Uchambuzi wako una kasoro ya kutoihusisha kabisa Mtibwa ambayo ina pengo la pointi nane dhidi ya Simba. Maana yake ni kwamba hata kama Simba itazifikia zote Azam na Yanga, bado itakuwa ni nyuma ya Mtibwa. Huenda sare ya leo ni mbaya zaidi kwa Simba kuliko kama timu mojawapo ingefungwa, kwa sababu hakuna kati ya hizo iliyopunguza pengo la pointi zake na Simba. Wenye uelewa wa hesabu za uwezekano (probability) watajua kwamba uwezekano wa Simba kufanya vizuri kuanzia sasa, huku Azam, Yanga na Mtibwa zote kwa pamoja zikifanya vibaya ni chini ya asilimia hamsini. Aidha, utabiri wako hauzizingatii kabisa timu kama Ruvu JKT na Coastal zilizo juu kwenye msimamo wa Ligi kuliko Simba. Ingawa zenyewe zinatofautiana na Simba kwa pointi kiduchu, uwezekano wa zote hizokufanya vibaya huku Simba pekee ikiendelea kufanya vizuri naoni mdogo pia. Ni kweli timu zote hizo zitapokutana zenyewe kwa zenyewe huwa zinaji-offset, lakini bado kufungwa kwa mmoja ni kushinda kwa mwenzake. Namna pekee ambayo Simba inaweza kupata nafasi za juu ni kwa mkono usioonekana kuingilia matokeo ya kila mechi ili yaisaidie Simba, mpaka itapofanikiwa kuingia kwenye kundi la watatu wa juu. Lisilowezekana kwa mwanadamu, kwa Mungu lawezekana.