Ateketea kwa moto aliouwasha shambani kwake

Ateketea kwa moto aliouwasha shambani kwake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
MKAZI wa kijiji cha Kilongo, Muheza mkoani Tanga,
Saidi Sekizenge (72), amefariki dunia kwa kuteketea kwa moto akiwa shambani kwake.

Tukio hilo lilitokea juzi katika kijiji hicho ambako Sekizenge alikuwa anaishi na familia yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, alisema mzee huyo alifariki dunia kutokana na kuungua na kuteketea wakati akichoma moto majani yaliyokuwa yamekauka shambani mwake.

Alisema wakati akichoma majani hayo shambani, ghafla moto ulimzidi nguvu kutokana na upepo mkali, hivyo kuhamia
katika mashamba ya watu ambayo wamepakana na shamba lake na moto kuanza kuyaunguza.

Kamanda Bukombe alisema baada ya moto huo kushika katika mashamba
ya watu wengine, Shekizenge alijaribu kuuzima ili usiendelee kuunguza mashamba hayo lakini alizidiwa na moshi wa moto.

Bukombe alisema baada ya kuzidiwa na moshi akiwa anazima, alizingirwa na moto, hivyo kushindwa kukimbia kutokana na ulemavu aliokuwa nao na hatimaye kuungua mpaka kuteketea kabisa.

Diwani wa Songa wilayani Muheza, Leslie Nchimbi, alisema baada ya tukio hilo, viongozi walitoa taarifa katika kituo cha Polisi Wilaya ya
Muheza.

Alisema polisi na daktari kutoka Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, walifika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi kisha kuruhusu mwili wake uzikwe baada ya uchunguzi.

ITV
 
Huyu ni shujaa wa taifa,nashauri moja ya barabara hapo Muheza ipewe jina lake kama kuenzi na kutambua mchango wake wa kufanya kazi kwa nguvu zote japokuwa hali yake ya ulemavu ilikiwa mwilini.
RIP mzee wetu,sio baadhi ya watu kupata upele tu wanataka kuishi kwa kuombaomba!!
 
Lakini moto haufichiki, ilikuwaje mpaka mtu anafariki ndio wanasimulia jinsi alivyopambana kuuzima? Ina maana msimuliaji alikuwepo eneo la tukio kwanini hakutoa msaada kwanza? Au kama marehemu alikuwa pekeyake hiyo nadharia imetokea wapi? R.I.P ndugu.
 
Sio lazima alikuwepo ni mazingira ya ajali ndio yanapelekea kutoa sababu hizo za mauti yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu angalia mzee wa miaka 72 tena mlemavu..anahangaika na maisha anatafta chchte maisha yasonge...wengine ht kushika jembe hawajui..wapo wapotu kazi kubet tu!lol..pumzika kwa amani mzee !
 
Huyu ni shujaa wa taifa,nashauri moja ya barabara hapo Muheza ipewe jina lake kama kuenzi na kutambua mchango wake wa kufanya kazi kwa nguvu zote japokuwa hali yake ya ulemavu ilikiwa mwilini.
RIP mzee wetu,sio baadhi ya watu kupata upele tu wanataka kuishi kwa kuombaomba!!
ni kweli ußsemayo ..inaumiza sana ..hili liwe funzo aisee
 
Poleni Sana wafiwa ndio hivyo tena
Wazee wa zamani ni kiboko huyu 72 anashika jembe Yule 74 kaepua jiko si mchezo respect kama zote
 
Back
Top Bottom