Awamu ya JK yaongoza kuficha fedha nje ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Awamu ya JK yaongoza kuficha fedha nje ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Aug 19, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 18 August 2012 23:37 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [​IMG]

  YAFUATIA YA NYERERE,MKAPA NA MWINYI, ZITTO ASEMA WAJISALIMISHE
  Mwandishi Wetu
  RIPOTI ya utafiti wa utoroshaji wa fedha nchini kwenda kufichwa katika benki za nchi za nje ikiwamo Uswisi uliofanywa na na Shirika la Global Financial Integrity umeonyesha kuwa fedha nyingi kutoka Tanzania zilitoroshwa kati kipindi cha utawala wa awamu ya nne kati 2005 na 2009.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuhusu utoroshwaji wa fedha kwa njia haramu kutoka Afrika kwenda mataifa yaliyoendelea, ambayo gazeti hili limeipata, katika kipindi hicho fedha zilizofichwa nje ya nchi ni Dola za Marekani 7,967.4 milioni (sawa Sh12.7 trilioni).

  Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa katika kipindi cha utawala wa kwanza ulioishia 1985, fedha zilizofichwa nje zilikuwa Dola 3,493.3 milioni (Sh5.5 trilioni) na katika awamu ya tatu kati ya 1995 hadi 2005, zilikuwa Dola 2,108.8 milioni (Sh3.3 trilioni) wakati katika awamu ya pili zilitoroshwa Dola 529.1 milioni (Sh846 bilioni).

  Utafiti huo wa Shirika Global Financial Integrity unaonyesha pia nchi 20 za Afrika zinaongoza kwa kuficha fedha nje ya nchi, Nigeria ikiongoza.

  Jumla ya Dola za Marekani 1.8 trilioni zimefichwa katika benki mbalimbali nje ya nchi kutoka katika nchi za Kiafrika katika kipindi cha mwaka 1970 hadi 2009.

  Mpina
  Akizungumzia ripoti hiyo jana, Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina alishauri mambo mawili muhimu yafanyike ili kukabiliana na ufisadi wa kutorosha fedha na raslimali za nchi kwenda nje ya nchi.

  Alisema kuwa hatua ya kwanza ni kufanya marekebisho ya sheria za nchi na pili ni kujenga mfumo madhubuti wa kukabiliana na mafisadi nchini.

  Kuhusu marekebisho ya sheria, Mpina aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa baadhi ya viongozi wasio na uchungu na nchi wamekuwa wakitorosha kirahisi fedha na rasilimali za nchi kutokana na udhaifu wa sheria.

  “Ni lazima kwanza sheria zetu ziwe na nguvu ya kuweza kulinda fedha na rasilimali za nchi,” alisema mbunge huyo ambaye hivi karibuni alionyesha kukerwa na tabia hiyo aliyosema inazidi kuwadidimiza Watanzania kwenye wimbi la umaskini.

  Akizungumzia hatua za kuchukuliwa dhidi ya wahusika, Mpina alielezea kusikitishwa kwake na woga walionao baadhi ya viongozi kwa kuogopa kuwataja hadharani mafisadi.

  “Mfano suala la Rada… limekuwa ni tatizo na hakuna nia ya dhati ya kukabiliana na wahusika,” alilalamika.

  Alitaka mfumo wa kukabiliana na ufisadi ubadilishwe na uwe na lengo la kupata namna ya kurejesha fedha za umma badala ya ilivyo sasa ambapo mtuhumiwa anapopatikana na hatia mahakamani anaadhibiwa kwa kufungwa jela tu.

  “Kwa mfano kwenye kesi mbalimbali, kama vile fedha zilizoibwa kwenye EPA (Akaunti ya Madeni ya Nje) tunasikia mtu kahukumiwa miaka mitatu jela, anatumikia mwaka mmoja na nusu halafu anarudi kuendelea kula fedha alizoiba,” alilalamika.
  Katika Bunge lililopita Mpina, alikabidhi bungeni ushahidi wa ripoti mbalimbali zinazoeleza jinsi Sh11.6 trilioni zilivyotoroshwa nchini kwenda ughaibuni kuanzia mwaka 1970 hadi mwaka 2008 na kutaka Serikali kuwachukulia hatua wahusika.

