Azam TV, wizi kwa wote

Azam TV, wizi kwa wote

Omwami Nshomile

Senior Member
Joined
Jan 26, 2015
Posts
132
Reaction score
28
Azam TV walisema wana aina moja ya kifurushi ambacho cost yake ni Tsh 12500. Leo bila ya taaarifa yoyote wanapandisha kutoka 12500 mpaka 20000.


Nawaomba mrudishe 12500 yangu nkanunue vingamuzi vya elfu 4000
 
Kya kya kya. . . .. hivi na wewe uliamini waliosema ivo. . ..after all ni wafanya biashara tu nao
 
Wana vifurushi aina tatu vya Tsh 10,000 ,15,000 na 20,000 kile cha awali 12500 ndio 15000 kwa sasa na wameondoa baadhi ya channel na kuipeleka kwenye kifurushi cha 20,000.Kilichoniudhi hawakutangaza hiyo bei mapema bali walisema watafungua channel kama za BarcaTv na Liverpool TV na tukifungua kuanzia March 1,tutaona hizo channel zilizoongezwa ,na hawakusema hizo channels zitakuwa kwenye kifurushi kipya cha 10,000,tayari wameshalewa sifa,mgema akisifiwa tembo hulitia maji.kiko wapi walichodai eti tv yao ni ya watu inayowajali watu wa hali ya chini?hichi kifurushi cha 10000 hakuna kitu,ni afadhali hata StarTimes cha 4000
 
Jana ndio nimelipia cha 12500,leo wameongeza bei? Ama kweli tajiri hana urafiki na maskini,
mwezi ujao nahama azam.
Azam count me out in april
 
Oh pole sana ila kwasasa hatuna cha waziri wala tcra maana haya makampuni yanafanya yatakavyo
 
Nina mpango wa kuuza king'amuzi changu cha ZUKU nijiunge na Azam, mnanifanya nijifikirie mara mbili.
 
Hivi king'amuzi cha Azam pamoja na kidish ni sh. ngapi nahitaji kukinunua
 
Mmewekewa chaneli ya madrid na liverpool ndo mlipe 12500? Bado ligi ya bongo unaona
 
Back
Top Bottom