AU kutozingatia ushauri wa Tanzania kuhusu machafuko Burundi

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,206
AU kupeleka jeshi la kulinda amani Burundi kinyume na ushauri wa Tanzania. Uhuni wa CCM kubaka demokrasia Zanzibar umekosesha Tanzania uhalali wa kushauri majirani utatuzi wa migogoro ya kisiasa.
 
Mkuu hapa wanadai ni sababu za kiuchumi zaid . Yaani hasa hawa jamaa wa COW wanataka wapandikize kibaraka wao ili iwe rahisi kuifakia Congo. So far tz wanataka Nkurunzinza amalize mda wake ili wafanye figisu kuhakikisha wanamuacha tena mtu atakae rinda masirahi ya tz. Any way ngoja wenye data kamiri waje
 
Tanzania wamepoteza heshima kubwa sana katika nyanja za kimataifa kutokana na suala la uchaguzi wa Zanzibar. Hutomuona Lord wa Malofa ama Kikwete tena katika duru ya masuala yankupatanisha. Jonatahna Goodluck kashika mpini kwa sasa. Cheaters never win
 
Wapuuzi nyie, tz bado inaheshma yake. Utalinganisha tz na wale wanaobadilisha katiba. Unatarajia Rwanda na Uganda wamtenge Kurunzinza wakati wao wanamalengo hayohayo? Chuki yenu dhidi ya tz haitafanikiwa.
 
AU kupeleka jeshi la kulinda amani Burundi kinyume na ushauri wa Tanzania. Uhuni wa CCM kubaka demokrasia Zanzibar umekosesha Tanzania uhalali wa kushauri majirani utatuzi wa migogoro ya kisiasa.
Mungu ibariki AU .
 
Nenda kibanda maiti ukazungumze huu upuuzi wako uone utakachofanywa .
 
Tanzania wamepoteza heshima kubwa sana katika nyanja za kimataifa kutokana na suala la uchaguzi wa Zanzibar. Hutomuona Lord wa Malofa ama Kikwete tena katika duru ya masuala yankupatanisha. Jonatahna Goodluck kashika mpini kwa sasa. Cheaters never win

UKAWA opinion
 
Jamani sio kila jambo mliongelee mengine mko weupe mno sio mtoa mada wala wachangiaji, siasa za kimataifa mtu anaweka sentensi moja na mnamuachia na thread za kimataifa si anatifanya waTZ wote tuonekane viazi katika uwanja huu. Nje huko ni facts sio majungu kama mlivyozoea, sasa hapa mtu hata kuutolea balance inakuwa taabu Zanzibar hajafa hata kuku, burundi roho za watu zinapotea wengine wanakuwa wakimbizi kwa sababu ambazo zingezuilika kabisa.

Burundi inahitaji sana intervention ya wa TZ kuliko Zanzibar, ambapo Seif na Shein wanagonga cheeres na kucheza bao Ikulu na wananchi kila mtu anaendelea na maisha yake. Buja watu hawana uhuru tena hata Piere hayuko huru na kabumbu achezi tena na aendi kumsifu mungu kama alivyozoea. Watu wanazo silaha mikononi mwao na wanapinga kwa mtutu wa bunduki Peter kujiongozea muda kwa hila. Wababe wakina Rajabu hawajulikani walipo na Palipehutu kimerudi na wapiganaji wako mguu sawa.

Zihaka na maisha ya watu sio poa, ufaransa wamekufa wazungu response ilikuwa ndani ya masaa. Buja watu wanakatika kwa hila watu wako katika mipango mikakati na mazungumzo, msuluhishi M7 yeye mwenyewe anamikono michafu na hila zinazofanana na Peter tena ndio Mentor wake. Hata kama Piere Nkurunzinza yuko sahihi lakini isiwe kwa gharama za maisha ya watu. Hivi mlishawahi kwenda Burundi mkaona madhara ya vita vya miaka ya 90 mbona makovu bado yapo.

Tunahitaji majirani walio na amani ili tuendelee kufanya na biashara nasi tukue, sasa JPM asipo ingia kazini kiukweli itatugharimu na Peter ni Jipu kule ambalo linahitaji kutumbuliwa japo limekaa sehemu mbaya. Tunafahamu diplomasia na inteligensia inayo nafasi yake lakini let stop breeding. Maraisi waEAC wanachelewa kuchukua hatua onlu Magifuri style can turn things arround. Kamwe ya Zanzibar tusilinganishe na burundi hata siku moja, Zanzibar muhalifu anaitwa post kwa samansi anaenda Buja watu wanazo grinade, AK 47 na SMG za lutosha sana na wanayo makovu ya kuwapa nguvu ya kukaa mstari wa mbele.

