Matangazo ya mpira wa ligi kuu Tanzania bara na yale ya nchi jirani yameanza kuwa na dosari. Kwa mtu mgeni anaefungua tv kuangalia matangazo hayo hataelewa kama matangazo hayo ni LIVE au RECORDED kwa sababu hayo maandishi siku hizi hayawekwi.
Hata matangazo ya ligi za nje kama Ulaya pia alama hizi haziwekwe.Hatujui sababu ya kuondoa maandishi hayo ni nini lakini AZAM tv wanapaswa watuiambie. Tatizo lingine ni lile liloonekana katika mechi ya Yanga na Mtibwa tarehe ya jana 5/02/2017 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Kamera za Azam tv zilitegwa nyuma ya bendera ya taifa iliokuwa inapepea uwanjani hapo. Matokeo yake badala ya kuangalia mpira vizuri bendera hiyo ulikuwa inafunika screen karibu theluthi moja na kufanya matangazo kuonyesha bendera badala ya mpira.
Kazi ya fundi mitambo aliekwepo pale inashangaza ni kwa nini hakuona kuwa kamera za Azam zinazibwa na hiyo bendera. Uongozi wa Azam unapaswa kuwa makini na wafanyakazi waliopewa majukumu ya kuwezesha chombo hiki kinachopendwa na wengi. Ni matumaini yetu kuwa kasoro hizi mbili zinarekebishwa haraka.