ATN kuonyesha laivu 16 bora ya Mabingwa Ulaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ATN kuonyesha laivu 16 bora ya Mabingwa Ulaya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mazengo, Feb 9, 2011.

 1. Mazengo

  Mazengo Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  [​IMG] [​IMG]
  KITUO cha televisheni cha ATN ( Agape Television Network) kitaonyesha mechi zote 19 za Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kuanzia hatua ya raundi ya 16 itakayoanza Jumanne ijayo.

  Kituo hicho ndicho chenye haki ya kipekee nchini katika kuonyesha mechi hizo za UEFA.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Meneja Mkuu wa Huduma za Maudhui wa kituo hicho, Steven Mshana alisema mechi hizo zitaonekana katika njia ya digital kuanzia Februari 14.

  "Hivi sasa ATN imeanzisha vipindi vipya ili kufurahisha watazamaji wake, vipindi hivyo ni Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Mapitio ya magazeti, vipindi vyenye radha ya Kiafrika, maigizo, vichekesho na sinema,"alisema Mshana.

  Wiki ijayo ligi ya Mabingwa Barani Ulaya itaendelea, ambapo Jumanne, AC Milan itacheza dhidi ya Tottenham, Valencia itacheza dhidi ya Schalke na siku ya Jumatano Roma itacheza dhidi ya Shakhtar Donetsk wakati Arsenal itakuwa ikipambana na Barcelona, pia mechi zingine za hatua hiyo zitachezwa Februari 22 na 23.

  Mshana alisema kituo hicho ambacho kinamilikiwa na Agape Life Church hivi sasa kimefunga mitambo yake ya kisasa Kisarawe,Tanga, Moshi,Arusha,Mwanza,Dodoma,Mbeya, Kigoma na Sumbawanga, hivyo watazamaji watarajie kuona picha zenye ubora wa juu.

  Alisema kituo hicho hivi sasa kipo katika mchakato wa kuwa cha kawaida zaidi na kuanzisha televisheni nyingine ambayo itakuwa ikirusha vipindi vya kidini vya dini mbalimbali.

  Alisema Agape Life Church ambalo makao yake makuu yapo Mbezi Beach, pia la matawi ya kanisa hilo sehemu mbalimbali mbalimbali nchini Tanzania.

  Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya zinatarajiwa kuchezwa Mei 28 kwenye Uwanja wa Wembley nchini England, wakati zile za robo fainali zitachezwa Aprili 26,27 na Mei 3,4, ambapo hatua ya robo fainali itachezwa Aprili 5,6 na 12,13.

  Klabu ya Inter Milan ya Italia ndiyo inayoshikilia ubingwa wa mashindano hayo, ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao 2-0.
  source: ATN kuonyesha laivu 16 bora ya Mabingwa Ulaya
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  peleka sports & entertainment.....tutaisoma huko
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  DUh kila mtu anabinafsisha anachoweza si mchezo
   
 4. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  safi hiyo
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Dah ATN huwa iko very clear! Tuta enjoy sanaaaaaaaaaaaaa
   
 6. k

  kiwadama Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yani kaka hawa jamaa wana2saidia cc walala hoi. Mungu awabrik.
   
 7. Mazengo

  Mazengo Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  The feeling is mutual.
   
 8. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  asante sana kwa taarifa
   
 9. aye

  aye JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  hongereni sana kwa kutujali tusioweza DSTV
   
 10. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Good news!
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ving'amuzi vya ATN vinauzwa wapi?
   
Loading...