Imagine, kuna shule moja juzi nililazimika kupeleka binti yangu bording, darasa la nne wanalazimisha wakae boarding. Mtoto wangu ana mwili mdogo nilimuwahisha na hana nguvu za kupigana, kitu cha kwanza nilikuwa naogopa bullying shule (mateso toka kwa wenzake), pili matron wao nilisikia anafinya sana watoto na kuwapiga mkwara wasitoe siri, na watoto wengi wanatii amri hiyo ukiwauliza wanakwambia hatuteswi.
Nimelazimika kumfuata huyo matron na kumtoolea ya moyoni kwamba mimi naleta mtoto wangu hapa, najua mnawatesa, wakwangu uwe naye makini bora uwe rafiki yangu kuliko kuwa adui yangu ukimtendea baya hata ukisema asije kusema atanambia tu (na ndivyo mwanangu alivyo), nimekuja siku nyingie mwisho wa mwezi kumwangalia, nimejihakikisha kwa vyanzo vya intelijensia yangu kuwa mtoto wangu amemuweka dabodeka ya chini tena karibu na pale anapolala yeye ili amwangalia kwa ukaribu zaidi, ikabidi niongee naye kiume tu sasa uyo matron (biinti kama wa 30 hivi), na kumpa hela ya chai walau fifty.
Nitakuwa nampa za chai kumtia moyo hivyohivyo sio kwasababu hela haiumi lakini nahangaika mtoto wangu asiteswe na kunyanyasika nafsi. mambo kama hayo ndiyo yanafanya mtu akija kufanikiwa akiangalia wale waliokuwa wanamtesa, hana hamu nao kabisa.