Crocozilla
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 469
- 335
Mimi ni mteja wa CRDB Bank, hivi majuzi nilikuwa Arusha na nilipata huduma ya kuchukua pesa katika ATM ya CRDB Bank pale Ngulelo kwenye kituo cha mafuta. Kwa kweli nilishtuka kuona pesa Ilizotoka kwenye mashine maana zilikuwa chafu sana na chakavu kweli.
Kwa bahati mbaya mimi nikuwa mwathirika mapema tu kwa kupewa pesa chakavu na chafu sana MBAYA ZAIDI NOTI MOJA YA 10,000 ILITOKA KIPANDE! Nilifika katika tawi lao kuomba kubadilishiwa nikaanza kukemewa sana kuwa mbona hiyo pesa ni kipande nikatoa maelezo ambayo hata hivo hayakukubalika kabisa kwa maelezo kwamba NAMBA ZOTE LAZIMA ZIWEPO ndo ibadilishwe. Najiuliza namba za wima nitazipataje wakati kipande cha noti kipo kwenye ATM yao?
Kwa hali hii ya uchumi inauma sana kupatwa na janga kama hili kwa sasa natembea na kipande cha pesa CRDB Bank hawakitaki na watoa huduma mtaani hawataki. Kumbuka ni pesa zangu na nimechajiwa kwa kutoa pesa na kodi juu.
Naomba management ya bank najua wanapita humu iangalie suala ya kuweka pesa safi hasa pale Ngulelo. Vilevile bank kuu watuasaidie wateja wa bank tunapoonewa kama hivi najua wanao uwezo huo.
Wenu victim wa pesa chafu, chakavu na Kipande cha noti Ngulelo Arusha.