Attack za CCM Mtandao vs. CHADEMA Mtandao

Attack za CCM Mtandao vs. CHADEMA Mtandao

ushauri mzuri sana Junior Zito..Nasikia kaka yupo nje ya nchi kweli haya..joking?
Haaahaaaa mkuu unanikumbusha kisa cha zitto kule sumbawanga.....asee huyo jamaa hta kma mie polisi siendi kumkamata 😀😀😀😀
 
Hili Jukwaa limeharibika baada ya Uvccm walipojua ukiwatukana viongozi wa Upinzana wanaku Makonda.yani unateuliwa ndio maana umeona ukiongea baya kuhusu Serikali hawa Uvccm wanakujibu km wao ndio wasemaji.
 
Tatizo ni kwamba wengi wanaounga mkono ccm hapa jf ama watoto wa viongozi au wake zao , ama ni viongozi wenyewe , kwahiyo wako tayari kufa kwa ajili ya maisha yao yanayotegemea kudra za ccm .
 
Jana niliandika mada kuhusu kushake kwa diplomasia ya Tanzania kimataifa. Ulikuwa ni ushauri tu kwa viongozi wetu ambao kimsingi siyo watawala kwakuwa tume/wamechaguliwa.

nilipata kebehi KUTOKA kwa vijana ccm..Mara wazee wa kata tatu, baada ya kipigo cha kata 19,wengine wakaniita nyumbu sijui., mwingne akaniambia mshauri mbowe achana na Magufuli wetu. Wengine eti mkalipie kodi jengo lenu.

Wiki moja imepita niliwahi pia kuandika ukimya wa viongozi wa chadema/ juu ya Ben saanane pamoja na shutuma za kubenea. Aisee, napo nilioga shutuma nyingi sambamba na kejeli kutoka kwa chadema. Mara Lumumba huyu, Mara propanga wa Lumumba, Mara buku kazini. Wengine wakaniita kilaza wa Lumumba. Mara bendela fata upepo.

Jukwaa hili tunaliharibu sana. Binafsi nilijiunga 2010 siyo kwa akaunti hii kipind kile Jamii forum kulikuwa MTU akiibua hoja anajibiwa kwa hoja. But Leo tunajiabisha sana na kama siyo wasomi vile. Let's discuss issues- pinga kwa hoja, kubali kwa hoja.

Tukumbuke sisi ndo vijana wa Leo..wengine tuna watoto/ wengine tutapata pia. Tunabishana na kusuguana kwa ushabiki. Kizazi chetu kitakuwaje. Tuwe vibrant.

Ushabiki wa kisiasa usitutoe kwenye agenda ya maendeleo. Wananchi na wanajamii forum tunataka maendeleo, siasa safi na utu wa mtanzania uheshimiwe.Forum ya kisiasa isiwe km kijiwe cha celebrity forum!
Tukiruhusu kutumika na wanasiasa tutaipoteza Tanzania. Anakutumia anakupa shilingi ngapi na mwambie akupe na life insurance basi.

Shukrani.

Agenda yetu iwe ni maendeleo na siyo vyama.

Sure
 
Naunga hoja mkono.ingawaje hili ni jukwaa la siasa leo hii limebadilika na kuwa la vyama viwili. Ccm na chadema. Hii inaleta mkanganyo sana kwani kwa asiye na chama matusi ,kejeli vitakuishia. Kuna baadhi ya majukwaa wako smart sana,wanabishana kwa hoja bila kejeli wala matusi,ni bora sasa wanaojiita timu lumumba au timu ukawa kubadilika ili hata kwa ambao siyo wanasiasa kuweza kujiunga na chama fulani kupitia hoja zinazitolewa hapa
 
Huu Uzi c wa kichama lakn kunabaadhi ya comment zimeingia uchama zaidi ila Luna baadhi ya watu kutukana ni moja ya maisha yao katk jamii.

Kiukwel nimekuwa nikisoma threads mbali mbali cjawahi kuona Uzi wowote ule unaoelezea maendeleo na jinsi ya kujifunza maendeleo na jinsi gan maendeleo yanapatikana watu wamekuwa uccm uchadema mpaka kelo wengne hatu vyama kabisa na c washaabiki wa vyama. Mm ningeomba kila mtu Ajitambue kiukwel kikwel maswala ya siasa yametuchosha wengne na hili swala vijana wasio kuwa na maada za mcng wakae pembeni kiikwel
Na kunakitu k1 nimekigundua humo JF mtu akianzisha thread ya kizungu wachangiaji ni wachache cn weng wao watabakia kupita tu au kuandika tuneno 2 tu kwa muda mwingne tubadili hata lugha tuone matuc yatakuwepo
 
Vijana wa kizazi hiki wengi wamewakabidhi wanasiasa zao
 
Hill jukwaa limevamiwa na watu ambao think capacity haifikilii kingne nahc weng wao ni wanaoshinda kwenye vibanda vya magazeti kusoma vichwa vya habar vya magazeti
 
Vijana wa CCM na CHADEMA kwakweli wanaharibu maana halisi ya "Home of Great Thinkers"
Asilimia kubwa sana hatutumii akili zetu vizuri.
Utashangaa mtu akileta mada ambayo haihusiani na siasa wachangiaji watakuwa wachache sana.
Let's use our heads guys....
 
Kuna wanasiasa tuliwaambia kipindi kile kuwa walimu wamegoma mgomo mrefu, wanasiasa wakapinga wakiwapa vitisho kisha kuwalaghai.
Wakawalazimisha watoto wafaulu, walimu wakatii kisha wakaanza kutemgeneza kizazi cha watoto wawezao kufaulu mitihani ya taifa huku wakikosa stadi nyingi.

Kizazi hicho kimeendelea hivyo hivyo na kilivyokutana na upepo wa siasa vikakumbwa nao na ndicho kinachosumbua sahizi.
Hicho hakipingi kwa hoja , bali hupinga hoja kwa kuwatusi watoa hoja, kuwakashfu hata kudharau, kimetiwa upofu wa vyama vya siasa wanavyoviamini huku wakiona kuamini tofauti na wanavyoamini ni Upumbavu ama dhambi kubwa wakati mwingine wakitamani wabaki wao pekee(yaani chama wanachokiamini)

Hao ndio wanaofurahia vifo vya watu wanaoamini vyama tofauti na wanavyovifuata, wapo tayari kuwatusi wazazi wao ama jamaa zao kisa wanaamini tofauti na wanavyoamini hawana nafasi ya kuelimisha na kushawishi maana hawajawahi kuelimishwa ama kuelimika, wamefanya vyama ni dini ama imani.

Na bahati mbaya kizazi hicho kinaendelea kuendelezwa kwani hao wanaenda kuwa walimu , walezi , wazazi na viongozi. Hakitakoma kwani ni kama ugonjwa wa urithi uendao vizazi na vizazi.


Demokrasia ni kama wimbo wa msibani, haufurahishi na wala haupendwi ila ipo siku kama hutouimba, utausikia na usipousikia utaimbiwa
 
Kiapo cha nitasema ukweli daima ni kiapo cha TANU,CCM kwao zidumu fikra za mwenyekiti hivyo hata kama utakuwa msomi fikra zako na mawazo huru unafukia ardhini.


Wew jamaa yani tayari ushaanza siasa tena! Kweli jf ya sasa si kama ile ya zamani
 
Back
Top Bottom