Ikiwa Takribani ni miaka 20 ya Mabadiliko ya kiteknolojia yaliyoleta huduma za Simu za mkoni nchini pamoja na Duniani kote kwa ujumla Tumeshuhudia mitandao ya Simu ikianzishwa na Kufanikiwa huku Kukiwa na ushindani mkubwa wa Kibishara.
Makampuni kama Vodacom, Tigo, Airtel, Halotel, TTCL pamoja na Zantel yanachuana vikali lakini soko bado linaonesha kuna opportunities nyingi katika Sekta hii ya Mawasiliano.
Makampuni mengi yamekua yakitoa huduma dhaifu kwa bei kubwa na kusababisha usumbufu Kwa mteja na hivyo Azam Mobile inatarajiwa kuleta huduma bora kwani wameshajifunza Kwa mda mrefu wanachokosea washindani wake hasa katika masuala ya internet ambapo mitandao mingi imekua ikijinasibu kuwa inatoa huduma bora lakini ukweli ni kwamba hata video za YouTube mda mwingine huwezi kuplay.
Ninatarajia Azam kuja na Mkakati wa
-Kuboresha huduma (Speed)
-Kuleta bei ya kiushindani.
Kila laheri Azam Telecom Kwa uwekezaji huu.
View attachment 800823