Baa na vilabu kufungwa saa tatu usiku; tuko serious?

Baa na vilabu kufungwa saa tatu usiku; tuko serious?

Mnaoshabikia funga funga ni wapumbavu, kama mnachotamani mko serious ombeni usafiri wa umma uzuiwe huko ndo kuna msongamano wa kugusana ana kwa ana na sio baa, halafu baada ya wiki mtakuja kuomba poo wenyewe
 
Sasa mkuu zikifungwa moja kwa moja wale dada zangu wapendwa wanaofanya kazi huko watakula nini?
 
Kuna watu wana familia wanaishi kwa kuendesha hizo baa...
Jinsi janga la CORONA lilivyoshughulikiwa na serikali ya Tanzania imeonyesha wazi kipi hasa ni kipaumbele cha serikali hii. Ni dhahiri Wananchi si miongoni mwa vipaumbele hivyo. Ni kweli kuwa total lockdown haina uhalisia na maisha ya mtanzania lakini Bar zina athari gani endapo zitafungwa kabisa kwa kipindi hiki. Anaehitaji kunywa anunue akanywe kwake. Hii haitamuathiri mmiliki wa bar kumuondoshea kipato chake wala kumhini mnywaji asiyeweza kukaa bila pombe.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Wacha tuendelee kujivutavuta, ila nasema itafika hatua baa, shughuli za ibada mikusanyiko misibani nk vitafungwa!sifurahii ila ni hatua za lazima. Dunia inaposisitiza lockdown lengo iondokane na gonjwa ili kwa pamoja, na wasi wasi tutaongoza kwa kuadhirika kwa Africa mzima na kupelekea kutengwa sijui hali itakuwaje, na lazima awepo wa kulaumiwa!
Tunakoelekea tutapigwa Lockdown na jumuia ya kimataifa. Kama tutaendelea hivi ugonjwa utaendelea kuwepo kwetu wakati maeneo mengine duniani umedhibitiwa.

Nchi nyingine wataendelea kufanya biashara baina yao isipokuwa sisi, hapo ndipo tutakapojua kuwa dharau zina madhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilala imepigwa marufuku kabisa mtu kukaa bar
Hawa nao wanatuchanganya kila kiongozi anapokuja na utaratibu wake, hapa inatakiwa itoke statement ya jumla kwa nchi nzima, kwani ni tatizo la nchi nzima, sio nusu nusu!!!
 
Bar na klabu za pombe inatakiwa kifungwa kabisa kipindi hiki, mchezo wa pool table upigwe marufuku.
Watu wacheza pool table huko bar na kwenye vilabu vya pombe
 
Ndio Viongozi wetu vijana ambao Kuna jamaa alifungua uzi kuwasifia,,Iyo habari nlimsikia Jana mhe. Albert akisema kuwa baa zote zifungwe saa tatu usiku kwa kuwa kuanzia saa tatu usiku wanywa pombe wanakuwa wamelewa na kuanza kushikana🤣🤣🤣 Duh nkasema yani RC anajenga hoja Kama hii si Bora tu angekaa kimya.
Siyo lazima wote waongee wengine wafunge tu midomo yao Mana kila wakiongea 🙈🙈🙈

Huyu RC huwa namfananisha na Bashite... Full mihemko katika matamko na maamuzi yake
 
Back
Top Bottom