Azinduka Baada ya Miaka Mitano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azinduka Baada ya Miaka Mitano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon ambaye alizimia na kuingia kwenye hali ya koma ya kutokujitambua tangu mwaka 2006 ameanza kuonyesha dalili ya kuzinduka.
  Waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon mwenye umri wa miaka 82 ambaye miaka mitano iliyopita amekuwa akiitumia hospitalini kwenye chumba cha watu mahututi akiwa hajitambui akiishi kwa msaada wa mashine, ameanza kuonyesha dalili za kuzinduka.

  Sharon ambaye aliiongoza Israel kuanzia mwaka 2001 hadi 2006, kwa miaka mitano sasa amekuwa usingizini bila ya kuonyesha dalili yoyote ya kujitambua.

  Sharon alikumbwa na ugonjwa wa kiarusi januari 4 mwaka 2006 ambapo ubongo wake ulipata madhara makubwa.

  Akiongea jana kwenye televisheni ya taifa ya Israel, daktari maalumu wa Sharon, Shlomo Segev alisema kuwa kwa mara ya kwanza waziri mkuu huyo wa zamani amefungua macho yake baada ya kusikia watu wakizungumza pembeni ya kitanda chake.

  Hata hivyo, mshauri mkuu wa zamani wa waziri mkuu huyo, Raanan Gissin, aliliambia shirika la habari la AP kuwa hakuna mabadiliko yoyote ya hali ya Sharon.

  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
Loading...