Azam Tv kurusha Mkutano wa Lowassa

Azam Tv kurusha Mkutano wa Lowassa

Status
Not open for further replies.

Super Handsome

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
3,844
Reaction score
6,468
Taarifa kutoka kwa "Wanyetishaji" ni kwamba kituo cha Televisheni cha Azam kinatarajia kurusha matangazo ya mkutano wa Mgombea Urais kupitia Ukawa Edward Lowassa kutoka viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dsm kuanzia saa kumi jioni!

Hutaki Unaacha!
 
Hivi best wewe uko upande gani?Mimi nilidhani uko na rafiki yako popoma ila kwa hii thread umenichanganya kidogo...
Hata hivyo asante kwa hii habari njema.
 
Ndiyo maana wamekata umeme!!!!!, nilikuwa najiuliza sababu ya kukata umeme muda huu nini kumbe ni lowassa.
 
Ocampo four,ITV ndio kituo ambacho kina wide coverage,UKAWA wafanye juu chini angalu mikutano miwili iwe live kwa kila week hadi siku ya mwisho kwani maCCM yanapata fursa ya kuwapumbaza dada na mama zetu kila siku Star TV!!

Napendekeza ITV japo matangazo yanaweza kushutiwa na Azam TV ila Azam hapatikani Ving'amuzi vyote ni hadi uwe na Azam TV ila ITV yupo kote na ni bure!!!
 
Hivi best wewe uko upande gani?Mimi nilidhani uko na rafiki yako popoma ila kwa hii thread umenichanganya kidogo...
Hata hivyo asante kwa hii habari njema.

Huwezi kunielewa hata siku moja kwa maana sieleweki! Cc GENTAMYCINE aka Gwakisa haha
 
Last edited by a moderator:
Kumbe ndio maana kinondoni nzima umeme umekatika muda huu
 
Na nyie mliokwenda kuwaona Lowasa na Sumaye pale Tanganyika Packers kweli hamjiulizi?Mawaziri wakuu ambao wameshindwa kufufua hicho kiwanda na leo wanaona poa tu kufanyia mikutano hapo,Wakati kiwanda hicho kingepunguza unemployment Tanzania.
 
Uulize na watanzania watakao wasikiliza nao hawaoni aibu? Alipoomba uwanja wa taifa mlimnyima akaomba jangwani mkaweka zengwe.
 
View attachment 293472
Lowasa na Sumaye ndo wamesababisha kuwepo na magofu kama haya badala ya viwanda

Lowasa na Sumaye wanatufanya watanzania hamnazo! kwa kuwa niko hapa jirani, ngoja nikasikilize utu.mbo wao sijui wataruhusu maswali! Na tunavyoendaga kuwashangaa utawasikia "Umeona nyomi"kumbe wengine tunawashangaa tu!
 
mbona una maneno ya ajabu?? Tangu lini waziri mkuu akalaumiwa kwa sababu ya rais?? Wa kuona aibu ni huyo raisi aliyekuweko madarakani si PM.
Tukuulize, weye jina lako litaharibikaje nyumbani kama una baba mwenye nyumba?
 
Na nyie mliokwenda kuwaona Lowasa na Sumaye pale Tanganyika Packers kweli hamjiulizi?Mawaziri wakuu ambao wameshindwa kufufua hicho kiwanda na leo wanaona poa tu kufanyia mikutano hapo,Wakati kiwanda hicho kingepunguza unemployment Tanzania.

Unapoteza muda tu ndugu, watu tulishafanya maamuzi long time. Tunasubiri tarehe ili kuweka kumbukumbu vizuri.

Mabadiliko hayazuiliki!
 
Azam Tv Matukio Ya Maana Hawaonyeshi ILA Haya Ya Kipuuzi Puuzi Kama Nyosso Kumpiga NDOLE Bocco,

Kiatu Kibaya Cha Msenegal Wa Simba N'diaye Na Misafara Ya Mzee Wa KUUKWEKA Lowassa Ndiyo Huwa WANAJITUMA Mno Kuionyesha. Anyway CCM Taratibu Sasa Tunaanza Kuwajua WANAFIKI Wetu.

Mwambieni Huyo MPEMBA Kuwa Lile File La Kesi Ya Ile Meli Iliyobeba UNGA Mbovu Wa NGANO Kipindi Kile Bado Halijafungwa Hivyo Aende ADO ADO La Sivyo TUTAKINUKISHA Kesi Iendelee TUHESHIMIANE Mjini Hapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom