Aua mumewe kwa kumvuta sehemu za siri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aua mumewe kwa kumvuta sehemu za siri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE mmoja wa Kijiji cha Mambegwa Msowelo Kilosa ,Morogoro anashikliwa na polisi Mkoani Morogoro, kwa tuhuma za kumuua mume wake kwa kumvuta sehemu za siri. Taarifa hizo zilitolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Thobias Andengenye ofisini kwake na kusema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 17 mwaka huu, katika kijiji cha Mambegwa.

  Kamanda huyo alimtaja mwanaume aliyeuawa kuwa ni, Masanja Kakoro (40) na kwamba kuuawa kwake, kunafuatia ugomvi uliozuka wakati wakiwa wamejipumzisha chumbani kwao.

  Alisema kusema hata hivyo chanzo kikuu cha ugomvi huo, hakijafahamika na kwamba mtuhumiwa anahojiwa zaidi na polisi na baadae atafikishwa mahakamani.

  Alisema baada ya mahojiano ya kina na mwanamke huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni, taratibu za kumfikisha Mahakmani kujibu tuhuma za kumpotezea maisha mwenzi wake kwa makusudi zitafuatia.

  Katika tukio lingine, mkoani humo mtu mmoja amefariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuiba dukani.

  Alisema mtu huyo alitambulika kwa jina moja la Masenga na tukio hilo lilitokea juzi katika maeneo ya Kiwanja cha ndege mkoani humo.

  Alisema mtu huyo ilidaiwa aliingia dukani na kujaribu kuiba vitu vililivyokuwemo ndani na kukamatwa na kupigwa hadi kupoteza maisha. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2875614&&Cat=1
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  sasa atafaidi nini? haya tuiache sheria ichukue mkondo wake
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  kudadeki!
   
Loading...