Awekwa rumande kwa kuibiwa mke wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Awekwa rumande kwa kuibiwa mke wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BWANA Jackson Cleophans (30) mkazi wa Buguruni, jana alishangaa kufikishwa mahakama kwa kosa la unyang’anyi baada ya kupewa haki yake kwa kuwa yeye ndiye aliyenyang’anywa mke wake kwa kumfumani aliyemshitaki.
  Mshitakiwa huyo alishangazwa kutiwa hatiani na mahakama ya Wilaya ya Ilala na kupewa kosa hilo.
  Akitoa maelezo yake mahakamani hapo mbele ya Hakimu Luhwago, alidai siku ya tukio alifika eneo hilo kwa lengo la kumfumania mke wake aliyekuwa akifanya mapenzi na bosi wake aliyemtaja kwa jina la Farook Ahmed.

  Alidai muda mrefu mke wake alikuwa akimlalamikia kuwa bosi wake huyo alikuwa akimtaka kimapenzi na kwa muda mrefu, hivyo siku hiyo alifika eneo la tukio na kukuta mke wake akiwa na bosi huyo katika hali ya kimapenzi na kuwapiga picha na kupeleka ushahidi wa kamera kituo cha polisi cha Msimbazi na mke wake alikamatwa.


  Hivyo baada ya maelezo hayo hakimu alinayesikiliza kesi hiyo aliutaka upande mashitaka ambao ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka Daniel Buma, kufanyia upelelezi wa kina kuhusiana na hoja hizo na hakimu alisema endapo itakuwa kweli atamuachia mshitakiwa na kuwa huru.


  Hati ya mashitaka ilisomeka kuwa Jakson na mwenzake Abraham Hassan (25) walifikishwa katika mahakama hiyo wakikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la unyang’anyi wa kutumia silaha na kujipatia mali zenye thamani ya Shilingi milioni 4.8 walipokuwa eneo la fumanizi.

  Hati hiyo ilisomeka kuwa, washitakwia hao walifanya makosa hayo, Desemba 13 mwaka jana, majira ya saa 1 asubuhi katika mtaa wa Livingstone Kariakoo na kufanikiwa kuiba fedha taslimu Shilingi 250,000, dola za Marekani 1,400 na kompyuta mbili mali za Farooq Ahmed na kabla ya kujipatia mali hizo waliweza kumtishia mlalamikaji kwa silaha aina ya bastola.

  Hata hivyo washitakiwa hao walikana mashitaka hayo na walipelekwa rumande kwa kukosa dhamana kwa kuwa mshitakiwa anayeshitakwia na kosa la wizi wa kutumia silaha huwa hana dhamana , kesi hiyo itarudi tena mahakamani hapo Januari 13 mwaka huu kwa kutajwa.
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Sijui nani mkweli sasa...kama 'muibiwa mke' ndio mkweli, basi anastahili pole sana!
   
Loading...