  Mpina alisema Julai tano, mwaka huu vyombo vya habari vilimnukuu Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, akieleza kwamba Serikali haifahamu juu ya utoroshaji wa fedha hizo, lakini akapinga kwa kueleza kuwa Serikali inaufahamu uhalifu huo.

  Mpina aliishauri Serikali kutazama upya mashirika ya umma kwa kuwa yanaingiliana kiutendaji na majukumu yanayofanana.

  Zitto: Tutawataja wahusika
  Akizungumzia suala hilo jana, Zitto alisema kuwa walioficha fedha nje ya nchi wanapaswa kujisalimisha wenyewe kwa kuwa Serikali inaweza kupata orodha yao kutoka mamlaka ya Uswisi.

  Alisema kuwa amekuwa akishauriana na mmoja wa wabunge wa zamani wa Afrika Kusini ambaye ndiye aliyefanya naye utafiti kuhusu fedha hizo za kifisadi zilizofichwa Uswisi.

  “Tutawataja mmoja baada ya mwingine maana taarifa zetu ni za uhakika na hazina mashaka,” alisema Zitto.

  Alisema fedha hizo zimetokana na rushwa kwenye mikataba ya kutafuta mafuta, gesi na Kampuni ya Meremeta.

  Kashfa ya kuwapo kwa vigogo walioficha fedha zao nchini Uswisi iliibuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini mwezi Juni mwaka huu na baadaye mwangwi wake kulitikisa Bunge katika mkutano wake wa nane uliomalizika Alhamisi ya Agosti 16 mjini Dodoma.

  Habari hizo zilikuwa zikinukuu taarifa iliyotolewa na Benki Kuu ya Uswisi kuonyesha kuwapo kwa kiasi cha Sh315.5 bilioni, zilizotoroshwa na Watanzania na kufichwa nchini humo na vigogo ambao ni wanasiasa pamoja na wafanyabiashara.

  Jumatano wiki hii, tuhuma hizo ziliibuka tena bungeni pale Kambi ya Upinzani ilipodai kwamba inawafahamu wahusika wa ufisadi huo na kutishia kuwataja ikiwa Serikali haitawataja.

  Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, Zitto alipokuwa akiwasilisha hotuba ya kambi yake kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi alisema kuwa miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini, pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

  Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara, ndiyo walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

  Mwananchi limebaini pia kuwa kiasi cha fedha kilichothibitishwa kumilikiwa na Watanzania hao ni jumla ya Dola za Marekani 186 milioni (karibu Sh300 bilioni) kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1600 kwa dola za Marekani.

  Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni), mwingine dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki dola milioni 10 (Sh16 bilioni).

  Kwa kuangalia fedha hizo ni dhahiri kwamba vigogo watano tu kati ya kundi la Watanzania 27, wanamiliki dola milioni 126 (Sh201.6 bilioni) sawa na asilimia 67.74 ya fedha hizo, wakati wengine 22 waliobaki wanamiliki dola milioni 60 (Sh96 bilioni) sawa na asilimia 32.25.

  Kwa hesabu za kawaida, kiasi cha Sh300 bilioni, kinaweza kugharimia ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 33,300, ikiwa chumba kimoja kinagharimu kiasi cha Sh9 milioni.

  Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wafanyabiashara wanaomiliki kiasi cha dola kati ya milioni mbili na milioni saba.

  Wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere ambao akaunti zao zina kiasi kisichozidi dola 500,000 kwa kila mmoja.

  Wasomi wazungumza
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema kuwa hatua zilizochukuliwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuunda kamati kuchunguza suala hilo imechelewa.

  Alisema kuwa kwa kipindi kirefu baadhi ya wabunge wamekuwa wakituhumiwa kwa rushwa, huku akitolea mfano tuhuma za rushwa zilizowahi kutolewa na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, lakini Bunge lilikaa kimya.

  “Vitendo vya rushwa vipo na Kafulila aliwahi kulieleza Bunge kwamba katika Kamati yake ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) kunanuka rushwa, aliwataja wahusika lakini Bunge halikuchunguza mpaka mmoja wa aliyetuhumiwa amedakwa na Takukuru kwa madai kuwa kapokea rushwa,” alisema Dk Bana.

