Auawa akiamulia ugomvi wa wanandoa

Auawa akiamulia ugomvi wa wanandoa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,609
MKAZI wa Lizaboni Manispa ya Songea mkoani Ruvuma, Mohammed Hamim, ameuawa kwa kupigwa na kipande cha bomba la chuma kichwani alipokuwa akiamulia ugomvi wa mume na mkeo ambao ni majirani zake.

Akizungumza na Nipashe jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tatu usiku katika mtaa wa Pacha Nne, kata ya Lizaboni .

Kamanda Mushy alisema siku hiyo ya tukio hilo, Hamim alikuwa amekwenda nyumbani kwa Soud Mdoka baada ya kusikia kelele zilizokuwa zikiashiria kuomba msaada na baada ya kufika, aliwakuta Mdoka na mke wake, Paulina Mlenga (35) wakiwa wanapigana.

Alisema baada ya kuona hivyo, Hamim alianza kuwaamulia jambo ambalo lilisababisha apigwe na kipande cha bomba la chuma kichwani na kumsababishia kifo papo hapo.

Mushy alisema Mdoka baada ya kubaini kuwa amemfanyia kitendo kibaya jirani yake kwa kumpiga na kufa papo hapo, alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Kutokana na kitendo hicho, Kamanda Mushy alisema Jeshi la Polisi mkoani hapa linamsaka Mdoka na akipatikana atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu mashtaka ya mauaji yanayomkabili.

Pia alisema mke wake, Paulina Mlenga, anashikiliwa na polisi katika jitihada za kumtafuta mume wake na mwili wa marehemu umeifadhiwa kwenywe chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea kwa uchunguzi.

Itv
 
Wanaacha kufyatuana ili wapeane raha wao wanapeana maumivu, aisee
 
Mimi nawaelewa watu wa nchi zilizoendelea kwa nini wanazingatia call 911.Huku kwetu kila MTU anapaswa kuwa na namba ya Mjumbe/Mgambo au Polisi unabofya Call Mjumbe/Call Polisi..maisha haya ukingilia ugomvi wa ndoa unaonekana kama na wewe unahusika..
 
Mimi nawaelewa watu wa nchi zilizoendelea kwa nini wanazingatia call 911.Huku kwetu kila MTU anapaswa kuwa na namba ya Mjumbe/Mgambo au Polisi unabofya Call Mjumbe/Call Polisi..maisha haya ukingilia ugomvi wa ndoa unaonekana kama na wewe unahusika..

kaka huku ni bongo ukipiga simu hujibiwi piga hiyo namba kama watakuja kwa mda huo hata mjumbehaohao tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom