Athari za umaskini kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Athari za umaskini kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MwanaHaki, Sep 21, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Umaskini uliokithiri kwenye maeneo mengi hapa nchini unaelekea kuwa tishio la kuchangia kutokuwapo kwa mabadiliko yanayotarajiwa kwa kuwa hivi sasa asilimia kubwa ya Watanzania walio maskini wanatanguliza maslahi binafsi zaidi kuliko yale ya taifa.

  Hili limedhihirishwa na vijana wasio na ajira rasmi, wanaoshindwa kutwa kwenye vijiwe, ambao wamebuni sera ya "mtu kitu", ambapo wanadai kwamba, ili kupiga kura wanapaswa kulipwa kwa kuwa hawana ajira rasmi, hawawezi kupoteza muda wao kusimama kwenye foleni na kwenda kuwapigia kura viongozi watakaowawakilisha bila kulipwa.

  Huko mikoani, wengi wa viongozi wa vyama vya upinzani wanavikimbia vyama vyao na kuingia CCM kwa sababu kuu mbili: Vitisho kutoka kwa wagombea wa CCM kwamba wasipoichagua CCM watakosa fursa za maendeleo, na pili, rushwa ya fedha wanayopewa na viongozi na wagombea wa CCM, pamoja pia na ahadi za kupewa madaraka ya ngazi za juu kwenye serikali ijayo.

  Huu ni ufisadi uliokithiri, kwani mfumo huu hauna tija. Utaendeleza yale yaliyopo, kwa hiyo malalamiko yatabakia kuwa yale yale, tena maradufu zaidi.

  Umaskini utaipa CCM kura nyingi sana, kwa kuwa Watanzania wazalendo ni wachache sana. Ni vigumu kuwa mzalendo wakati unashinda njaa, huna uhakika wa kupata mlo mmoja kwa siku, hujui pesa ya kupata kifungua kinywa cha siku ijayo utaipata wapi.

  Lakini bado unaenda kuipigia kura CCM, ukitarajia ahadi zinazotolewa sasa ni za kweli. CCM kubadilika ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano. Haiwezekani!

  Nadhani imetosha kwa leo. Lakini msiwalaumu viongozi wa CCM mtakaowachangua iwapo hawatatimiza ahadi zao.

  -> Mwana wa Haki
   
 2. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anayenunua uongozi kamwe hatofanya kazi kwa maslahi ya wananchi walompigia kura. Kadhalika wanaonunuliwa kupiga kura hawana haki ya kudai chochote toka kwa mgombea waliyemchagua
   
Loading...