  Alisema kuwa Takukuru iliwahi kuweka wazi kwamba wabunge wanalipwa posho mara mbili, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

  “Labda walimwona Kafulila ni mpinzani na bado kijana mdogo…, lakini tuhuma kama hizi zikitolewa inatakiwa hatua zichukuliwe mapema ikiwa ni pamoja na kuchunguza,” alisema Dk Bana.

  Alisema kuwa masuala yote yanayohusu rushwa siyo tu yajadiliwe bungeni, pia watu wa kada mbalimbali wanatakiwa kuyajadili na kutoa mapendekezo yao.

  Kwa upande wake, Mhadhiri wa chuo hicho, Dk Kitila Mkumbo alisema jana kuwa hadhani kama mambo yanaweza kuwekwa wazi kama watu wanavyodhani kwa kuwa Bunge ni lilelile, halijabadilika.

  “Watu wanatoa tuhuma za rushwa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kufuatilia, wabunge kujadili rushwa ni suala zuri ila hatujui hiyo kamati itakuja na majibu gani, tusubiri tuone,” alisema Dk Mkumbo na kuongeza:

  ”Ikibainika tuhuma ni za kweli basi Bunge linatakiwa kujipanga upya kuhakikisha kuwa linapambana na rushwa.”

  Alisema kuwa pamoja na hayo, Bunge linajichunguza lenyewe, hivyo hana imani kama ukweli utakaopatikana utawekwa wazi.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]RIPOTI ya utafiti wa utoroshaji wa fedha nchini kwenda kufichwa katika benki za nchi za nje ikiwamo Uswisi uliofanywa na na Shirika la Global Financial Integrity umeonyesha kuwa fedha nyingi kutoka Tanzania zilitoroshwa kati kipindi cha utawala wa awamu ya nne kati 2005 na 2009.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuhusu utoroshwaji wa fedha kwa njia haramu kutoka Afrika kwenda mataifa yaliyoendelea, ambayo gazeti hili limeipata, katika kipindi hicho fedha zilizofichwa nje ya nchi ni Dola za Marekani 7,967.4 milioni (sawa Sh12.7 trilioni).

  Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa katika kipindi cha utawala wa kwanza ulioishia 1985, fedha zilizofichwa nje zilikuwa Dola 3,493.3 milioni (Sh5.5 trilioni) na katika awamu ya tatu kati ya 1995 hadi 2005, zilikuwa Dola 2,108.8 milioni (Sh3.3 trilioni) wakati katika awamu ya pili zilitoroshwa Dola 529.1 milioni (Sh846 bilioni).

  Utafiti huo wa Shirika Global Financial Integrity unaonyesha pia nchi 20 za Afrika zinaongoza kwa kuficha fedha nje ya nchi, Nigeria ikiongoza.

  Jumla ya Dola za Marekani 1.8 trilioni zimefichwa katika benki mbalimbali nje ya nchi kutoka katika nchi za Kiafrika katika kipindi cha mwaka 1970 hadi 2009.

  Mpina
  Akizungumzia ripoti hiyo jana, Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina alishauri mambo mawili muhimu yafanyike ili kukabiliana na ufisadi wa kutorosha fedha na raslimali za nchi kwenda nje ya nchi.

  Alisema kuwa hatua ya kwanza ni kufanya marekebisho ya sheria za nchi na pili ni kujenga mfumo madhubuti wa kukabiliana na mafisadi nchini.

  Kuhusu marekebisho ya sheria, Mpina aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa baadhi ya viongozi wasio na uchungu na nchi wamekuwa wakitorosha kirahisi fedha na rasilimali za nchi kutokana na udhaifu wa sheria.

  “Ni lazima kwanza sheria zetu ziwe na nguvu ya kuweza kulinda fedha na rasilimali za nchi,” alisema mbunge huyo ambaye hivi karibuni alionyesha kukerwa na tabia hiyo aliyosema inazidi kuwadidimiza Watanzania kwenye wimbi la umaskini.

  Akizungumzia hatua za kuchukuliwa dhidi ya wahusika, Mpina alielezea kusikitishwa kwake na woga walionao baadhi ya viongozi kwa kuogopa kuwataja hadharani mafisadi.

