Atimuliwa Baada Ya Kukiri Kuzini Na Shoga. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atimuliwa Baada Ya Kukiri Kuzini Na Shoga.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Oct 26, 2008.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Oct 26, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  http://en.wikipedia.org/wiki/Ted_Haggard

  http://www.ted-haggard.com/

  Mchungaji Ted Haggard (50), baba mwenye ndoa na watoto watano, alikuwa Rais wa shirikisho la Makanisa ya Kiivanjeli.National Association for Evangelicals.(NAE ) nchini Marekani.

  NAE inasimamia makanisa yapatayo 45,000 ikiwa na idadi wa wafuasi wasiopungua milioni 30. Haggard alianzisha kanisa lake mnamo mwaka 1985 na aliweza kuwavutia watu wengi ndani na nje hadi kuchaguliwa kuwa Rais wa NAE.

  Pia mchungaji Haggard licha ya kuwa mtu aliyekuwa akiheshimika sana, alikuwa ni mmojawapo wa marafiki wa Ikulu ya Marekani na chama cha Republican cha Rais Bush.

  Lakini hadhi na mamlaka yote hayo yalifikia kilele siku nne kabla ya uchaguzi wa Marekani baada ya shoga Mike Jones kujitokeza na kulifumua bomu hili la uzinzi na Haggard.

  Haggard alimchukiza "mpenzi" wake Jones ambaye kwa mujibu wake, walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi kwa miaka mitatu hadi Augusti mwaka huu. Mike alipoulizwa ni kwanini ameamua kujitokeza wakati huu wa uchanguzi alisema

  "Kwanza ninataka kuonyesha kukerwa kwangu na Haggard kwa unafiki wake wa kupiga kampeni ya kuzuia ndoa za watu wa jinsia moja"

  Mwanzoni Mchungaji Haggard alikanusha kuwa na uhusiano wa kingono kinyume cha maumbile na Jones. Alisema kuwa alikwenda kwa Jones kufanyiwa Massage. Pia katika wakati huo, alishawishika kununua madawa ya kulevya ambayo baadaye anasema aliyatupa. Alisema "Nilishawishika,nikanunua madawa lakini sikutumia niliyatupa".

  Jumapili ya tarehe5 Novemba, Haggard aliandika barua kwa waumini wake kukiri kuwa alikuwa na matatizo ya ngono kwa muda mrefu. Aliongeza kuwa alikuwa muongo na mnafiki kwa muda mrefu.

  Baada ya kusomwa waraka huo huko Colorado kwenye kanisa lake lenye washarika wapatao 15,000, kanisa lake rasmi liliamua kumtimua Haggard.
  Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi wa madhehebu ya kisasa ambayo yanatiliwa shaka na watu wengi kuanguka. Miaka ya themanini walianguka magwiji kama J. Baker na Jimmy Swaggart.

  Kimsingi uhuru na urahisi wa kufungua makanisa haya ndicho chanzo cha matapeli wengi kufanikiwa kudanganya watu na kuwaibia kwa jina la Mungu. Hebu fikria unatoa sadaka, askofu au mchungaji wako anazitumia kuhongea mashoga na kununua madawa ya kulevya.

  Kazi kwenu huko nyumbani ambako uamsho umekuwa fasheni ya hali ya juu hadi kwenye matelevisheni. Wafuatilieni viongozi wenu mjue wanaishi kimungu au la. Atakayethibitika kuwa kama Haggard mfukuzeni bila kujali kuwa ni mwanzilishi wa kanisa lenu.
   
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Dini jamani dini hizi
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama dini ndio tatizo. Tatizo hapa ni huyu firauni aliyekalia 'kiti cha Musa' huku akiwahadaa kondoo za Bwana wake... Sidhani kama ni mawazo ya dini aaliyokuwa aakiiongoza ndo yaliyompeleka kufanya makufuru aliyoyafanya..hivyo ahukumiwe kama yeye na si dini yake. Maana kama dini ndo inafundisha hivyo, hapo ndo kungekuwa na tatizo.

  Halafu hii habari naona inakuwa recycled.. nadhani ina umri wa kutosha hivi sasa zaidi ya 6 months..
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,285
  Trophy Points: 280
  Naamini uchafu huu, upo pia katika makanisa haya hapa nyumbani Tanzania. Wanapata wafuasi wengi kutokana na uwezo wa miujiza. Kutokana na watu kukumbwa na shida lukuki zinazochangiwa na umasikini uliokithiri, magonjwa, mapepo na imani za uwepo wa nguvu za giza wanajikuta wakiangukia katika dini hizi. Waumini wanaweza kufanyiwa chochote na viongozi wao. Tatizo kwa hapa wale wanaotendwa hawana ujasiri wa kujitokeza hadharani kufichua maswahibu yao.
   
Loading...