AU na nchi za Afrika kutoitambua serikali ya waasi Libya?

Sawa tu heri kuwa mbwa wa mzungu utapangiwa bajeti yako kuliko kuwa mbwa wa mwafrika na kuachwa ukijitafutia chakula majalalani.

Ouch!, Mnajua mashujaa wetu waliopigana kufa na kupona kumtoa mwafrika na mtu mweusi utumwani na pia kuikomboa Afrika kama akina Mkwawa, Kinjeketile, Milambo, Kambarage, Karume, Lumumba, Nkrumah, Malcom X, Martin Luther King, Steve Biko na wengineo wakisikia maneno kama haya huko huko makaburini miili yao itakuwa inatetemeka kwa hasira!

 
<br />
<br />
Wewe unafikiri usalama wa Taifa wa Tanzania ni dhaifu kama Libya? Tofauti na Libya ambako Gaddafi hakujenga kikosi imara cha kijeshi na badala yake kutengeneza jeshi la kifamilia, hapa kwetu hali ni tofauti kabisa. CCM ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga jeshi lenye sura ya utaifa na bila chembe ya ukabila. Kwa maneno mengine, jaribio lolote la kuwatenganisha watanzania kwa makabila yao, dini zao etc haliwezi kufanikiwa kamwe, udhaifu ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo uliosaidia kuiangusha serikali ya Gaddafi.
Sawa mjumbe wetu wa shina.
 

Ouch!, Mnajua mashujaa wetu waliopigana kufa na kupona kumtoa mwafrika na mtu mweusi utumwani na pia kuikomboa Afrika kama akina Mkwawa, Kinjeketile, Milambo, Kambarage, Karume, Lumumba, Nkrumah, Malcom X, Martin Luther King, Steve Biko na wengineo wakisikia maneno kama haya huko huko makaburini miili yao itakuwa inatetemeka kwa hasira!

Ni kweli mashujaa wetu waliomtoa mkoloni wakisikia watatetemeka kwa hasira hasa wakisikia Mugabe na Gaddafi bado wanaendelea kuwa marais. Vilevile watasikitika kuona viongozi waliowaachia madaraka wao ndio wamekuwa wakoloni tena wabaya kuliko wajerumani, wafaransa na waingereza waliopigana nao very sad. Kwa kuongezea tu Nyerere akifufuka leo halafu atembelee Nyamongo akute shule inahamishwa ili mwekezaji achimbe dhahabu na jengo la mahakama ya rufaa linabomolewa ili mwekezaji apate parking ya magari yake lazima ataomba arudishwe kaburini.
 
Updates: Kutoka kwenye mkutano wa AU unaoendelea leo, wametoa masharti mawili makubwa kabla ya kuitambua serikali ya waasi (NTC) ya Libya.

1. Waasi wawashirikishe maafisa wa Gaddafi kwenye mazungumzo ya serikali mpya itakayoundwa.
2. Serikali ya waasi wanao control sehemu kuwa ya Libya wahakikishe kwanza usalama wa raia.
 
Umoja wa Nchi huru za Afrika hauna mpango wowote kama kweli wanaweza tuungane na kuwa nchi moja ili tusionewe kizembe kama huyu Col Gaddhafi walivyomfanya.
 
LIVE: AU imegawanyika kuhusu Libya hadi sasa nchi 16 zimeitambua serikali ya waasi najaribu kuzipata hizo nchi nitawabandikia hapa mkutano unaendelea.
 
Upinzani mkubwa uko kwa SA inayoonekana na nguvu kwa sasa, SA walikataa kuachia pesa (assets) za Libya walizozizuia hadi jana walipobanwa na UN security council lakini wamesema hawatazitoa kwa serikali ya NTC, kinachoonekana ni kwamba SA inataka serikali ya waasi ionekane imeshindwa kwa vile hadi sasa wananchi wanasubiri mishahara.
 
Mtonye na mkulu kuwa hata kupokea vyandarua ni aina na stairi nyingine ya kutawaliwa na ndio maana wazungu kuwa always beggers have no choices
 
Habari nilizonazo kutoka Addis Ababa mkutano umeisha na AU imekataa kuitambua serikali ya waasi 'they need an inclusive government', lakini wameruhusu individuals states kwa mapenzi yao kuitambua kama wanataka, hadi sasa zaidi ya nchi 20 zimeitambua.
 
Nchi zilizoitambua serikali ya NTC hadi sasa ni zaidi ya ishirini nimebahataka kupata zifuatazo..
Nigeria, Rwanda,Misri,Ethiopia,Gambia,Senegal,Bukinafaso,Ghana,Ivory coast,Chad,Tunisia,Morocco,Algeria(neutral),Kenya(neutral). Zingine ziko kimya zinasubiri uelekeo wa upepo.
 
Nchi zilizoitambua serikali ya NTC hadi sasa ni zaidi ya ishirini nimebahataka kupata zifuatazo..
Nigeria, Rwanda,Misri,Ethiopia,Gambia,Senegal,Bukinafaso,Ghana,Ivory coast,Chad,Tunisia,Morocco,Algeria(neutral),Kenya(neutral). Zingine ziko kimya zinasubiri uelekeo wa upepo.

AU is a paper tiger!
 
Wakati nchi nyingi zikibadilisha bendera ya Libya nimepita ubalozi wa Libya nchini Tanzania bado unapeperusha ile ya zamani ya kijani tupu wanasubiri nini kubadilisha, waangalie tusije kunyimwa misaada na Libya mpya.
 
Back
Top Bottom