William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Lula wa Brazil si msomi, na nchi yake iko katika nchi kumi zenye uchumi bora duniani.
Eva Morales wa Bolivia si msomi lakini anaendesha nchi na kinaeleweka.
Ni Waafrika pekee tunaopenda Prestige za Usomi kama vile ni tija na njia ya kuleta maendeleo!
FMES...MZEE mwinyi alisema "kila zama na kitabu chake" ,zama za mrema zimepita ..na sioni mantiki ya kumfananisha na viongozi wa sasa ...kwani zaidi labda ya ubunge hakuna nafasi zaidi ya hiyo anaweza kustahili...kifupi hana nafasi ya kugombea urais tena!!!
!
- Mkuu hizo system unazoziongelea zimedumu kwa miaka karibu 300 sasa, wakati yetu ni only 45 years old, kumbuka kwamba hata hizo system unazozisema kua saafi zilianzia tulipo sasa, infact zao zilikua even worse, kwa mfano kule US wanawake na masikini hawakuruhusiwa kupiga kura wala kujihusisha na siasa, na imewachukua muda mrefu sana kurekebisha hayo,
- Huwezi ku-question propaganda kama kweli unaelewa maana ya hili neno politically, Mrema alikuwa na a big chance ya kuwachafua CCM kuliko walivyomchafua yeye, lakini kwa vile na yeye alikuwa fisadi ndio maana alishindwa kusema anything worthy against the establishment, mimi naamini kwamba kulikuwa na an agreement ya siri between CCM na Mrema ya kutogusana kwenye maovu yao.
- Tizama majuzi Chadema na Zitto, ngoma ilivyoishia kua draw wamejaribu kumchafua Zitto na yeye akawachafua, ikaja Compromise unafikiri bila ya Zitto kuwa na elimu ya juu na clean leader angeweza kuyafanya haya, ya kuwachafua Chadema na kubaki Naibu Katibu wao? au unafikiri yametokea kwa bahati mbaya tu bila elimu kutumika?
- Maovu yote ya CCM yaliyokuja kutolewa baadaye na Mrema, yalikua ni yale ya kupewa na Mzindakaya tu na sio aliyoya-experience yeye mwenyewe kama waziri, unafikiri ni kwa nini mkuu? Kwa nini hakuongelea tena dhahabu ya Airport?
Respect.
FMEs!
FMES,
Kwa nini Tanzania tunataka ku-reinvent the wheel wakati wenzetu waliotutangulia wameshafanya exeriment zote na kwa miaka mingi na walipo sasa hivi ni proven kuwa ni maendeleo mazuri?
Kwa nini sisi tunaendelea kulia kuwa bado ni nchi changa, sijui aah wenzetu walipata Uhuru zamani, mara wao hawakuwa koloni na vijisababu vingi tunavyovijaza kwenye jedwali kuhalalisha upofu na ubishi wetu wa kuchukua yale yanayofanya kazi vizuri na yenye matokeo mazuri?
Kama sisi bado ni nchi changa, kwa nini hatutumii kuni na taa za karabai tusubiri miaka 150 tupate Thomas Edison wetu atuvumbulie taa ya cheche za Bibo la korosho? au tuendelee kuswaga lami kwa mguu tukisubiri Karl Benz, Wright Brothers wetu watuletee ungo unaopaa kwa juisi ya matopetope na kuwa na kenge wakubwa kutubebea mizigo?
Kwa nini leo tumebadilisha pasipoti kuwa za sumaku na hata tunataka kuwa na vitambulisho vya uraia vya kisumaku na kimataifa?
Inakuwaje inapokuja kwenye uzalishaji mali, ufanisi na demokrasia, bado tunalilia kuwa sisi ni Wajima na tuachwe tukue huku tunatambaa?
Je si Nyerere alidai wenzetu wanapaa, inapaswa tukimbie na si kutambaa?
Ni dhana hii ya kudai sisi bado ni wachanga ambayo inadumaza unyonge na umasikini.
KUbadilisha na kuleta mfumo bora wa Kiutawala hauhitaji miaka 300 ya kuishi kwa pamoja, hakuitaji tuchapane mapanga kama Renamo n Frelimo au RPF na wenzao, hatuhitaji kumwaga damu.
Tulishafanya makosa zamani tulipoamua kuwa na nchi yenye chama kimoja na uchumi wa kijamaa bila kuwa na nyenzo, ufundi na utaalamu tosha wa kuweza kutuvusha mto tukiwa wachanga.
