Azam Two wanaonesha mchakato mzima wa uchaguzi Dodoma lakini TBC bure kabisa

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Imenishangaza Azam Two kurusha live na kila hatua ya kinachoendelea Dodoma, TV ambayo bila kulipia huoni lakini li TV letu la Taifa liko DW sijui wapi naona wazungu tu. Mahojiano kati ya Kingunge na Chaz Hilaly yalikuwa murua kabisa na Kingunge kasema kilichotendeka si haki na katoa ushauri mzuri kwa ccm wenzie. Hii TBC waala.....

ANGALIENI AZAM TWO RAHA TUPU..... Wassira amekimbia waandishi.

by GHOSTRIDER|
Hakika tangu nimeachana na DSTV Mmekuwa msaada mkubwa Sana kwangu binafsi na jamaa zangu kupata Habari, burudani na mengine mengi kede wa kede.

Haya si muhimu Kwa Leo; lililonisukuma kuandika uzi huu ni baada ya kutathimini Kwa ukaribu matangazo yenu ya Shughuli Za CCM huko Dodoma.

Awali nilipata hofu juu ya matumizi ya TV mpya Kwa masilahi ya Kambi fulani katika mchakato huu; niwapongeze mpaka dakika hii mmesimamia weledi Kwa kuwa balance, fair na very Objective.

Siamini sana kama Ivona kuchelewa kuja Dar Es Salaam kulidumaza kipawa chako; huu ndio ulikuwa wakati wake bila shaka Kwa mapenzi ya Manani, umeacha UCCM wako na umeitendea haki Taaluma.

Mmetufanya tuliopo mikoani kuhisi Kama tupo Dodoma Kwa namna mlivuotuhabatisha Kwa mtandao safi na wanahabari Mahiri Muhuza, Nurdin, Charles, Uwesu na wengine wote wanaoshiriki.

My Take:

Msiishie Kwa CCM tu kubalance muktadha wa kisiasa na UKAWA wapewe coverage Kama hii hata Kama itakuwa haina mbwembwe Kama za CCM

Naamini mtafanya hivi hata katika Uchaguzi Mkuu, Kampeni zote, upigaji kura hadi kuhesabu matokeo Kama Slogan yenu nilivyoiona Azam TV Kituo chako cha Uchaguzi.

Kwa haya machache niliyoyaona kwenye coverage hii ya CCM niwashauri wakati wa Uchaguzi Mkuu toeni huduma hii hata kwenye community Centers huku mikoani kwa kuweka big Screen ili kuwaunganisha watanzania wote ktk Uchaguzi huu wa kuhistoria na Mabadiliko Tanzania.

Endeleeni kuwa fair Kama hivi watazamaji wenu tunajenga Imani kwenu.
 
tbc wamemaliza mahojiano na nape kasema bado hawajapata majina matatu wakipata ndipo watajiunga live kutafuta jina moja.kuwa mpole
 
JF rudisheni accessibility ya JF kwa guest? Kwa nini muda huu tu?, mbona siku zingine access ipo?

Aya senior member ngoja nimwambie mhusika moja kwa moja kama kuna sababu maalum nitakujuza. Hata hivyo jam ni kubwa wakiaccess wote kusomeka itakuwa ngumu.
 
Hakika tangu nimeachana na DSTV Mmekuwa msaada mkubwa Sana kwangu binafsi na jamaa zangu kupata Habari, burudani na mengine mengi kede wa kede.

Haya si muhimu Kwa Leo; lililonisukuma kuandika uzi huu ni baada ya kutathimini Kwa ukaribu matangazo yenu ya Shughuli Za CCM huko Dodoma.

Awali nilipata hofu juu ya matumizi ya TV mpya Kwa masilahi ya Kambi fulani katika mchakato huu; niwapongeze mpaka dakika hii mmesimamia weledi Kwa kuwa balance, fair na very Objective.

Siamini sana kama Ivona kuchelewa kuja Dar Es Salaam kulidumaza kipawa chako; huu ndio ulikuwa wakati wake bila shaka Kwa mapenzi ya Manani, umeacha UCCM wako na umeitendea haki Taaluma.

Mmetufanya tuliopo mikoani kuhisi Kama tupo Dodoma Kwa namna mlivuotuhabatisha Kwa mtandao safi na wanahabari Mahiri Muhuza, Nurdin, Charles, Uwesu na wengine wote wanaoshiriki.

My Take:

Msiishie Kwa CCM tu kubalance muktadha wa kisiasa na UKAWA wapewe coverage Kama hii hata Kama itakuwa haina mbwembwe Kama za CCM

Naamini mtafanya hivi hata katika Uchaguzi Mkuu, Kampeni zote, upigaji kura hadi kuhesabu matokeo Kama Slogan yenu nilivyoiona Azam TV Kituo chako cha Uchaguzi.

Kwa haya machache niliyoyaona kwenye coverage hii ya CCM niwashauri wakati wa Uchaguzi Mkuu toeni huduma hii hata kwenye community Centers huku mikoani kwa kuweka big Screen ili kuwaunganisha watanzania wote ktk Uchaguzi huu wa kuhistoria na Mabadiliko Tanzania.

Endeleeni kuwa fair Kama hivi watazamaji wenu tunajenga Imani kwenu.

Adios
 
Mnaosema rekoded anglieni mahojiano na watu tofauti acheni..............kukariri tv yetu tbc kama kawaida yake matatizo.
 
Mkafanye kazi wenzenu wapo kwenye usahili kutafuta ajira zao mnakaa kuwashangilia.Wewe hapo huna cha kuchangia utake usitake
 
Azam TV kageuka kuwa TV ya Taifa; hongereni Sana Viongozi wa Chombo hicho Bw. Tido Muhando na Yahaya Mohamed( japo umekimbia JF Siku hizi). Bakhresa Group kweli no compromise in quality
 
Server itakuwa imeelemewa. Na hizi ndo faida za kuwa member. Wenye Azam TV wanapata taarifa toka Azam TWO na waliobaki mitandaoni ni JF kwingine ngonjera tu
 
Back
Top Bottom