Auawa Kwa Kuhisiwa Kuwa ni Mshirikina

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
ANYAMBILILE KASOTE [60] ameuawa kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba yake kwa kile kilichodaiwa wananchi wamechoshwa na tabia zake za ushirikina.
Kasote aliuawa jana huko wilayani Mbalali mkoani Mbeya, kijiji cha Igurusi baada ya watu wasiofahamika kuvamia nyumba yake na kumchoma moto.

Taarifa za awali zilidai kuwa, watu hao ambao walidai kuwa kuwa na machungu ya kurogwa, walifika nyumbani kwa marehemu huyo majira ya saa 4 asubuhi na kumkuta amekaa nje ya nyumba hiyo.
Watu hao walimtaka mzee huyo aingie ndani.

Imedaiwa kuwa mzee huyo alipoingia ndani, watu hao walichukua mafuta ya petrol na kuyamwaga ndani kabla ya kumfungia ndani mzee huyo na kisha kumwaga petroli maeneo ya kuizunguka nyumba hiyo na kisha kuipiga kiberiti.

Moto mkubwa uliozuka ulisababisha kifo cha mzee huyo ndani ya nyumba yake.

Sababu ya watu hao kufanya vitendo hivyo ni kudaiwa kuwa mzee huyo ni mshirikina anauwa watu kijijini hapo, kuwaroga watu na vitendo vingine vinavyohusishwa na ushirikina

Katika tukio hilo hakuna mtu mwingine aliyedhurika maisha yake kwani imedaiwa kuwa mtoto aliyekuwa akiishi na mzee huyo alitoka kwenda kanisani kabla ya watu kuivamia nyumba hiyo na kuichoma moto.

chanzo:

Auawa Kwa Kuhisiwa Kuwa ni Mshirikina

h
izi imani mbovu za kishirikina zitatuondoka lini jamani............??????????????
 
Mambo ya kudhaniana hayakubaliki katika nyanja yoyote ile. Sheria zoote zinahitaji saana ushahidi kwenye kila jambo, vinginevyo tutatesana na kumalizana kwa kudhaniana tu. Imani zingine nazo MMMhhhhhh!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom