Azam tufungulieni Channels Zingine kufidia "FTA" mlizoziondoa

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
Azam wana vifurushi mbali mbali,
Kuanzia Kifurushi 10,000/=, kuna cha 18,000/=, cha 23,000/= na 28,000/=.

Vifurushi vyote hivi vimeathirika kwa kuondolewa channels za hapa nyumbani, maarufu kama "FTA".
Sasa basi kwa kua kulikua na "Implied Contract" ya kulipia vifurushi ambavyo vimepunguzwa channels, inabidi mfanye "compensations" kwa kufanya "up grades" kwa kila alielipia.

Mfano alielipia kifurushi cha 10,000/= kwa mwezi apelekwe kifurushi cha 18,000. Yaani mumuongezee channels zingine kwenye kifurushi chake ili awe sawa na alielipia 18,000= ambae nae ataongezewa channels vile vile. Hii itajenga uaminifu wenu kwetu na itaondoa ile dhana kwamba kwa sasa mnatubia kutulipisha bei ile ile wakati vifurushi vimepunguzwa channels.

Nina imani ushauri huu utazingatiwa na Utawala wa Azam. Pia TCRA mnaweza kuuchukua huu ushauri mkakaa chini na kujadiliana na hawa Azam ili kuhakikisha haki za mtumiaji zinalindwa.
 
Habari za jioni bandugu!Mimi nipo Moshi
kwa sk za hivi karibuni ktk kingamuzi cha Azam channel nyingi za bongo zimekuwa hazionekani.Ningependa kujua sababu nini sanasana
 
A
Habari za jioni bandugu!Mimi nipo Moshi
kwa sk za hivi karibuni ktk kingamuzi cha Azam channel nyingi za bongo zimekuwa hazionekani.Ningependa kujua sababu nini sanasana
Kuna post nyingi sana hapa jf za kuhusu kngmz cha azam na zishatolewa ufafanuzi
Jaribu ku search
 
Nimeathirika sana na hii kitu, wiki ijayo acha nifunge cha Startimes hata kama kipo hafifu kimuonekano
 
Hivi hizi FTA zimeondolewa kimoja au hizo taratibu waki-clear wanarudi nazo?Kesho kifurushi kitaisha niko dilemma kama nilipie au nianze mchakato WA Startimes.
 
Hivi hizi FTA zimeondolewa kimoja au hizo taratibu waki-clear wanarudi nazo?Kesho kifurushi kitaisha niko dilemma kama nilipie au nianze mchakato WA Startimes.
Walioruhusiwa kua na hizi ni Continental, Ting na Digitek, so pengine wanataka tuhamie huko
 
Back
Top Bottom