AU na nchi za Afrika kutoitambua serikali ya waasi Libya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AU na nchi za Afrika kutoitambua serikali ya waasi Libya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Facts1, Aug 23, 2011.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuna kila dalili ya AU kutoitambua serikali ya waasi (TNC) iliyomwangusha Col. Gaddafi. Hadi sasa zaidi ya nchi 50 ulimwenguni na mashirika mbalimbali ya kimataifa EU, NATO,UAE yameitambua serikali hiyo lakini hakuna nchi yeyote ya Afrika ukiacha Tuniasia wala AU iliyowatambua. Jana jumatatu ulikuwa umeandaliwa mkutano wa AU mjini Addis Ababa Ethiopia lakini kwa hali ya sintofahamu ukaahirishwa dakika za mwisho hadi Alhamis ijayo.

  Akihojiwa na vyombo vya habari jana waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Afrika Kusini Maite Nkoana-Mashabane alisema hawaitambui serikali ya waasi na hawataitambua iwapo itaingia kwa mabavu.

  Inasemekana mapema AU ilikuja na Road Map ya kuumaliza mgogoro kidplomasia lakini ukapingwa na waasi na kuungwa na NATO kuwa haukuonyesha lini Gaddafi ataachia madaraka wakasema lengo la Road Map ni kumlinda Gaddafi abaki madarakani.

  "Nobody talked to us, nobody consulted us," says Jean Ping, chairman of the African Union Commission when asked about international military ...
  Mwandishi mmoja wa BBC Kenya aliandika hivi,
  Sababu ya kusuasua kwa nchi za ki Afrika ni kutokana na Gaddafi kuwa kipenzi na mfadhili mkubwa wa AU na baadhi ya nchi nyingi za Afrika. Hizi sababu na zingine ndizo zinazosababisha nchi nyingi za kiafrika kusita kuwatambua waasi wa Libya. Je wataendelea na msimamo huu hadi lini.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kinachowasumbua hawa viongozi wa Africa ni u-matonya. Gadaffi amekuwa anawalisha for years na ndio maana tangu mwanzo AU (viongozi) wamekuwa ama wako kimya au wamekuwa wanataka 'mazungumzo ya amani'. Kituko ni kwamba wakati UN wanapitisha Azimio la kulinda watu against Gadaffi sauti iliyokuwa ya muhimu ni ya sauti ya ARAB LEAGUE! Kwa hiyo kama AU wataendelea na kejeli kwanza wajue watawakasirisha wajomba wao na hasa sisi hapa bongo tuliowekeza kwenye u-matonya kama mkakati wa kupata chakula.

  Lakini nijuavyo, Senegal tayari wanawatambua hawa waasi.
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Unatarajia nini kwa nchi ambazo nusu ya bajeti zao inawezeshwa na EU, Marekani ni mashirika ya misaada ya kimagharibi? Umasikini, mgawanyiko na uroho wa madaraka ndiyo vinaiponza Afrika. Viongozi wetu wanajipendekeza na kuogopa kwamba wakiiunga mkono Libya, kibao kitawageukia. Wamesahau kuwa Marekani haina rafiki au adui wa kudumy.
   
 4. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Ipo siku waafrica tutajuta kwa kuwashabikia wamarekani. Nilikuwa naongea na jamaa yangu mmoja ambaye ofisini kwao wako na mtu kutoka iraq, yule jamaa analia sana na anasema iraq siyo sehemu tena ya kuishi, kiasi kwamba wananchi wanatamani utawala wa mtu waliyemchukia sana. Ukiacha hayo ukifuatilia hali ya misri kwa sasa naamini wapo wamisri wengi wanatamani utawala ulioangushwa, kwani hali ya kimaisha imekuwa mbaya kuliko maelezo. Tukija libya unaweza ona kuwa hao mnaodhani wako kulinda haki zenu hawapo huko ila wako tayari kuwachonganisha na kuwauwa ili wao wachukue mali zenu, libya hata vita haijaisha tayari ufaransa wamesha tia timu begazi kwenye mafuta, pia nasikia kuna contract kuwa waasi wakiingia madarakani hao waliowadhamini watacontrol mafuta kwa miaka 60. Jamani ivi haya kweli ni ya sisi waafrica kuyashangilia? Gadafi kama binadamu hawezi kukosa madhaifu yake lakini tunatakiwa kuangalia madhara ya madhaifu yake na madhara yanayokuja kwa bara la africa.
  Kwa wale wenye magari itakuwa ni ndoto tena mafuta kushuka kwani visima vyote wanataka viwe chini ya control yao then wao ndio watakuwa wanapanga bei. Sisi maisha yetu hayatokuwa sawa mpaka ardhi inatanduka.
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Miafrika ndivyo ilivyo itatawalia mpaka mwisho wa dunia
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  AU kwa kawaida huwa hawatambui ncho yoyote iliyochukuliwa kimabavu and Libya.

  Hawa rebels kwanza wana ma Islamists within their ranks

  Pili rebels are now Killing black Libyans and foreigners

  tatu I wonder who gets to keep Libya's 143.8tonnes of gold. (siisi tuna tones ngapi)?

