Azam tatizo la kukabia macho ni kubwa mno

oladipo

JF-Expert Member
Mar 8, 2022
1,432
2,291
Nikiwa kama shabiki wa Azam nimesikitishwa mno na perfomance ya timu Yangu hasa kwenye ukabaji wa timu

Timu ya Azam linapokuja suala la ukabaji ni wachezaji wachache sana wanaotimiza wajibu wao inavyotakiwa

Leo hii Yanga wamepata alama tatu kwa sababu ya wachezaji wa Azam kukosa nidhamu ya ukabaji

Hebu angalia yanga walivyokuwa wanafika kirahisi golini kwa Azam bila kustruggle yaani wangekuwa makini wangeshinda hta goal saba

Azizi ki pekee yake alikuwa na short on target karibia saba alikuwa yupo huru mno shukrani kwa kipa vinginevyo leo ingekuwa aibu kubwa

Azam kuanzia mbele kwa Dube, Sopu sillah na Feisal hawa wote walikuwa wanawasindikiza Yanga kwenda golini kwao yaani hawakabi kabisa wanakabia macho

Leo kama Azam angeshinda mpira ungekuwa haujatenda haki kabisa!!
 
Yanga timu yangu imeshinda ila nimekereka mno, Kuna kaunta attack Yani wachezaji wa yanga wanne wako na beki mmoja wa Azam wakashindwa hata kutengeneza nafasi, azizi k alifanya heavy touch akapoteza muelekeo, yaani Hio ni dhambi kabisa kwenye mpira, 4 against 1 wanashindwa
 
Yanga timu yangu imeshinda ila nimekereka mno, Kuna kaunta attack Yani wachezaji wa yanga wanne wako na beki mmoja wa Azam wakashindwa hata kutengeneza nafasi, azizi k alifanya heavy touch akapoteza muelekeo, yaani Hio ni dhambi kabisa kwenye mpira, 4 against 1 wanashindwa
Yanga leo walikuwa washinde hata goli sita coz azam nidhamu yao ya ukabaji ipo chini mno

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Sio azam tu, ni timu nyingi tz, tizama singida kilichomkuta kule uarabuni.
Yaani ningekuwa kocha ningewaonyesha wachezaji wangu mechi ya mazembe na esperence jinsi mazembe walivyokuwa wanadiscpline kwenye ukabaji

Yaani walikuwa wakipoteza mpira wote wanarudi nyuma kukaba na kukaba wanakaba kweli na sio kukabia macho kama wachezaji wa kibongo

Warabu walipata ahort on target moja tu mechi nzima

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hata yanga hawakuwa kwenye form yao Yani timu zote zilikuwa zinakabia macho goli la kwanza la Azam uzembe sio technical yanga walikuwa wanakabia golini tofauti na wale wa mwanzo wanakaba kuanzia katikati,

Azam kidogo wanakaba ila wakichukua mpira wanakimbia kama wameshinda
Azam fighting spirit yao ipo chini mnoooo!!

Yaani wameridhika mno kama wanacheza mpira kujifurahisha na sio kazi

Namuonea huruma sana kocha wa azam
Anafundisha wachezaji ambao hawana njaa ya ushindi kabisa

Aziz ki leo alikuwa yupo huru kufanya atakacho wachezaji wa azam hata kumghasi walikuwa hawataki

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom