Ni kweli Simba na Yanga zimefeli kuidhoofisha Azam?

bujashi25

JF-Expert Member
Jun 17, 2013
623
112
Ukifumba macho na kuangalia miezi takribani sita au saba iliyopita unaweza leo hii ukabaki mdomo wazi, kipindi hicho Mtibwa sugar ilikuwa inaongoza ligi ya Tanzania na ndicho kipindi Mecky Mexime alikuwa anaonekana kocha bora mpaka wenye matege yakufikiri wakawa wanapendekeza apewe timu ya taifa.

Mwenyewe Mexime ndicho kipindi alichokuwa anaropoka hovyo na hata kufikia hatua kuwaponda makocha wenzake, lakini wachache tulibaki tu kumsikiliza na kujiuliza kwa ukocha gani alionao?

Lakini hivi tunavyozungumza Mtibwa inapigania kushuka daraja na Mexime mdomo ameufyata lakini pia ukifumba macho na kuiangalia ligi ya msimu uliyopita, utaona jinsi Mbeya city walivyoleta amsha amsha katika ligi ya tanzania na style yao yakurudisha wanachokipata kwa wananchi wahitaji.

Mashabiki wao walikuwa na style yakwenda mahospitalini kuwaona na kuwafariji wagonjwa na mwisho wa siku waliweza kujitolea kufanya usafi katika jiji lao, watu tukasema sasa timu ya kijamii imepatikana.

Lakini kilichotea hivi sasa kila mtu anashika kichwa, walianza kutimuana wenyewe kwa wenyewe, siasa za kimkoa zikawatafuna hatimaye wamepotea na usishangae msimu ujao tukawakuta wakiwa katika nafasi yakupigania kutoshuka daraja.

Haya siyo mapya kwa sisi tuliokula chumvi nyingi kidogo kuyaona katika ligi ya tanzania, kulikuwepo na timu nyingi tu za aina hii, kwa kawaida timu kama hizi, tunaziita “timu mlipuko”.

Walikuwepo kajumulo fc, chini ya tajiri wa kitanzania Alex Kajumulo ambaye maisha yake yalikuwa pale Marekani na ambaye alikuwa mwanachama wa Simba alikuja kwa mbwembwe kubwa, Tukuyu Stars, Parsons chini ya tajiri ambaye alikuwa anamiliki migodi ya dhahabu na alikuwa mwanachama wa Simba, ushirika Moshi, hawa wote walikuwepo na wamepotea… tatizo ni nini?

Tatizo kubwa linaloziathiri timu hizi mlipuko ni moja tu…nalo ni malengo yao yakuwepo ligi kuu malengo yao siku zote hayawi katika kuchukua kombe la ligi kuu bali malengo yao ni kuja kushindana na Yanga na Simba, hasa hasa Yanga, hapo ndipo wanapoanza wenyewe kujipoteza.

Ukiiangalia Azam fc utaona kama ni klabu ambayo ipo kisasa zaidi ni kweli ina kila kitu tena kuzishinda klabu nyingi na muda mwingine hata ulaya kwenyewe, lakini zaidi yakuchukua kombe la ligi kuu ya vodacom nini kingine hasa ambacho wanaweza kusimama mbele ya watu na kujivunia na utajiri wote ambao wanao?

Malengo ya uanzishwaji wa azam yalikuwa yapi? kwanza ieleweke Azam ni chimbuko la timu ya wafanyakazi wa Bakhresa Group of Campanies ambao waliamua kuunda timu yao kwa ajiri ya kujifariji baada ya kazi ngumu za kukanda unga wa chapati na kuuza juice, mwisho wa siku waliamua kununua haki za kipawa Combine fc, na rasmi kuanza kushiriki ligi za ngazi ya chini.

Mzee Bakhresa ambaye ni mshabiki na mwanachama mkubwa wa Simba alipoona mawazo yake yakuiendesha klabu ya simba kisasa yamekataliwa ndani ya Simba ndipo rasimi alipoamua kuwekeza nguvu kwa azam akiwa na lengo kuu lifuatalo; kuhakikisha azam na simba wanashika nafasi mbili za juu huku Yanga ikishika kuanzia nafasi ya tatu, ndipo alipokuja na sera zakubadilishana na kuuziana wachezaji wa simba kwenda azam na wa Azam kwenda Simba.

Hii ndiyo sumu kubwa ambayo Azam walijitengenezea wenyewe na kuamua kuinywa, ingawa Yanga ilipitia misukosuko mingi ikiwemo Azam kuingiza mkono katika mechi nyini za Yanga lakini haikusaidia kitu zaidi yakuiacha yanga ikiwa imara zaidi na kuendelea kubaki katika nafasi mbili za juu, huku swahiba mkuu Simba akibaki kupotea katika mbili bora

Maji sasa yamezidi unga kwa Simba wamechoka sasa nao wanaitaji kujikwamua kutoka katika aibu ya kila mwaka ya kukosa nafasi mbili bora ndipo tunapoona ndugu kwa ndugu wameanza kuombeana mabaya.

