msem
JF-Expert Member
- Nov 7, 2015
- 1,833
- 1,628
Siku za karibuni tumesikia tamko la serikali kupitia baraza la mazingira (NEMC) likitoa tamko la kukazia marufuku ya kelele katika makazi ya watu na kwamba atakayekwenda kinyume atachukuliwa hatua kali.
Katika hili tunaipongeza serikali lakini tunaiomba serikali "kukaza buti" katika kanuni na sheria zake zinazokataza uwepo wa vitu hivi kwenye makazi ya watu kwani athari zake ni kubwa katika jamii,kwa uchache wa kuzitaja kero hizo ni kama kelele zinazobughudhi wanafunzi wanaojisomea majumbani na hata wagonjwa waliopumzika,mmomonyoko wa maadili kwa watoto wanaoishi jirani na baa hizi,taka zinazotupwa na kuzagaa hovyo katika maeneo jirani n.k.
Nionavyo mimi udhibiti wa vitu hivi kwenye makazi ni rahisi sana( kama kweli serikali ina nia ya dhati kutatua tatizo hili) na kama kukiwa na ufuatiliaji makini ndani ya masaa 24 vitu hivyo vitabaki kuwa historia kwenye maeneo ya makazi;kwa mfano,baraza la mazingira lingeweza "kuwatask" wenyeviti wa serikali za mitaa wakishirikiana na mabalozi wa nyumba kumi kuhakikisha kwamba wanatoa taarifa mara moja kwenye baraza pale inapobainika uwepo wa vitu hivi kwenye mitaa yao ili kwamba kama kitu cha namna hiyo kitaonekana kwenye mtaa husika basi viongozi hao wa mtaa wachukuliwe kuwa ni majipu yanayostahili kutumbuliwa mara moja,au kama viongozi wa mtaa wameshareport NEMC nayo ikashindwa kuchukua hatua basi ijulikane kuwa NEMC nayo ni jipu.
Kasi inayotumika kudhibiti ujenzi holela ingetumiwa na NEMC kwenye kero hii nadhani serikali ingekuwa imeshafunika "chapter" hii,lakini tumebaki tunaulizana wataanza lini manake tangu tangazo kutoka mpaka leo hatuoni utekelezaji.
Tuna imani na serikali yetu,tuna imani kwa usikivu wake italifanyia kazi tatizo hili,pamoja na kwamba wapo watakaoumia lakini ni wachache kulinganisha na wengi wanaoumizwa na hili.