Azam TV: The most boring customer service in Tanzania

Azam TV: The most boring customer service in Tanzania

ngonani

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2012
Posts
1,366
Reaction score
599
Kuanzia juzi nimejaribu kuwasiliana na azam TV huduma kwa wateja kwa namba yao 0764700222 nikiwa na shida ya ufafanuzi wa jambo fulani,ukipiga unapokelewa na maelekezo yaliyorekodiwa kuwa kwa kiswahili bonyeza mbili etc.

Baada ya hapo unakuja muito wa simu na kisha yanakuja maelekezo yaliyolekodiwa kuwa subiri utahudumiwa hivi punde.

Maneno hayo yanajirudia na mtu unashika simu kwa nusu saa mpaka inakuwa ya moto, Hivi punde inakuwa mwaka.

Unakata simu na kujaribu tena baada ya saa moja hali inakuwa ileile.

Naomba mbadilike hii ni biashara, Mtapoteza wateja kwa ajili ya nyodo, Muwe kama Vodacom au mitandao mingine ya simu ambao wana respond haraka kwa calls za wateja.

 
Mkuu afadhali na ww umeliona hili..ki ukweli hawa jamaa wanatakiwa wabadilike bwana coz hii ni biashara..kuna siku nlipiga hizo namba hadi nikakasirika..wahusika boresheni Idara yenu ya custumer care haraka..
 
Hapo hujakutana na customer care ya makonda wa daladala...utajuta kuingia anga zao
 
We itakuwa ni mtu wa dar bila mnapenda sana kulalamika hata kwa mambo yasiyokuwa na msingi! huenda number yako walisha i note kuwa wew ni msumbufu na unawauliza maswali ambayo hayana msingi ndiyo maana wanakukaushia!
 
Hili ndio tatizo la sisi wa tz, kila anapokuwa mhudumu waki tz sehemu inakuwa shida sana, lia huyo huyo ukimpeleka akafanye kazi nchi za watu anajituma sana , yaani akishaajiriwa tu ,na kujiakikishia kuwa kuna vigezo vinamlinda asitimuliwe kwa haraka, basi ni uzembe kwa kwenda mbele.
 
Mnaongea sana bila kufikiri mada imekujaje, Customer care maana yake nn? na Customer service maana yake nini??

Hata kama mtu anapiga simu na kuuliza swali la aina yoyote ni wajibu wako kumsikiliza na kumshauri.

Mimi Azam wamenikera pia kwa suala la kupoke simu. mimi sipo dar kama Kaka Jambazi anavosema kua watu wa dar ndo wasumbufu.

Azam hadi leo wameshindwa kunibadilishia Receiver yangu kilichopigwa na radi.

Na kinachonikera ni Mawakala wao wa mikoani wanashindwa kuwacliana wenyewe na hatimae wanisaidie mimi mteja wao , either wanitengenezee au wanibadilishie receiver. sina hamu nao sasa unless otherwise
 
Achana na hao waswahili. Njoo Zuku. Huku wenyewe ndio wanakupigia mara kwa mara kukuuliza iwapo huduma ni nzuri na labda waongeze nini. Isitoshe haikatiki katiki kama Azam au DSTV Wakati wa mvua
 
kwanini kichwa cha habari usingetumia kiswahili? au sifa tujue unajua na kiingereza
 
Hahahaha mdogo mdogo wameanza ngwengwe kama za startimes, mtujuze wakati unasubirishwa wanakata credit? :biggrin:
 
Message naona imewafikia,jana niliwapigia tena walipokea muda huo huo na huduma niliyoitaji ikapatikana baada ya sekunde mbili,Asante sana JAMII FORUM
 
Hata mie nilipiga jana ikawa poa tu japo kweli huko nyuma ilianza zengwe,ila niwakumbushe kitu Azam .... studio zenu ziko poa sana so jaribuni kuweka na watangazaji wanaomatch na ubora was studio,si mbaya sana ila baadhi ya wanaokaa mbele ya camera zenu katika vipindi tofauti wengi wao hawawezi kuichangamsha studio,they rnt vibrant kama ilivyo kuweza kuichangamsha studio sometimes wanaweka sana sauti zao low pitch,not vocal enough.Kitu kingine,mbona watangazaji was kipindi kama taharifa za habari hambadilishi watu jamani toka mmeanza,jaribuni kuwarotate at least itasaidia
 
[FONT=times new
roman]Kuanzia juzi nimejaribu kuwasiliana na azam TV huduma kwa
wateja kwa namba yao 0764700222 nikiwa na shida ya ufafanuzi wa jambo
fulani,ukipiga unapokelewa na maelekezo yaliyorekodiwa kuwa kwa
kiswahili bonyeza mbili etc.

Baada ya hapo unakuja muito wa simu na kisha yanakuja maelekezo
yaliyolekodiwa kuwa subiri utahudumiwa hivi punde.

Maneno hayo yanajirudia na mtu unashika simu kwa
nusu saa mpaka inakuwa ya moto, Hivi punde inakuwa mwaka.

Unakata simu na kujaribu tena baada ya saa moja hali inakuwa ileile.

Naomba mbadilike hii ni biashara, Mtapoteza wateja kwa ajili ya nyodo,
Muwe kama Vodacom au mitandao mingine ya simu ambao wana respond haraka
kwa calls za wateja.
[/FONT]

mkuu mimi apa npokuangaika nao nimelipia kifurush cha 20000 wamenpa cha 10000
 
Kuanzia juzi nimejaribu kuwasiliana na azam TV huduma kwa wateja kwa namba yao 0764700222 nikiwa na shida ya ufafanuzi wa jambo fulani,ukipiga unapokelewa na maelekezo yaliyorekodiwa kuwa kwa kiswahili bonyeza mbili etc.

Baada ya hapo unakuja muito wa simu na kisha yanakuja maelekezo yaliyolekodiwa kuwa subiri utahudumiwa hivi punde.

Maneno hayo yanajirudia na mtu unashika simu kwa nusu saa mpaka inakuwa ya moto, Hivi punde inakuwa mwaka.

Unakata simu na kujaribu tena baada ya saa moja hali inakuwa ileile.

Naomba mbadilike hii ni biashara, Mtapoteza wateja kwa ajili ya nyodo, Muwe kama Vodacom au mitandao mingine ya simu ambao wana respond haraka kwa calls za wateja.

Jaribu ya kingereza mim huwa naongea nao upesi.
 
Tatizo kubwa hapa ni ajira za kujuana. Niliwahi mimi mwenyewe kwenda ofisini mwao na hayo unayoyasema yako hivyo.
Ukifika pale na kueleza tatizo lililokuleta pale unaangaliwa kama vile unam'disturb' tu. Wavulana kidogo afadhali lakini ninadhani hata vijikozi vya customer care wengine hawajawahi kwenda.
 
Back
Top Bottom