  “Mfano suala la Rada… limekuwa ni tatizo na hakuna nia ya dhati ya kukabiliana na wahusika,” alilalamika.

  Alitaka mfumo wa kukabiliana na ufisadi ubadilishwe na uwe na lengo la kupata namna ya kurejesha fedha za umma badala ya ilivyo sasa ambapo mtuhumiwa anapopatikana na hatia mahakamani anaadhibiwa kwa kufungwa jela tu.

  “Kwa mfano kwenye kesi mbalimbali, kama vile fedha zilizoibwa kwenye EPA (Akaunti ya Madeni ya Nje) tunasikia mtu kahukumiwa miaka mitatu jela, anatumikia mwaka mmoja na nusu halafu anarudi kuendelea kula fedha alizoiba,” alilalamika.[/FONT]

  [FONT=&amp]Katika Bunge lililopita Mpina, alikabidhi bungeni ushahidi wa ripoti mbalimbali zinazoeleza jinsi Sh11.6 trilioni zilivyotoroshwa nchini kwenda ughaibuni kuanzia mwaka 1970 hadi mwaka 2008 na kutaka Serikali kuwachukulia hatua wahusika.

  Mpina alisema Julai tano, mwaka huu vyombo vya habari vilimnukuu Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, akieleza kwamba Serikali haifahamu juu ya utoroshaji wa fedha hizo, lakini akapinga kwa kueleza kuwa Serikali inaufahamu uhalifu huo.

  Mpina aliishauri Serikali kutazama upya mashirika ya umma kwa kuwa yanaingiliana kiutendaji na majukumu yanayofanana.

  Zitto: Tutawataja wahusika
  Akizungumzia suala hilo jana, Zitto alisema kuwa walioficha fedha nje ya nchi wanapaswa kujisalimisha wenyewe kwa kuwa Serikali inaweza kupata orodha yao kutoka mamlaka ya Uswisi.

  Alisema kuwa amekuwa akishauriana na mmoja wa wabunge wa zamani wa Afrika Kusini ambaye ndiye aliyefanya naye utafiti kuhusu fedha hizo za kifisadi zilizofichwa Uswisi.

  “Tutawataja mmoja baada ya mwingine maana taarifa zetu ni za uhakika na hazina mashaka,” alisema Zitto.

  Alisema fedha hizo zimetokana na rushwa kwenye mikataba ya kutafuta mafuta, gesi na Kampuni ya Meremeta.

  Kashfa ya kuwapo kwa vigogo walioficha fedha zao nchini Uswisi iliibuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini mwezi Juni mwaka huu na baadaye mwangwi wake kulitikisa Bunge katika mkutano wake wa nane uliomalizika Alhamisi ya Agosti 16 mjini Dodoma.

  Habari hizo zilikuwa zikinukuu taarifa iliyotolewa na Benki Kuu ya Uswisi kuonyesha kuwapo kwa kiasi cha Sh315.5 bilioni, zilizotoroshwa na Watanzania na kufichwa nchini humo na vigogo ambao ni wanasiasa pamoja na wafanyabiashara.

  Jumatano wiki hii, tuhuma hizo ziliibuka tena bungeni pale Kambi ya Upinzani ilipodai kwamba inawafahamu wahusika wa ufisadi huo na kutishia kuwataja ikiwa Serikali haitawataja.

  Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, Zitto alipokuwa akiwasilisha hotuba ya kambi yake kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi alisema kuwa miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini, pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

  Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara, ndiyo walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

  Mwananchi limebaini pia kuwa kiasi cha fedha kilichothibitishwa kumilikiwa na Watanzania hao ni jumla ya Dola za Marekani 186 milioni (karibu Sh300 bilioni) kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1600 kwa dola za Marekani.

  Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni), mwingine dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki dola milioni 10 (Sh16 bilioni).

  Kwa kuangalia fedha hizo ni dhahiri kwamba vigogo watano tu kati ya kundi la Watanzania 27, wanamiliki dola milioni 126 (Sh201.6 bilioni) sawa na asilimia 67.74 ya fedha hizo, wakati wengine 22 waliobaki wanamiliki dola milioni 60 (Sh96 bilioni) sawa na asilimia 32.25.

