Awamu ya 5 (2015-2020 ) ni yupi Waziri bora ( ulovutiwa na utendaji wake) kwa upande wako

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Apr 28, 2019
491
1,000
Tupo mwishoni mwa muhula wa kwanza wa serikali ya awamu ya 5, kuna mengi yamefanyika yanayokera na mengi pia yanayofurahisha ila tulio wengi tunafanya tathmini juu ya utendaji kazi wa Serikali hii kwa kumuangalia Rais pekee.

Leo nataka tulitathimini baraza la Mawazili la serikali hii ya awamu ya Tano kwa kila mmoja kumtaja Waziri wake anaeamini ni bora zaidi na kipi kilichokuvutia zaidi katika utendaji wake wa kazi.

Kwa upande wangu nimevutiwa sana na utendaji wa Waziri wa Ulinzi Mh: Husseni Mwinyi. Binafsi nimevutiwa na ukimya wake, sio mropokaji, si mpenda sifa, sijaskia akimtumbua mtu au akimkosoa hadharani mtendaji yeyote katika wizira yake. Sijui ni kwasababu anawaogopa wazee wa kazi au ni mfumo wake wa utawala.

Je, wewe ni nani Waziri wako bora?
 
Majaliwa na waziri mwenye zamana na uchaguzi(waziri mwenza wa tamisemi- jpm)
 
Aliye vunja kabati ni huyu waziri mtunza kibubu. Yeye amevunja record ya kukaa kwenye mikobani kwa muda mrefu pasipo kuiva kama majipu ya awamu hii
 
jamani..mmeshasahau

Waziri Ummy Mwalimu...hadi sasa kama taifa ujasiri na kipawa cha uongozi wake vimetuvusha dhidi ya janga LA Corona

pamoja na changamoto zinazoendelea kwenye wizara yake
 
Mimi binafsi
1: Waziri mkuu
2: waziri wa afya
3:waziri wa mambo ya nnje

Katika awo kama wataleta mapendekezo ya kuwania urais waziri mkuu nampitisha bila shida yoyote aise
 
Tupo mwishoni mwa muhula wa kwanza wa serikali ya awamu ya 5, kuna mengi yamefanyika yanayokera na mengi pia yanayofurahisha ila tulio wengi tunafanya tathmini juu ya utendaji kazi wa serikali hii kwa kumuangalia Raisi pekee.

Leo nataka tulitathimini baraza la Mawazili la serikali hii ya awamu ya Tano kwa kila mmoja kumtaja Waziri wake anaeamini ni bora zaidi na kipi kilichokuvutia zaidi katika utendaji wake wa kazi.

Kwa upande wangu nimevutiwa sana na utendaji wa Waziri wa Ulinzi Mh: Husseni Mwinyi. Binafsi nimevutiwa na ukimya wake, sio mropokaji, si mpenda sifa, sijaskia akimtumbua mtu au akimkosoa hadharani mtendaji yeyote katika wizira yake. Sijui ni kwasababu anawaogopa wazee wa kazi au ni mfumo wake wa utawala.

Je wewe ni nani Waziri wako bora?
Waziri Mahiga-alikuwa na busara sana.

Waziri wa Ardhi -Kawanyoosha sana maafisa ardhi .Ni wala rushwa sana.
 
Tupo mwishoni mwa muhula wa kwanza wa serikali ya awamu ya 5, kuna mengi yamefanyika yanayokera na mengi pia yanayofurahisha ila tulio wengi tunafanya tathmini juu ya utendaji kazi wa serikali hii kwa kumuangalia Raisi pekee.

Leo nataka tulitathimini baraza la Mawazili la serikali hii ya awamu ya Tano kwa kila mmoja kumtaja Waziri wake anaeamini ni bora zaidi na kipi kilichokuvutia zaidi katika utendaji wake wa kazi.

Kwa upande wangu nimevutiwa sana na utendaji wa Waziri wa Ulinzi Mh: Husseni Mwinyi. Binafsi nimevutiwa na ukimya wake, sio mropokaji, si mpenda sifa, sijaskia akimtumbua mtu au akimkosoa hadharani mtendaji yeyote katika wizira yake. Sijui ni kwasababu anawaogopa wazee wa kazi au ni mfumo wake wa utawala.

Je wewe ni nani Waziri wako bora?
Awamu hii hakuna waziri aliyekuwa huru kuonyesha ujuzi wake wizarani , huwezi kuwapima , mteuzi ndio alikuwa mtoa amri na maelekezo , waliojaribu kufuata weledi waliishia kutimuliwa
 
Back
Top Bottom