FMES,
Tulishafanya makosa zamani tulipoamua kuwa na nchi yenye chama kimoja na uchumi wa kijamaa bila kuwa na nyenzo, ufundi na utaalamu tosha wa kuweza kutuvusha mto tukiwa wachanga.
- Sawa sawa Mchungaji, na mpaka leo bado hatujajitoa hapo kwenye hilo shimo huku wengine mki-suggest kwamba tunaweza kutolewa kwenye hilo shimo na kiongozi asiye na elimu, that is incredible mkuu!
Respect.
FMEs!
FMES...MZEE mwinyi alisema "kila zama na kitabu chake" ,zama za mrema zimepita ..na sioni mantiki ya kumfananisha na viongozi wa sasa ...kwani zaidi labda ya ubunge hakuna nafasi zaidi ya hiyo anaweza kustahili...kifupi hana nafasi ya kugombea urais tena!!!
ni ukweli usio kificho kuwa ukitaja viongozi watatu maarufu [of all the time ] kisiasa miongoni mwa wananchi ...basi mrema,sokoine na nyerere ndio watakaotajwa....tofautisha list hiyo na uamue kuandaa viongozi bora kabisa ...wenye busara kitaifa[wenye busara si lazima wapendwe na wananchi]...ambapo hapo unaweza kumpata tena nyerere,salim,malecela,warioba,mkapa,mwinyi etc........kikwete hapo aingii yeye atakuwa anaingia kwenye kundi la kwanza la popular leaders....na anaweza kuwa chini ya mrema kwenye list ya viongozi waliopata kupendwa na watanzania..[populist]
kwa hiyo napingana na wewe kufananisha mrema na wapiganaji wa sasa kama slaa,zitto ,mbowe na wale wa ccm...kila kitu na wakati wake...wakati wake umekwisha,lakini kubalini kuwa wakati mrema anaapigana na ufisadi enzi zile....watu walikuwa hawamuelewi kama wananchi sasa wanavyoanza kuellewa...enzi zile walikuwa wakimshabikia kama mpira kuliko kumsikiliza ...na hili mwalimu aliliona ,...ndio maana alikuwa akiwaambia serikali wasimchape au kumpiga mabomu...maana ilikuwa kama kuwaamsha wananchi!!!
ni wazi kuwa heshima ya mrema kwenye siasa za nchi hii au legacy yake ipo,na kwa kuwa sasa sio tishio hakuna haja kuogopa kumkiri....hakuna kiongozi aliyepata kuigharimu CCM na idara ya usalama pesa kummaliza kama mrema...kuna watu wamekuwa mabilionia ..just kwa ku hold budget vote ya kummaliza mrema....na wengine iliwagharimu maisha just kwa kushindwa kumdhibiti.....ikabidi wapate "court marshall assasin"!!
kwa kuwa amezeeka na afya yake sio nzuri ..si vema kusubiri vinginevyo kuikiri legacy yake...pande zote !
Mkuu heshima mbele,
Leo nimeona kwenye habari ya ITV saa 2 Makamba akiwa Urambo akimpigia debe spika sitta na kuwaeleza wananchi kua anafaa wamchague 2010.
Akazidi kutanabahisha kua,CCM inaunga mkono wale wote wanaopinga ufisadi,hiyo haikutosha akamshika mkono spika mpaka kwa mama yake sitta na kumueleza kua watu wanataka kuwagombanisha!!
Hii ni pure politics,hakuna rafiki/adui wa kudumu.
Inaelekea maelezo ya mkulu yamewastua.
Kweli presha ya wapiganaji 11 imeanza kulipa,no wonder akapatikana mbunge wa 12 Makamba soon.
Wamesoma alama za nyakati.
Shime mkulu tuwaswage hadi ufisadi uishe ccm na nchini.kwa spidi hii mpaka march2010 wote watakua wmeshakua sidelined
- Mkuu kwanza ninapata kizungu zungu sana ninapoona some of The Great Thinkers wakijaribu kwa nguvu zote ku-promote ujinga, na kwamba eti Tanzania tunahitaji kiongozi asiye na elimu as a solution to our political, ecomomics na legal problems.
- Na besides, hao viongozi uliowasema ni kweli hawakusoma kabisaa angalau Mrema anawazidi mno kwa elimu, lakini tofauti ni kwamba wao wanaheshimu sheria za nchi zao na maamuzi mengi wanayoyafanya hayaendi kinyume na katiba ya nchi zao, as opposed na maamuzi mengi ya Mrema, ingawa Morales naye alitumia ufisadi sana kupitisha ile national memorandum.
