Azzani Zungu Atukanwa Na Wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azzani Zungu Atukanwa Na Wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuandamane, Apr 19, 2008.

 1. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mbunge alalamikia kutukanwa na wananchi
  JIBU LA SWALI LA MBUNGE JIMBO LA ILALA

  MBUNGE wa Ilala, Musa Azzan Zungu (CCM), amelalamikia kutukanwa na wananchi wake kutokana na kutokarabatiwa kwa Barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam, ambayo ni kero kwa wananchi hao.

  Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, mbunge huyo alisema kuwa ubovu wa barabara hiyo umekuwa ukimsababishia matatizo na kutoelewana na wananchi wake, ambapo baadhi yao wamefikia hatua ya kumtolea lugha ya matusi kutokana na kutokarabatiwa kwa barabara hiyo.

  Aliiomba serikali kutoa kipaumbele kwa barabara hiyo muhimu na yenye historia katika nchi, ambayo pia itasaidia kuwapunguzia kero wananchi katika jimbo lake.

  “Hivi mimi mbunge natukanwa kwa kosa gani hasa? Naomba serikali iingilie kati ujenzi wa barabara hii na iitazame kwa jicho la huruma,” alisema.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Celina Kombani, alisema kuwa serikali ikipata fedha itatoa kipaumbele katika barabara hiyo, ili kumsaidia mbunge kuepukana na matusi hayo ya wapiga kura.

  Swali hilo la nyongeza liliulizwa kufuatia swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Masasi, Raynald Mrope (CCM), aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuzifanyia ukarabati barabara za Masasi na zile zilizopo Masasi Magharibi.

  Akijibu swali hilo, Kombani alisema katika mwaka wa fedha 2007/08, fedha zimetolewa kufanya matengenezo ya kawaida kwa kilometa 488 kwa gharama ya sh milioni 327.5, ambapo matengenezo hayo yatalenga sehemu korofi, madaraja, makalavati na matengenezo ya muda maalumu.  Maoni ya Wasomaji

  khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.... yani kumbe mpaka wabunge watukanwe ndio barabara ipewe kipaumbele kutengenezwa?????????

  jamani tunakwenda wapi
   
 2. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Kumbe solution hapa ni kuwatukana hawa jamaa ndio watafanya kazi sio? Kwa maana hiyo bila kutukana na kulalamikiwa wao wataendelea kula pesa za walipa kodi kama kawa sio?

  Haya bwana haya ni maneno ya mbunge na majibu halisi ya waziri wetu jamani, huyu waziri anadhibitisha kuwa mkitaka kupata huduma yoyote katika eneo lenu, mtukaneni mbunge jamani

  Ndio Tanzania yetu hii, na hawa ndio viongozi wetu, reflection yetu wenyewe, kwa maana hiyo nasisi ndivyo tulivyo, haya kazi hipo hapo
   
 3. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Kwahiyo hiyo barabara itajengwa kuepusha matusi kwa mbunge na siyo kwa manufaa ya wananchi???. ina maana matusi yasipokuwepo tena hakuna haja ya hiyo barabara kujengwa. jamani tuna pumba si mchezo
   
Loading...