Simba sasa anamuombea Azam apoteze mechi zake ili apate nafasi ya pili na azam naye anamuombea simba apoteze mechi zake ili apate nafasi ya pili wote hawa hakuna anayemuombea yanga apoteze mechi zake kwa sababu wanajua wazi Yanga haiwezekani tena.

Azam kabla yakupambana na Yanga alipaswa kwanza kujua asili na chanzo cha mkubwa wake simba, Simba ni zao la yanga ata jina lenyewe la Simba lilipendekezwa na mwanachama namba moja wa Yanga mzee Karume rais wa kwanza wa Zanzibar siku zote ninawaheshimu Yanga,

Azam wasipobadilika kimtazamo nao watapotea na uwanja wa Chamanzi utabaki kama sehemu ya kuhifadhia makontena au maonyesho kuwa kulikuwepo na timu ya Azam dalili zinaanza kuonekana, hatua ya juzi, siku walipocheza na Mbeya city viongozi wao kutukanana hadi kushikana mashati ni dalili tosha.

Siku zote chenye nguvu kina maisha marefu na kinadumu
 
Kwa ukweli ndg umetueleza vizuri kabisa, kinacho iua azam ni kujidai ujamaa na Simba, hata wasimamizi wa hiyo timu hawana lolote zaidi ya kumtia hasara bakhresa.
 
tatizo la AZAM me nadhani linasababishwa na watu wanaoizunguka timu hii. viongozi na wadau wao hasa watangazaji wengi wa azam media wamejikita kwenye kusifia timu yao kwa sifa ambazo hata hawastahili. kwa mtindo huo bila shaka hata ushauri wanaoutoa kwa mmiliki wa timu ni wa kulenga kumfurahisha bosi ili waonekane wazalendo, badala ya kuongea ukweli.
lapili ni hili la kutaka kupambana na yanga na simba hususani yanga, me nadhan hawakufikiria vizuri. kwakuwa wao wana kila kitu walitakiwa kushawishi TFF kuruhusu timu zisajili wachezaji wa kigeni bila kikomo. kwa kufanya hivyo wangeweza kuwa na timu nzuri kama Mazembe
 
wangeingia kwenye ligi wakiwa na malengo yao wao kama wao Bila kujichanganya na mambumbumbu a.k.a mikia wangekua mbali sana lakin kuungana na wale PAKA SHUMI wa msimbazi ili kuidhoofisha YANGA ndiko kunakowaharibia
 
Azam inatakiwa isimame yenyewe kama Azam . Ushirika wao na Simba sasa umefikia kikomo. Nani ashike nafasi ya pili. Pia wameanza mambo ya ajabu. Kuzipa timu hela au kuziwezesha kwa namna yoyote ili ziikomalie Yanga kwenye mechi zake. Nashangaa kwa nini wasikomalie ushindi wa kwao? Kama wanaweza kuziwezesha timu ziikomalie Yanga, kuna ugumu gani timu huzo kuuza mechi kwa Azam?

Sasa ni dhahiri viongozi wake wameanza "uswahili" na bila shaka wanatafuna tu fedha ya tajiri wao. Wasije shangaa kutumia pesa sawa na TP Mazembe lakini wakabaki wa hapa hapa tu.
 
Azam na Simba wamekuwa na ushirika, kwa muziki wa Yanga ni lazima watafarakana tu ili kila mmoja afe kivyake.

Simba amejipanga kuifumua Azam ili apate nafasi ya pili, ushindi wa Simba utaifanya Yanga itangaze ubingwa mapema sana.

Hakuna shaka siku Yanga ikicheza na Azam, mikia wataishangilia Yanga ili wapate nafasi ya pili. Kwa kuwa Yanga atakuwa ametwaa ubingwa, mimi nitapenda Azam iifunge Yanga ili Simba atoke kapa tena ikiwa ni kisasi kwa Simba kwani mwaka jana walicheza kinazi na kufungwa na Azam ili kuikosesha Yanga ubingwa.

Ngoja tusubiri hadi mwisho tuone Simba ataishia wapi!
 
Hee!!,maelezo meeeengi,pumba tupu,hivii,Simba ishirikiane na Azam kuiua vyura fc kwa mantiku gani,yaani eti mtu utumie gharama kuubwa kuwa na timu na miundombinu yake kuimaliza vyura,khaa,mi naamini mmiliki wa Azam hadi sasa ana malengo mazuri sana na timu yake sema wachezaji ndio wanaomuangusha,haiingii akilini kutumia gharama kubwa kuanzisha timu halafu unaungana na timu nyngn kuiumiza timu nyingine,hayo ni mawazo mgando na ya kishabiki ya shabiki wa vyura fc
 
shafii dauda kaeleza ukwel kabsaa angekuwa Eddo kumwembe angeuma uma bila kujua anataka nn viongoz weng Wa azam wame kaa kinafki mnoo msikilize alivyo kuwa anachambua kusifia azam.
Kiukwel hela aliyo wekeza azam group kwenye tim ni nying mno tofaut na matokeo ayapatayo Azam wasipo kuwa makini watapotea kama Moro united a.k.a Zaragoza ya barabou
 
kuanzia leo nitakuwa nawaita PAKASHUMI Wa msimbazi naona umbumbumbu wenu unazidi kuongezeka badala ya kupungua
 
tatizo mambumbumbu fc wazee Wa kilimo kwanza hawataki kuelezwa ukweli sasa unabaki kujiuliza Haya mamtu yalikwenda shule kweli? Mbona hayataki kusikia ukweli wala kubadilika? Yaan yenyewe yanaamin katika ujinga Hata kama yanajua ukweli ulivyo Ndio maana yule mwenyekiti wao hakukosea kuyaita mambumbumbu
 