  After all Hugo Chavez wants to take physical delivery of the gold Venezuela owns that is stored in Western vaults

   
 7. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,321
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Kama gadaff kang'oka, ****** anatushinda nini?
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,026
  Likes Received: 745
  Trophy Points: 280
  Bendera fuata upepo,mwenzao kapakatwa.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  sisi ni wanafiki,afrika is no more after Nyerere na wazalendo wengine,wamembakiza Mugabe tunaemponda hata sisi kwa vigezo vya "democrasia" ya hawa wazungu! Afrika imetekwa kifikra mpaka kiuchumi!
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nchi nyingi za kiafrika zinaongozwa na viongozi wanafiki na waoga. Hawana msimamo kuonyesha either kupinga au kuunga mkono yanayotokea kwenye bara letu la africa. Tatizo kubwa la viongozi hawa ni mifumo iliyowaweka madarakani.
   
 11. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Wewe unafikiri usalama wa Taifa wa Tanzania ni dhaifu kama Libya? Tofauti na Libya ambako Gaddafi hakujenga kikosi imara cha kijeshi na badala yake kutengeneza jeshi la kifamilia, hapa kwetu hali ni tofauti kabisa. CCM ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga jeshi lenye sura ya utaifa na bila chembe ya ukabila. Kwa maneno mengine, jaribio lolote la kuwatenganisha watanzania kwa makabila yao, dini zao etc haliwezi kufanikiwa kamwe, udhaifu ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo uliosaidia kuiangusha serikali ya Gaddafi.
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mwita, Chacha, Wambura, Marwa!!! Potiiiiii.

  Kwa Libya sio kukosa usalama wala nini. Gadafi alijenga usalama wa kufa mtu ndani wa nchi yake na hata nje ya mipaka ya Libya. Alikuwa na uwezo wa kusafiri kwa magari toka Tripoli hadi Cape Town na kulala kwenye mahema. Kuna wakati alishambuliwa na mabeberu akaishi kwenye mti kwa siku mbili!!! Alikuwa na ulinzi mkubwa sana. Tatizo ni kwamba Gadafi amaepigwa na kundi la mataifa kwa kisingizio cha UN. Gadafi amepigwa na NATO ambayo ina silaha na vifaa vya kisasa vya kivita lakini amehimili kwa muda wa miezi takribani mitano!! Hata sisi tungekuwa na mafuta wangekuja tu hao mabeberu. Ila sijui kama tuko salama na hii Urani ambayo inagunduliwa kila kukicha hapa nchini mwetu!!

  Mkuu viongozi wa afrika ni mapimbi sijawahi kuona. Gadaffi alifarakana na waarabu kwa kujitoa Arab League akisema yeye ni Mwafrika leo anashambuliwa na mabeberu viongozi wa kiafrika wamekaa kimya (samahani) kama wanawake!!
   
 13. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  AU hawana ubavu wa kutowatambua waasi wa Libya kama UK, France na USA wameshawakubali. In nay case Libya hawaitaji kutambiliwa na AU they are more Arabic than African. Kusema kweli AU is an irrelevant institution-a club for African leaders just.
   
 14. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani gadaff ndio kinini hasa mpaka tumlilie?

  kwa nini anataka atawale maisha??
   
 15. A

  Awo JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 793
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Who is Quaddaf? It is time to go end of story!
   
 16. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata mimi sijui!!!!
   
 17. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
 18. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wataringa tu na mwisho wataitambua.

  hapa afrika kuna nchi ina ubavu wa kutotambua kilichokwishatambuliwa na marekani na washirika wake? they are just doing politics, sioni hoja itakayobaki imesimama hapo!

  kama kweli AU ipo, imalize suala la somalia kwanza, manake ni dogo sana ukilinganisha na la libya wanakojidai kuwa walikuwa na road map,

  la libya wameishachemsha, waachane nalo, watuambie sasa road map ya somalia ikoje. huko ndiko kuna mateso makubwa kushinda hata libya
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu

  Kwa taarifa yako hali tuliyo nayo sasa usije thubutu katu kusema hayo maneno mkuu nchi siyo hivyo uidhaniavyo humu ndani wanajeshi wamechoka ndugu wa kumtii Amri Jeshi mkuu JK ni hao wakina Shimbo,Andengenye,Kova na wengineo itakuwa kama ile ya Egypt, kwahiyo usijipe matumani issue kama hiyo ikitokea humu ndani honestly wanajeshi wata chukua nchi na viongozi wao wa juuu wata kimbizwaaa usipaime maana huko kwa majeshi yetu kuna dhuruma kubwa kwa askari hawa wa chini.

  Usalama wa taifa ya nchi hiii unadhani utasaidia zaidi ya kuwatorosha viongozi hawa walipo. Ukitaka kulisema Jeshi letu labda usema kulinda mipaka yetu hapo sawa wengi watakuwa front ila ndani kwa ndani sisi kwa sisi nakuapia wajeda wanawageuka wakubwa wao hata tukipinga ntakuzurumu pesa yako mkuu ila kubali usikubali ukweli ndio huo nakupa
   
 20. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  After all, what is AU in world power, security, nothing. Ni kundi la madikteta wa kiafrica christined viongozi. Mikutano yao yote ni kulindana madarakani. daima huwa hawakubaliani sana sana ni kurudi na briefcase zimejaa " ifs" if ......then if......so if.......
   
Loading...