Azimio la Beijing ndio anguko la mwanamke

Azimio la Beijing ndio anguko la mwanamke

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii imesema nchi ya Tanzania katika kipindi cha miaka 30 ya azimio la Beijing imefanikiwa kutekeleza malengo ya mkutano wa Beijing kwa mafanikio, ikiwemo kuongeza idadi ya wanawake katika vyombo vya maamuzi.
image1024x768.jpg


Habari hii ni njema sana kwa wanawake ambao ni fighters, namtazama Dada yangu Joyce Kiria akiwa na furaha sana kuona habari hii, nawatazama wale walimu wa masuala ya Gender Equality kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
5ec.jpg


Ila kuna maswali ambayo sidhani kama yanaulizwa na wadau wa maendeleo, sijajua hawawezi kuhoji maswali haya kwa sababu ya uoga ama kulinda masilahi (ugali).

1. Utofauti ya Blue Collar Job na White Collar Job.
Ukitazama mlengo mkuu wa Azimio la Beijing ni katika kumpa nguvu mwanamke aweze kupata nafasi kwenye nyanja kadha wa kadha ndani ya jamii, sawa na mwanaume, wao wanasema iwe 50/50, ukitazama manifesto zao zimezungumza sana umuhimu wa kumpa nguvu mwanamke.
images - 2025-03-29T231750.192.jpeg


Ila mkazo mkubwa umewekwa katika zile nafasi ambazo ni White Collar Jobs, nafasi ambazo kimsingi ni nafasi za maamuzi, sio ajabu kuona wakihubiri wanawake wapate nafasi za Uongozi pamoja na nafasi za maamuzi, aidha we Mkurugenzi Mtendaji, ama Afisa Mtendaji.
image1024x768 (1).jpg


Tunasahau kuwa hizi Blue Collar jobs ambazo kwa 80% wamejaa watoto wa kiume kwanini hazizungumzwi na viongozi kuwa ziwe na 50/50? Kwanini viongozi hawazungumzi na watoto wa kike kuwa wanaweza kwenda kufua vyuma? Kwanini iwe ni kwenye white collar jobs pekee?
5ec.jpg


Vyoo vyetu majumbani vikiziba ni wazi kuwa mtaalamu wa kujua namna bora ya kuzibua uchafu wengi wao ni wanaume! Gari lako lilivyopata hitilafu ya engine wangapi fundi ambaye alikuhudumia alikuwa mwanamke?
images - 2025-03-29T232614.502.jpeg


Kukiwa na uhalifu ama majambazi ni mara ngapi umepata kuona kikosi kazi cha polisi ama Kikosi cha FFU kikiwa na wanawake tupu kikituliza ghasia? Kuna mdau aliwahi kuniuliza kwanini benki kuu hazina askari polisi wakike?
images - 2025-03-29T232710.605.jpeg


Swali ambalo natamani kufahamu, kwanini kuna nguvu kubwa kwenye nafasi za maamuzi pekee?

2. Umuhimu wa maadili na familia (ndoa).
Nadhani katika vitu ambavyo viongozi wengi duniani wameshindwa kabsa kuzungumza kwa uwazi ni kuwaeleza ukweli kuhusu maadili pamoja na umuhimu wa kuwa na familia pamoja na ndoa. Hakuna afya yoyote kuwahubiria watoto wetu wa kike walio na miaka 20-26 kuwa wasome kwa bidii ili wapate kazi nzuri kama mtasahau wanapaswa kuishi.
images - 2025-03-29T232710.605.jpeg


3. Uwiano wa 50/50 unazidi kuwa mgumu.
Namibia ni mfano wa taifa ambalo limepata kuwa na viongozi wengi wanawake, suala ambalo limeonekana kama ni hatua kubwa sana, ila chukua picha, Rais ni mwanamke lakini pia Waziri ni Mwanamke, Mshauri wa Rais ni mwanamke, **Shughuli yake sio ya kitoto. Siku kikiumana je watakubali kuwa wao ndo wamesababisha au wanaume?
images - 2025-03-29T232421.252.jpeg


Ni miaka 30 ya azimio la Beijing miaka 30 ya moto sana kwa wanawake ambao wamejivika kiburi na majivuno, ni miaka 30 ambayo tumeshuhudia idai kubwa ya ndoa zikivunjika bila sababu za msingi

Ni miaka 30 ambayo ndo tumepata single mothers wengi ambao wana nafasi za maamuzi, ni miaka 30 ya moto sana katika malezi ya watoto, ila kubwa zaidi ni miaka 30 ambayo tusipokuwa makini wanawake wanaenda kulia na kusaga meno kupita maelezo.
image1024x768 (1).jpg


Ni miaka 30 ambayo wanawake wenye nafasi za maamuzi hawana tena muda na familia zao, **ni rahisi sana kwa kidada kilichotoka Iringa kumchukua mume wa Mtendaji Mkuu wa shirika fulani, kwa sababu tu ya Attention na heshima.

KWA BAADHI YA WASOMI WALIOPO VYUO VYA MAREKANI NA ULAYA WAMEONESHA WAZI KUWA AZIMIO LA BEIJING NI MKAKATI MWINGINE BORA WA KUFUTA KIZAZI CHA WANAUME.
 
Umetumia muda mrefu sana kuandika lakini umeandika upuuzi tupu mkuu. Mpaka dunia inaisha hakuna anguko lolote la jinsia yoyote litakalotokea. Mambo yapo yalivyo na yatabaki ya livyo. Jambo la msingi ni kila mtu kufanya kazi wake kwa waume tujenge uchumi wetu
 
Mw
Umetumia muda mrefu sana kuandika lakini umeandika upuuzi tupu mkuu. Mpaka dunia inaisha hakuna anguko lolote la jinsia yoyote litakalotokea. Mambo yapo yalivyo na yatabaki ya livyo. Jambo la msingi ni kila mtu kufanya kazi wake kwa waume tujenge uchumi wetu
Mwanaume anaetetea hizi harakati ni shoga...


Wewe ni shoga
 
Wanaume tumevunga tu tukijua wanachokitafuta watakipata... Itafika wakati tutaishi kama wanyama kiasi kwamba baba ukishatia mimba unapita zako hivi

Mwanaume akiona anasumbuliwa anaondoka kwa amani kabisa wala hutoona akigeuka nyuma
 
Umetumia muda mrefu sana kuandika lakini umeandika upuuzi tupu mkuu. Mpaka dunia inaisha hakuna anguko lolote la jinsia yoyote litakalotokea. Mambo yapo yalivyo na yatabaki ya livyo. Jambo la msingi ni kila mtu kufanya kazi wake kwa waume tujenge uchumi wetu
Soma upya halafu acha kushirikia mawazo yako! Ruhusu mawazo mapya Mkuu
 
Wanaume tumevunga tu tukijua wanachokitafuta watakipata... Itafika wakati tutaishi kama wanyama kiasi kwamba baba ukishatia mimba unapita zako hivi

Mwanaume akiona anasumbuliwa anaondoka kwa amani kabisa wala hutoona akigeuka nyuma
Mbona hayo wanaume wanayafanya tangu enzi na enzi hata kabla ya hayo mambo ya Beijing? Usitafute visingizio.
 
Back
Top Bottom