Lakini still, solution ya matatizo yetu Tanzania sio kiongozi asiye na elimu kama Mrema, na pia ningeomba kuwatahadharisha kwamba kuna vijana wadogo humu, sasa hizi message za kuwaambia kuwa elimu sio muhimu sana, inatisha sana wakuu!
Respect.
FMEs!
Kila kitu huenda na wakati, kuna maswali mengi sana humu ndani kwa nini Mrema alifanya hiki au kwa au mbona alishindwa.
Tunachofumbia macho ni kuwa Mrema hakuwa Rais, hakuwa na mamlaka ya mwisho au kauli ya mwisho. Sawa na Sokoine alivyokosa mamlaka ya mwisho kupigana vita na Uhujumu 1983-84.
"!
FMES,
Tanzania has nothing to loose tukipata Form Four leaver, Form Six leaver au Diploma moja.
If Mkapa with his Masters and Kikwete with his BA or Masters have failed, how can you tell somebody that we only need PHD holders?
Chenge went to Havard, so was Rostam LSE, wengne je? Mramba has masters, Warioba has masters, Salim, Salmin and Shein are PHD holders, Mwandosya is a PHD holder, Mbilinyi is PHD holder, Dr. Bilali is PHD holder, Mattaka has Masters, Late Balali had PHD, Mgonja and Yona are very well educated, and so is Magufuli, Masha, Mwagunga, Hussein Mwinyi, Pinda and so was Malecela, Msuya, Kibona, Malima, Makweta even Mtei!
Great leadership has nothing to do with college degree, to have it is a plus and could provide an advantage, but it is not a solution. We have proof in Tanzania!
- Mchungaji vipi tena unaanza kubadilika, kwani wapiganaji 11 unaowa-question effectiveness yao against Mrema, ni marais wa Tanzania?
Respect.
FMEs!
Rev. Kishoka,
Mkuu mkitaka kumsifia Mrema fanyeni nyie kwa mapenzi yenu lakini sii sote humu.Ni haki yenu kimsingi, kwani mimi binafsi, mtu kama Mrema kuwa rais wangu au hata kukaribua kuwa rais wangu ilikuwa inatisha sana. Record yake mbaya sana ukianza na vifo vya bi vizee kule Shinyanga..
Niliwahi kuandika mengi kuhusu Mrema akiwa waziri na kama sikosei mkuu JMushi1 alinipinga sana kwa sababu ambazo yeye mwenyewe anaijua. Hivyo poengine ukaribu wenu kwa mtu huyu mnamwelewa tofauti nasi ambao ni raia na hatuna nuru kwake....
Mrema ni kama viongozi wengine waliobobea ktk Ujamaa na mtu KGB system...Sifa za vyombo vya kijasusi au upelelezi ktk enzi za Ukomunist zina sifa yake ya ROHO MBAYA..Ni watu wasiotaka mtu mwingine afanikiwe ila wao au ktk system yao. Na hakuna njia bora ila ile wanayoiona wao..
- Tunahitaji wananchi waliosoma na viongozi waliosoma, na Tanzania ni mfano mkubwa sana wa wananchi wengi wasiosoma, kwa sababu inakuwa ni vigumu kwao kuwa-hold viongozi wao to the task, matokeo ndio tuliyonayo ya viongozi wetu kujifanyia wanayotaka.
Respect.
FMEs!
Mkuu issue hapa ni Mrema au sio?..na ukiniambia sifa za Mrema kuweza kuukwaa urais nitakusikiliza vizuri kuliko hizi habari za kumsifia mgema.Mkandara,
This is where you go wrong kwa ku-internalize na ku-personalize hii issue.
Una haki ya kumpinga Mrema, sawa na wale wanaompinga Nyerere lakini wewe unamtetea Nyerere.
The issue now is about quality character tunazohitaji, sasa kama ni hivyo hata tukisema tuweke jedwali tuandike, Mrema, Mwinyi, Kimario, Nyerere, Mkapa, Kikwete, sijui Kawawa au Msuya, kutakuwa na pros na cons!
Nyerere si aliamrisha watu wakaburuzwa kwenye vijiji vya ujamaa na wakapoteza mali zao na wengine kupoteza maisha?
Mkapa si aliamrisha jeshi litoe mkong'oto Pemba na Mwembechai na watu wakapoteza maisha?
