Mimi sitaraji jipya kwenye muundo huu wa utendaji na usimamizi. Masuala ya kitaaluma yanafanyika kisiasa na ya kisiasa yanafanywa kwa nguvu ya dola.
Ingia leo kwenye tovuti ya VETA na NIT, utashangaa na kama huna kitambi unaweza timua mbio. Chuo kinachojinasibu kuwa KINAFUNDISHA IT, website yake iko hoi. Lakini humo humo kwenye page ambazo hazijakuwa updated tangu 2009 utaona mtu kaandika wanafundisha WEB DESIGNING.
Hii ndio Tanzania na hao ndio watendaji wetu linapokuja suala la teknolojia ya mawasiliano. Jana nilienda HELSB kusubmit Payment Details za waajiriwa wa kampuni yetu wanaodaiwa. Nimewekwa kwenye benchi 67minutes nasubiri karani anatafuta taarifa za benki kwenye faili lenye kurasa si chini 200 kwa kalamu. Najiuliza, ufanisi uko wapi na yapi ni mazuri ya IT kwa nchi yetu?
Hapo ATCL si ajabu ukakuta vijamaa fulani vimeajiriwa kufanya wajibu huo. Vyenyewe vitakuwa aidha, vibrazamen au tuzee. Kama ni wazee, I reserve my comments na kama ni vijana basi huwa ni SSK (Suti Safi Kibaruani). Mashati saaafi ya dukani kama waimba kwaya, kikamba kimeshuka shingoni na kutokomea mfuko wa shati na kabeji saaaafi IT. Kazi kuvaa suruali za model na viatu vya kuchongoka mbele, website ya kampuni kichefuchefu. Wanapitapita tu makoridoni wakivuta muda ifike lunch time wakale juice na sambusa 2 kama mademu...pambaf!