Azimio hili asingepona mtu Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azimio hili asingepona mtu Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Apr 16, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  AZIMIO LA ARUSHA


  Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka
  29/1/67, inaazimia ifuatavyo:-

  A. VIONGOZI

  1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au
  mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au
  kikabaila.
  2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.
  3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.
  4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi
  5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
  6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu
  ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
  vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya Kiserikali.  wana JF hakuna mtu ambae angepona hapa,mwalimu na wenzake waliona mbari sana,cha kushangaza wanaopenda hayo wakaja na AZIMIO LA ZANZIBAR
   
 2. s

  sanjo JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kati ya vitu vya maana ambavyo watawala wetu wameamua kuvitupa ni Azimio la Arusha, Miiko ya uongozi na kufuta Jeshi la Kujenga Taifa kwa vijana wanaosubiri kwenda Vyuo vikuu.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Wanatengeneza shimo ambalo watakuwa wa kwanza kutumbukia.
   
 4. Sanja

  Sanja JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Mkuu waliona mbali sana,kila kitu siku hizi partial unaenda ofisi ya serikali unakuta mtu anaongea na simu zaidi ya nusu saa anaulizia miradi yake. Kwa azimio la Arusha mengi ya matatizo ya ki uongozi tusingekuwa nayo sasa.
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Ndio maana marehemu Nyerere alikuwa anasema kuwa kila akilisoma azimio la Arusha na kutafuta kosa la kufanya kutupwa halioni. Lakini huo ulikuwa ni kushindwa kwa viongozi wetu na tamaa ya utajiri sasa wanatafuta mpaka ambao sio halali .
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa walikuwa magenius yani walikutana kwa siku nne tu lakini walikuja na maamuvi ya maana sana. Hawa viongozi wetu wa leo ambao pamoja na kulipana posho kila wakikutana hakuna cha maana wanachofanya kumsaidia mwananchi.
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kiukweli kama ulivyosema,uongozi wa Mwal na wenzake wa kipindi hicho ulikuwa na lengo la kuwakomboa wananchi na kama kweli tungelifuata AZIMIO LA ARUSHA maisha haya labda yangekuwa na utofauti kidogo
   
Loading...