Inahitajika mabadiliko ya uongozi Burundi haraka, kuwe na serikali ya mpito kuelekea uchaguzi huru haraka na serikali ambayo itawajibika kufanya usuluhisi/upatanishi/kusamehana na ilivyofanyika south Afrika na baadae Rwanda. Kuna wababe wakivita wengi ambao wanaweza kusimamiA show hatare Peter yeye mwenyewe aliokota dodo kutoka kwa kina Rajabu na akawageuka na kuwasweka ndani watu waliopigana na kumweka madarakani ambao wanajikusanya huko Congo,Rwanda na Uganda kurudi kumtoa kwa namna ile alivyowrkwa madarakani. Tanzania ndio ilimaliza vita kwa kumshauri Agaton kukubari kuweka silaha chini na sio Peter mwenyewe tena kwa diplomasia na inteligensia tu. Sasa waTZ ndio partner sahihi katika kushughulikia mzozo wa burundi kuliko jirani yeyote yule warundi wenyewe wanajua. AU hawana record lakini watanzania wanayo records na watu waliofanya hivyo bado wapo.

Zanzibar bado iko undercontrol ukiondoa wengine wameona kama fursa baada ya kushindwa uchaguzi ili kuwatia adabu walioshinda, kijiko kikiitwa kijiko TZ inatakiwa kuingia kazini Burundi haraka sana na Magufuri atawajibika pia kama mauaji zaidi yakiendelea huko. Ila imani yetu washauri watakuwa wameshamwambia nini cha kufanya na asiogope kutumia pesa kwa ajiri ya majirani sababu wasipokaa vyema huko hatafikia malengo na atatupa kazi kubwa sana 2020 manake mwaka huu tumelala na viatu, hata hawa wanaoshoboka leo hawakumchagua na ndio waliokuwa wanapolomosha matusi humu.
 
UKAWA opinion

Waziri wa mambo ya nje asingewaita mabalozi wa nchi za nje na kuwaambia musitudharau kwa sababu ya Zanzibar.

Dr Magufuli asingetowa hutuba kanisani na kusema hayuko tayari kuzuiliwa safari za nje na misaada kwa sababu ya Zanzibar.

You can tranfer blames but not the consequences
 
AU kupeleka jeshi la kulinda amani Burundi kinyume na ushauri wa Tanzania. Uhuni wa CCM kubaka demokrasia Zanzibar umekosesha Tanzania uhalali wa kushauri majirani utatuzi wa migogoro ya kisiasa.
Mkuu kwani AU imekaa lini kujadili suala la Burundi na kufikia uhamuzi wa kupeleka jeshi Burundi? Mnacho sahau AU si kama C.O.W - kumbuka vile vile kwamba Tanzania anasikilizwa sana na kuhungwa mkono na nchi nyigi za Africa.
 
Dr Magufuli asingetowa hutuba kanisani na kusema hayuko tayari kuzuiliwa safari za nje na misaada kwa sababu ya Zanzibar.
Kama hatuko tayari kuwa internationally isolated kwa sababu ya Zanzibar, kama Magufuli alivyosema, basi tuvunje Muungano..

I really don't care much about foreign aid cut off lakini ki region cha Zanzibar kimetukosesha Katiba mpya, kinatu cost immensely Watanganyika, tuachane nacho...
 
TANZANIA NI "1" KATI YA "5" HATA KAMA WANGEKUWA WANATUMIA MFUMO WA KUPIGA KURA HAIWEZI KUSHINDA KAMWE!
CHAGUO LA WENGI CHAGUO LA MUNGU.
ii
 
Wapuuzi nyie, tz bado inaheshma yake. Utalinganisha tz na wale wanaobadilisha katiba. Unatarajia Rwanda na Uganda wamtenge Kurunzinza wakati wao wanamalengo hayohayo? Chuki yenu dhidi ya tz haitafanikiwa.
Hizi lawama zako unampelekea nani sasa , AU au mleta uzi ?
 
Tanzania pamoja na nchi zingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hazitapeleka askari wake Burundi. Nchi zingine zilizobaki za AU sioni hata moja yenye msisimuko wa kupeleka askari wake huko bila ushirikiano wa nchi za EAC ambazo ndiko askari hao watakapopitia kuifikia Burundi. Kupitia angani ni hatari kwao kwani majeshi ya Peter hayatawaruhusu - yatawatungua. Kwa hiyo AU haina namna.
 
Back
Top Bottom