  Kwa hesabu za kawaida, kiasi cha Sh300 bilioni, kinaweza kugharimia ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 33,300, ikiwa chumba kimoja kinagharimu kiasi cha Sh9 milioni.

  Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wafanyabiashara wanaomiliki kiasi cha dola kati ya milioni mbili na milioni saba.

  Wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere ambao akaunti zao zina kiasi kisichozidi dola 500,000 kwa kila mmoja.

  Wasomi wazungumza
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema kuwa hatua zilizochukuliwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuunda kamati kuchunguza suala hilo imechelewa.

  Alisema kuwa kwa kipindi kirefu baadhi ya wabunge wamekuwa wakituhumiwa kwa rushwa, huku akitolea mfano tuhuma za rushwa zilizowahi kutolewa na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, lakini Bunge lilikaa kimya.

  “Vitendo vya rushwa vipo na Kafulila aliwahi kulieleza Bunge kwamba katika Kamati yake ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) kunanuka rushwa, aliwataja wahusika lakini Bunge halikuchunguza mpaka mmoja wa aliyetuhumiwa amedakwa na Takukuru kwa madai kuwa kapokea rushwa,” alisema Dk Bana.

  Alisema kuwa Takukuru iliwahi kuweka wazi kwamba wabunge wanalipwa posho mara mbili, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

  “Labda walimwona Kafulila ni mpinzani na bado kijana mdogo…, lakini tuhuma kama hizi zikitolewa inatakiwa hatua zichukuliwe mapema ikiwa ni pamoja na kuchunguza,” alisema Dk Bana.

  Alisema kuwa masuala yote yanayohusu rushwa siyo tu yajadiliwe bungeni, pia watu wa kada mbalimbali wanatakiwa kuyajadili na kutoa mapendekezo yao.

  Kwa upande wake, Mhadhiri wa chuo hicho, Dk Kitila Mkumbo alisema jana kuwa hadhani kama mambo yanaweza kuwekwa wazi kama watu wanavyodhani kwa kuwa Bunge ni lilelile, halijabadilika.

  “Watu wanatoa tuhuma za rushwa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kufuatilia, wabunge kujadili rushwa ni suala zuri ila hatujui hiyo kamati itakuja na majibu gani, tusubiri tuone,” alisema Dk Mkumbo na kuongeza:

  ”Ikibainika tuhuma ni za kweli basi Bunge linatakiwa kujipanga upya kuhakikisha kuwa linapambana na rushwa.”

  Alisema kuwa pamoja na hayo, Bunge linajichunguza lenyewe, hivyo hana imani kama ukweli utakaopatikana utawekwa wazi.[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  uuuuuuh! twafa basi kama ndo hivo
   
 4. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ngoja nisiharibu siku yangu
   
 5. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngreeeeee!!!!!:mad::sad::angry::angry::mmph::sick::confused::bowl:
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Mimi niwalaumu sana wanachi, sisi ndo tunasababisha haya kupitia mahubiri ya AMANI, haiwezekani ihubiriwe amani huku fedha zikitoroshwa nje ya nchi, AMANI KITU GANI? Tusha fanywa mazezeta
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  Tuache chuki dhidi ya kikwete pekee,ukweli ni kwamba nchi hii imeanza kuporwa na Mkapa.Madudu yote yameanzia kwa mkapa, kikwete karithi madudu ikulu
   
 8. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  unamfahamu JK vizuri au unaropoka tu?
   
 9. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  id yangu shaharibika tena. ok, utajiri wa mh. Zito, na lowasa uhojiwe. . Haki ya nani
   
 10. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,694
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndo awamu yenye revenue collection kubwa, the more you see the more you steal
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Awamu yenyewe iliingia madarakani kwa pomps na kelele nyingi pamoja na kushangiliwa na matajiri. So kuficha pesa kule na serikali kukaa kimya ni namna ya kujaribu kulipa fidia
   
 12. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  madhambi yanayofichuka leo yalifanyika kipindi cha mkapa.
   
 13. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  madhambi yanayofichuka leo yalifanyika kipindi cha mkapa.
   
 14. d

  dizzle1 Member

  #14
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  hii hatari sasa
   
Loading...