Kikwete si karuhusu wawekezaji wajifanyie wanalotaka na kule Buzwagi, Nulyanhulu na sasa Loliondo, ni dola inatumika kunyanyasa Watanzania kwa kuchoma moto mali, kufunga watu na kila ina ya upuuzi kwa kisingizio ni uamuzi wa Serikali au Serikali kulinda maslahi ya Mwekezaji?
If Mrema was such an evil person, kwa nini Bosi wake Mwinyi ambaye aliwajibika basi tulimpa kura za ndiyo akatuongoza kwa miaka 10? naye Mwinyi huyo huyo, kwa kujiamini akampa Mrema uwaziri wa Mambo ya Ndani?
Acha utani mkuu,kuwa raisi wa Tanzania is much more than what?Pia ungesoma posting ya Philemon Mikael ungeweza kuona kuwa sifa ulizotaja hapo juu hazijawa proof kuwa a certain leader will accomplish anything.... Hapo nyuma kama ungenisoma vyema ungegundua pointi yangu kuwa siasa za vyama zimetuangusha...Sasa hapo kwenye red highlight ebu nieleze what do you mean?Vigezo tunavyowekeana sisi waafrika ndio vimetufanya tushindwe kujitawala,na certainly mzungu alivutiwa na udhaifu huo na ndio maana akatutawala,hatujui tunataka nini na kwanini....Vigezo alivyovitoa mwalimu vya kumchagua Mkapa ni tofauti kabisa na hivi unavyovitoa hapa..Kwamba ufanisi wake akiwa wizarani ndio kigezo cha yeye kuchaguliwa kama unavyotaka kudai si kweli,matter of fact hakuna aliyewahi kufikiri kuwa Mkapa will be a president,na sisi watanzania tulikuwa hatuna utaratibu wa kujichagulia viongozi bali someone decided for us! Pia vipi kuhusu Mwinyi? Ni ufanisi upi huo uliopelekea kuwa na sifa za urais?
Tanzani bado ni nchi changa sana na hatuwezi kuweka vigezo vya kumpata kiongozi nje ya hali halisi tuliyonayo...Kama ingekuwa ni enzi zile na wewe ukaambiwa uchague kati ya Mrema na Mr Smith basi si ajabu ungemchoose Mr Smith kwa vigezo ulivyoweka...Sisi tumezoea kuambiwa cha kufanya na kuchaguliwa viongozi na kwa hiyo uwezo wetu wa kutambua kiongozi anayetufaa ni mdogo ama inawezekana haupo kabisa kwa watanzania walio wengi..Tusiishi kwenye nchi ya kufikirika,kwamba tunaweza kutumia vigezo vya lets say USA ili kumpata kiongozi bora wa Tanzania...Yani umesoma elimu ya mzungu ya jinsi gani ya kumpata kiongozi halafu directly una imply kwamba inaweza kutumika Tanzania ama nchi nyingine ya Afrika,haya mambo huenda stage by stage,hatujafikia kutumia vigezo vya juu,bado tuko chini,tunahitaji mtu tuliye naye,mwenye kutuelewa ili kuondoka hapo tulipo,mkoloni kututawala kwa vigezo hivyo alivyokufundisha imetufikisha wapi? Kwa vigezo hivyo mtanzani atakombolewa kweli? Umesema Mrema ni mzalendo,halafu then hafai kutuongoza,urais kama taasisi,uzalendo ni hatua kubwa ya kwanza na mengine atapata msaada wa kimawazo kwani hizi si zile enzi za zidumu fikra sahihi za mtu mmoja.
Wananchi nao wanatatizo la kufuata sheria,mnajuwa kabisa kuwa sheria hazifuatwi,lakini nyie ndio wa kwanza kusema kuwa viongozi mnaowachagua ni vinara wa kufuata sheria...Kweli hiyo? Tungekuwa hapa tulipo? Eti you knew Mkapa will make a better president than Mrema,hapo umenichosha,umeshindwa kutambua tatizo kuu lililotufikisha hapa tulipo,bado hulielewi na tatizo la kusahahu mapema unalo...Yani ufisadi kushamiri na maisha ya mtanzania kuporomoka ndio kujenga uchumi kunakokufanya uwe proud kuwa ulimpigia Mkapa kura...?Tutaona mengi!
Alichokifanya Mrema ni kumchallenge Rais kwa kukataa Collective Responsibility na kuondona Serikalini na CCM.
