, haswa ukiwa mteja mgeni.
 
Nimekua nikisikia kua Tabata ndio kuna bata, basi siku za hivi karbuni nikawa na mambo yangu maeneo hayo.

Pia nikaamua kufanya utafiti usio rasmi kuhusu ubora wa misosi ya hizo bar. Kwa mfano 4040 pub, misosi ya hovyo sana.

Siku ya kwanza niliagiza ugali na makange ya kuku wa kienyeji. Msosi ulipokuja nyama ikawa na ladha chachu, nikauliza kama ni ya jana yake, nikaambiwa hapana ni ya siku hiyo.

Siku ya pili nikaagiza makange ya mbuzi, nikaletewa, nyama ina ladha ya uchachu, nikamuita mhudumu akashindwa kunipa majibu, nikaita mpishi akasema nyama haina tatizo labda tatizo liko kwenye nyanya, maana wanatumia nyanya za kopo.

Baada ya kuniambia kua wanatumia nyanya za kopo hata ham ya kula ikaniishia, nikalipa nikaendelea na mambo yangu. Binafsi hapa Bongo siwezi kula vitu vya kopo, bado tuna vitu fresh vingi sana. Nyanya fresh zinaoza Buguruni au Kariakoo sokoni alafu mtu unapikia nyanya za kopo?

Binafsi nikahitimisha kua Bar za Tabata kwa ubora wa misosi bado sana, bado hawajafikia misosi tunayokula Bar za mwenge au Kinondoni.

Kwa upande mwingine hata yale mambo yetu, watoto ni wa kawaida sana. Mimi nikienda bar naangalia misosi na totozi mara moja moja tu maana sinyi pombe na sijawahi kunywa na sina mpango wa kunywa.
nyinyi ambao hamnywi pombe ndo mnaosababisha bei za toto kupanda.
 
Hapa tutabishana kama misukule mkuu.
Mimi ni mlaji na naomba niweke wazi huwa napenda kupika tokea enzi za ujana wangu. Mara nyingi nimekuwa nikikutana na Makange ya kuku walioharibika yamejazwa ndimu/limao kupita kiasi. Kuna Bar fulani (jina kapuni) maeneo ya Ubungo niliwahi kula Makange ya kuku nyama ilikuwa inateleza kama mlenda, ikiwa imejazwa ndimu na tangawizi kupunguza harufu. Anachoeleza mleta mada kinafanyika sana kwenye mabaa, haswa ukiwa mteja mgeni.
We unakula?nipe Recipe ya makange yoyote maana tofauti huwa ni nyama tu.We unapenda kupika toka utotoni me nilikuwa chef sio mpishi,chef for 17 yrs na mpishi for 5 years.
 
MTU MZIMA BADALA AOE APIKIWE ANAZUNGUKA KWENYE MABAA KUTAFUTA CHAKULA.KAMA KUOA KAZI SI UPIKE KWAKO AU UTAFUTE MDADA WA KAZI.
NA KAMA UMEOA BASI NI WALE WABABA WANAOKULA MCHEMSHO BAR HUKU KWAKE WAMESHINDIA UJI
 
We unakula?nipe Recipe ya makange yoyote maana tofauti huwa ni nyama tu.We unapenda kupika toka utotoni me nilikuwa chef sio mpishi,chef for 17 yrs na mpishi for 5 years.
Ndio maana nilisema hapo awali "Hapa tutabishana kama misukule mkuu" to be exact.
Umeshinda Chef wa 17yrs.
Hii ni sawa na mtu analeta mada ya kwamba amepata ajali kwa sababu breki zimefeli, halafu mtu mwingine anakuja na kubisha ya kwamba haiwezekani breki zifeli bila kutoa sababu na vielelezo vya msingi, bali tu ni kwa sababu yeye ni makenika kwa miaka 28.
 
Umesema uchachu,nikakuambia labda lingine lakini ili pishi la makange likamilike kati ya viungo,kimoja wapo ni lamau au ndimu mkuu,mimi si shindani.Kama unakumbuka nilisema inawezekana alizidisha ndimu kwenye kipengele cha kuweka ndimu.
 
Back
Top Bottom