Atupwa jela miaka 3 kwa kutaka kupiga kura mara 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atupwa jela miaka 3 kwa kutaka kupiga kura mara 2

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Fidel80, Nov 3, 2010.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  DAUDI Gimbishi (41) mkazi wa Kijiji cha Mwamitumi, Kata ya Ipililo, Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, jana amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela bila faini kwa kosa la kutaka kupiga kura zaidi ya mara mbili kinyume na utaratibu wa sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 kifungu cha 102(a).
  Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Thomson Mtani, baada ya mshitakiwa kukiri kosa huku akijitetea kuwa alifanya kosa hilo baada ya kuahidiwa kupatiwa sh 10,000 kutoka kwa Matege Magoto, aliyewahi kuwa diwani kipindi cha miaka ya nyuma.
  Hakimu Mtani alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo huku akijua anafanya kosa kisheria, jambo ambalo lingeweza kuvuruga matokeo ya uchaguzi na kusababisha uvunjifu wa amani sambamba na kuondoa haki ya mchaguliwa halali, hivyo anamhukumu kutumikia kifungo hicho ili liwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
  Awali Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Pili, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 31 mwaka huu majira ya saa 7:00 mchana katika chumba cha kupigia kura kituo cha Ghalani kijijini humo.
  Upande wa mashitaka ulidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alikutwa na jumla ya karatasi sita za kupigia kura zikiwa mbili za udiwani, mbili za ubunge na mbili za urais huku tayari akiwa ameshapiga kura awali.
  Alidai wakala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bundala Ndogani, aliyekuwepo ndani ya kituo hicho aliweza kumgundua na kutoa taarifa kwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Jumanne Mkwama ambaye alimweka chini ya ulinzi na alipompekua alimkuta akiwa na karatasi hizo.


  Atupwa jela miaka 3 kwa kutaka kupiga kura mara 2

  Hii sheria kwa nini haiwabani wanao chakachua?
   
 2. E

  Edo JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Good lesson
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wanao chakachua wanapeta huyu kataka kupiga kura mara 2 kala mvua 3
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Huyu ni messenger karatasi za kupigia kura amepata wapi? Upelelezi ulitakiwa uende mbali zaidi ili kuchimbua hilo shina
   
Loading...