Ninacho wachallenge Wapiganaji 11 ni kumchallenge Rais na Mwenyekiti wao kwa kuwa chini ya Uongozi wake, Tanzania inagota na inayumba kupita kiasi.
Ndio maana nimesema kwenye zile thread nyingine, kelel za Ufisadi hazilipi, bali mengine yote ya kuonyesha wazi kuwa Serikali haina nguvu na aliye madarakani hafai.
This is what I expect from Wapiganaji, kutoa ultimatum ndani ya Chama na ndani ya Serikali si kwa ajili ya Mafisadi wachache bali mfumo mzima wa Kiutawala na Kiutendaji ambao ndio mzizi mkuu wa Tanzania kuwa hapa ilipo.
Kulilia shingo ya Chenge haitoshi na ndio maana kwenye majibu yangu kwa Mzee Mwanakijiji, nilisema wakaze Kende walilie kiti cha Kikwete na wapige mawe Serikali kwa kila kitu kinachoonekana ni udhaifu kama nilivyohoji kwenye thread ya Mafanikio gani ya Ari, Kasi na Nguvu.
Wanapoendelea kung'ata na kupuliza na kuchekeana na Mkuu wao, basi yanayotokea ni sawa na haya ya Makamba kwenda Urambo na kumpigia debe Sitta!
Je umesahau mnajimu wa humu ndani Mzee Mwanakijiji alisema kwenye makala yake kuhusu Wapiganaji kuungana na Mengi kuwa CCM na Mafisadi wanaweza kubadili kibao na kuanza kuwasifia kina Sitta na Mwakyembe na kuwapigia debe la nguvu ambalo halijawahai kuonekana?
Au umesahau kauli ya Kikwete majuzi kudai Chama hakina mfarakano wa kiitikadi bali ni jambo la kawaida watu kutofautiania (I think alitumianeno kuchikiana) na wapiganaji wakashangilia kauli hiyo na kusema ndiyo kukua kwa demokrasia ndani ya CCM?
Kama ndivyo kukua kwa demokrasia, iweje basi Mafisadi walioshikilia hatamu Chama walikuwa na kampeni kali kiasi hicho kumng'oa Sitta uanachama wa CCM na wenzake? au kuanza kupeleka pesa kwenye majimbo ya "Wapiganaji" na kuhonga wagombea wapya?
What kind of epiphany has emerged inside CCM hierachy that now Sitta ni shujaa?
So which one do we need, Taifa la walioelimika au Viongozi wasomi?
Maana wote hao ni Wasomi, sasa kama wao na Usomi na Elimu zao, wanashindwa kuleta maendeleo au kutoa hamasa ya maendeleo, leo wananchi tukielimika na kuanza kudai haki zetu kama tunavyofanya hapa si mbinu za kutumia mabavu zitatumika?
Kama wao wana nia ya kweli kuamsha umma wa Watanzania uwe wachangiaji makini wa maendeleo, basi wangeachana na Umangimeza na Utemi na kufanya kila mtu mpumbavu na kuimarisha Ujinga (ignorance not stupidity) kwa kuwa na mfumo bora na endelevu wa elimu, kuwa na mfumo wa haki na utu na mfumo wa kweli wa Kidemokrasia.
mkuu FMES pamoja na kelele wanazopiga wanaojiita wapiganaji 11...bado hawajafikia hadhi ya kufananishwa na mrema sembuse wapiganaji wa upinzani...wapiganaji 11 wanasukumwa na hidden ajenda...wapiganaji wa kweli lazima wasukumwe na utaifa...
- Anyways, Mkuu PM naomba kukubali kutokubaliana on this, maana kama wapiganaji 11 hawasukumwi na utaifa basi labda sijui wanapigania nini hasa! Ingawa pia bado siwezi kuwalinganisha na wapinzani, that is another subject for the future.
nina shaka labda baadhi ya wapiganaji 11 wanasukumwa na kukosa fursa kati ya sababu....wengine walikuwa tayari wamejitangaza kuwa wanateuliwa uwaziri wa maliasili....wengine wana presure ya kuwa upande wa pili mwaka 2005;;;
- "Nina shaka labda", ni clear kwamba hii sio fact, ila ni speculation.
etc ..pamoja na kazi nzuri wanayoifanya ..tuwape sifa wanazostahili...tusiwavimbishe kichwa!!
- Fair na balanced, ingawa it took a lot mpaka kuisema, I can take this home, na huu wako ni uungwana yaani kukubali inapobidi, bila conditions attached.
Respect.
FMEs!