Audio Files (.mp3) Kuwa Na Majina Mawili

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,924
8,174
Kuna baadhi ya music files za ku-download mfano wimbo Wa Mr II Sugu Motochini nimeu-download. Umeandikwa "Sugu - Motochini" lakini nikiucheza kwenye simu player inaandika "superdee" kama ndio jina lake.

Kwa nini hii iko hivi? Na namna gani naweza kubadili hiloj jina maana option ya ku-rename inanirudisha Kule kule kwenye jina la file?
 
Tumia computer, right click nenda kwenye details utaona meta data zote hizo. Na unaweza kubadilisha kila kimoja unavyotaka, kuanzia song title,album name,album artist,contributing artist etc
 
Naongezea tu kutoka kwa kiongozi ymollel , ufuatao ni mfano wa file la nyimbo lenye metadata.

2m513zp.png

Kuna vitu viwili vilivyokuwa vinakuchanganya, file name na song metadata.
Song metadata ni taarifa zinazowekwa kwenye faili la nyimbo ili kurahisisha utenganishaji wa nyimbo na kukusaidia kuweza kuongeza mpangilio wenye mantiki zaidi kwenye Music app/Music player/Library yako na vilevile kukupa taarifa za ziada kuhusu wimbo (mfano producer wa nyimbo na waandishi walioshiriki, na hata pia mashairi/lyrics). Mpangilio huo unaweza kuwa wa Cover art/artwork/album art, Albums, Title za nyimbo, wasanii, mwaka n.k. Kwa nchi zilizoendelea unaweza wameweza ku-organize nyimbo nyingi kwa kuweka metadata na kuziuza, mfano Itunes wanauza nyimbo zenye metadata sahihi. Ila kwa huku kwetu bado watu wengi hawapo interested na ku-organize music, na watu wengi sana wanakuwa wanahifadhi nyimbo bila kujali uwepo wa metadata au la. Kuna software mbalimbali zinazoweza kukusaidia kuweka/kuondoa/kuongeza/kurekebisha metadata kwenye music files mbalimbali. Mp3tag na dbpoweramp ni changuo zuri la software kwa kazi hiyo. Zipo very simple kutumia.
 
Back
Top Bottom