AU yaitaka DRC kutotangaza matokeo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
87335c94cf71d4402cc825b8c238cd55

Wagombea wa uchaguzi mkuu DRC 2018 Martin Fayulu wa upinzani (Kushoto), Felix Tshisekedi (Kulia) na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Shadary (Kati) -
Muungano wa Afrika (AU) umeitaka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iahirishe kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu.

Muungano huo unaonuia kuhimiza umoja na demokrasia, unasema una "shaka kubwa" na matokeo ya awali yaliotangazwa wiki iliyopita.

Matokeo hayo yalimpa ushindi mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi lakini mpinzani wa utawala uliopo, Martin Fayulu, anasisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa leo Ijumaa.

Kumezushwa maswali mengi kuhusu uhakika wa matokeo hayo huku kukiwepo shutuma kwamba Tshisekedi anapanga mpango wa kugawana madaraka na rais anayeondoka Joseph Kabila.

Baadhi ya viongozi katika Muungano wa Afrika na serikali walikutana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa jana Alhamisi na kutoa tamko kuhusu uchaguzi huo wa Desemba 30 unaopingwa pakubwa.

"Kumekuwa na shaka kubwa kuhusu namna matokeo ya awali yalivyokusanywa, kama ilivyotangazwa na tume huru ya kitaifa ya uchaguzi kwa kura zilizopigwa," taarifa ya muungano huo imesema.

"Kadhalika, AU imetaka kuahirishwa kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu huo," iliongeza taarifa.

Je tume ya uchaguzi inaweza kufanya nini?

87335c94cf71d4402cc825b8c238cd55-1

Felix Tshisekedi anaongoza chama kikubwa cha upinzani DR Congo kilichoanzishwa na marehemu babake mnamo 1982
Fayulu anatuhumu kwamba mshindi wa muda bwana Tshisekedi alikubaliana na rais anayeondoka Joseph Kabila.

Kabila amehudumu kwa miaka 18 na matokeo, iwapo yatathibitishwa, yataidhinisha ukabidhi wa kwanza wa uongozi kwa mpangilio tangu taifa hilo lipate uhuru kutoka kwa Ubelgiji mnamo 1960.

Tume ya uchaguzi imesema Tshisekedi alishinda 38.5% ya kura, ikilinganishwa na 34.7% alizoshinda Fayulu. Mgombea wa muungano wa serikali Emmanuel Shadary alijizolea 23.8%.

Fayulu aliwasilisha kesi katika mahakama ya katiba kupinga matokeo hayo Jumamosi akitaka kura zihesabiwe upya kwa mkono.

Matokeo hayo yanatarajiwa kutangazwa kama ni mapema sana leo, na wataalamu wanasema kuna uwezekano wa matokeo matatu.

Huenda mahakama:

  • Ikathibitisha ushindi wa Tshisekedi
  • Ikaagiza kura kuhesabiwa upya
  • Ikafutilia mbali matokeo yote na kuitisha uchaguzi mpya
87335c94cf71d4402cc825b8c238cd55-2

Lakini mahakama haijawahi kubatilisha matokeo katika siku za nyuma.

Kumekuwa na hisia gani?

Kutangazwa kwa Tshisekedi mshindi kumepingwa pia na kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa na ambalo pia linasema liliwatuma waangalizi 40,000 wa uchaguzi kote nchini.

Wataalamu waliopo katika serikali nchini Marekani, Ufaransa na Ujerumani pia wametilia shaka matokeo hayo.

p06w6b6r.jpg

Uchaguzi DRC: Ukatili na uhalifu wa asili uliopanda mbegu za vurugu
Wakati huo huo, Umoja wa mataifa unasema, vita vya kikabila magharibi mwa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo vimesababisha vifo vya takriban watu 890katika muda wa siku tatu mwezi uliopita,

"Duru za kuaminika" zinaeleza mapigano kati ya jamii za Banunu na Batende yalizuka katika vijiji vinne huko Yumbi, ofisi ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za binaadamu inasema.

Idadi kubwa ya wakaazi wa eneo hilo inaarifiwa wameachwa bila ya makaazi.

Uchaguzi mkuu wa Desemba 30 uliahirishwa huko Yumbi kutokana na ghasia.

Raia walioachwa bila ya makaazi ni pamoja na watu 16,000 waliotafuta hifadhi kwa kuvuka mto Congo hadi katika nchi jirani ya Congo-Brazzaville, umeongeza.

Nyumba 465 na majengo yaliteketezwa au kuharibiwa, zikiwemo shule mbili za msingi, kituo cha afya, soko na ofisi ya tume huru ya uchaguzi katika eneo hilo, Umoja huo umesema.

BBC
 
Kama waafrika haya ndio tunayoyafanya halafu eti tunasema vyombo vya magharibi vinatusema vibaya si ina maana sisi ni wanafiki.

Waandike kipi kizuri wakati habari zenyewe ndo hizi na baada ya hapo tena utasikia ghasia au vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kweli, Africa No Good.
 
Hatimaye umoja wa Afrika umeonya DRC iisitangaze matokeo ya Uchaguzi. AU imesema inamashaka makubwa na matokeo.
--------
The African Union continental body issued a surprise last-minute demand late Thursday for Congo's government to suspend the announcement of final results of the disputed presidential election, citing "serious doubts".

DRC's constitutional court is poised to rule as early as Friday on a challenge filed by the election's declared runner-up. Martin Fayulu has requested a recount, alleging fraud. Upholding the results could spark violence in a country hoping for its first peaceful, democratic transfer of power since independence in 1960.


The AU statement said heads of state and government agreed to "urgently dispatch" a high-level delegation to Congo to find "a way out of the post-electoral crisis" in the vast Central African nation rich in the minerals key to smartphones and electric cars around the world.

"This is truly incredible," tweeted Jason Stearns, director of the DRC Research Group at New York University. "Usually, the African Union defers to the subregion ... in this case they departed dramatically

Source: African Union urges DRC to suspend final election results
 
Nilijua tu wale jamaa wana nguvu Sana Na drc haitatulia mpaka awekwe mtu wao kwa hiari au kwa lazima kwa kweli ni wanaangalia maslahi yao Sana kuliko hata amani ya nchi nzima
 
Kiukweli pamoja na kazi nzuri waliyoifanya lakini ni kuwa tofauti ya kura kati ya mshindi wa kwanza na wa pili ni ndogo huku kukiwa na wananchi zaidi ya 2.3Millioni ambao hawakupiga kura sababu za kinachovumishwa ugonjwa wa Ebora. Mkoa ambao haukupiga kura ni ule unaomuunga mshindi wa pili.

Hivyo, kwa kuwa wameamua kuwa wazalendo wa kutangaza mshindi wa upinzania basi wafikirie zaidi hoja hizo ili kutoa haki kwa Fayulu
 
Kiukweli pamoja na kazi nzuri waliyoifanya lakini ni kuwa tofauti ya kura kati ya mshindi wa kwanza na wa pili ni ndogo huku kukiwa na wananchi zaidi ya 2.3Millioni ambao hawakupiga kura sababu za kinachovumishwa ugonjwa wa Ebora. Mkoa ambao haukupiga kura ni ule unaomuunga mshindi wa pili.

Hivyo, kwa kuwa wameamua kuwa wazalendo wa kutangaza mshindi wa upinzania basi wafikirie zaidi hoja hizo ili kutoa haki kwa Fayulu
Kura alizopata Fayulu ndiyo haki yake na huu ndiyo ukweli kwa Mabeberu!
 
Back
Top Bottom