Watangazaji/wachambuzi wa azam tv ni wachumia tumbo wao style yao ni ile ya mtumikie ------ upate mradi wako wao siku azam ikicheza timu hata ikicheza vibaya wao wana kazi moja tu ya kuisifia mwisho wake wanasifia hata ujinga yanga daima mbele nyuma mikia
 
Maelezo marefu utumbo mtupu.. Nyie wengine tunawajua mmeanza kuipenda Yanga kwa sababu ya kufananisha bendera ya CCM tangu mko kijijini. Yanga utasema wanamafanikio gani zaidi ya kuchukua kombe la FAT na TFF mara nyingi.

Na mara zote huwa ni mbeleko ambayo YANGA hubebwa na TFF, angalia Ratiba ya ligi inavyopangwa utagundua hilo. Ndiyo maana YANGA haina mafanikio makubwa kulinganisha na SIMBA linapokuja suala la michuano yasiyoandaliwa na TFF.

Kwa rekodi hakuna michuano ambayo imeandaliwa nje ya TFF YANGA wakaizidi SIMBA kwa rekodi. Kuanzia CAF, CECAFA, Kombe la HEDEX, Muungano, ABC bank, Mapinduzi, taya yote.. Yanga inasubiri kwa Simba..

Tunajenga timu yetu kwa sasa,, so endeleni kubebwa na TFF yenu.. tukirudi ni 5 - O za mfululizo
 
Azam pamoja na investment kubwa waliyoifanya lakini jinsi wanavyoendesha timu hawana tofauti na Simba na Yanga
 
MFUKUZI; mkuu umesahau na ndondo cup, chandimu, chibuku maana hizo ndo saiz yenu...lakin unaikumbuka LIBOLO?
 
Last edited by a moderator:
yote ulisema tumekuelewa lakini kilichoikumba yanga ni kitu kibaya sana takribani miaka mingi lakini yanga ni timu kubwa isingeweza kufa kama ilivyokufa nyota nyekundu kazi imefanyika kubwa nyinyi endeleeni kushangilia
 
kuanzia leo nitakuwa nawaita PAKASHUMI Wa msimbazi naona umbumbumbu wenu unazidi kuongezeka badala ya kupungua

ita vyovyote vile utakavyopenda mkuu ila daima ukweli utabaki kuwa ukweli na pumba na mchele lazima vitatengana tu,mtoa mada ni msukule wa yanga kama ulivyo wewe mkuu
 
Maelezo marefu utumbo mtupu.. Nyie wengine tunawajua mmeanza kuipenda Yanga kwa sababu ya kufananisha bendera ya CCM tangu mko kijijini. Yanga utasema wanamafanikio gani zaidi ya kuchukua kombe la FAT na TFF mara nyingi.

Na mara zote huwa ni mbeleko ambayo YANGA hubebwa na TFF, angalia Ratiba ya ligi inavyopangwa utagundua hilo. Ndiyo maana YANGA haina mafanikio makubwa kulinganisha na SIMBA linapokuja suala la michuano yasiyoandaliwa na TFF.

Kwa rekodi hakuna michuano ambayo imeandaliwa nje ya TFF YANGA wakaizidi SIMBA kwa rekodi. Kuanzia CAF, CECAFA, Kombe la HEDEX, Muungano, ABC bank, Mapinduzi, taya yote.. Yanga inasubiri kwa Simba..

Tunajenga timu yetu kwa sasa,, so endeleni kubebwa na TFF yenu.. tukirudi ni 5 - O za mfululizo

Unajua avatar yako ina rangi zipi? Rangi ya Simba iko wapi hapo? Kwa kuwa wewe unapenda hiyo bendera ya Tanganyika kwa nini usiwe mpenzi wa hiyo CCM?
 
Unajua avatar yako ina rangi zipi? Rangi ya Simba iko wapi hapo? Kwa kuwa wewe unapenda hiyo bendera ya Tanganyika kwa nini usiwe mpenzi wa hiyo CCM?

Hebu ishughulishe akili yako kidogo, Si lazima rangi za timu ya taifa zifanane na Bendera ya nchi.. Niambie uholanzi rangi ya bendera ndiyo rangi ya jezi zao za taifa, Ujerumani pia jezi za timu ya taifa ni tofauti na bendera ya nchi..

Usikariri.. Bendera ya taifa ina maana zaidi ya mpira..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom