ATCL kupeleka ndege Afrika Kusini pamoja na Airhostess walikuwa sahihi, tusichukulie kila jambo ni "ufisadi"

Yaani ndege nzima m5,? du wazalendo kweli kweli hawa na m10 juu.
Kumbe ni rangi juu ya rangi!
Amaa kweli hapa kazi tu.
rangi ya kisuzuki changu mchina kanipa proforma ya 2m. Kumbe hata machina ni mafisadi aisee, wacha tu tuendelee kupuliza rangi chini ya mikorosho.
Tanzania oyee.
 
Kuna wakati unaposikiliza hotuba za Mhe. Rais, zile ambazo amejijengea utaratibu wa kutuhutubia bila kuandika wala kusoma popote, basi unapata picha kuwa kuna baadhi ya wasaidizi wake, ama wanakuwa na ukosefu wa data za jambo fulani au ni vile wanafikisha lolote wanaloliona huko walikopandikizwa kwa sura ya ufisadi.

Wakati wa kumuapisha Balozi Mlowola, Rais kwa hotuba yake ya kusisimua, ameibua mjadala mkubwa sana ndani ya Taifa, mjadala unaochagizwa na kauli yake dhidi ya ATCL na ndege zake, mjadala unaoonyesha licha ya ukali wa Rais, lakini bado watu wanafisadi na kutumia mali za umma vibaya.

Wengi wameshangilia sana maneno yale ya Rais,
na kunogesha mjadala, Rais alitembelea "ATCL hangar" na kujionea jinsi ndege ilivyopakwa rangi kwa milioni 7, na kwa "Uzalendo" wa wapaka rangi, Rais akaongeza 10 ya juu.

Lakini tujiulize, hivi ni kweli katika kipindi hiki cha ukali na ufuatiliaji wa Rais bado kuna watu hawaogopi kiasi cha kutaka kuiba mbele ya macho ya bwana mkubwa? Tena uwizi ndani ya mahali ambapo jicho la Rais lipo saa 24? Maana katika nembo ya mafanikio ya awamu ya tano, basi ni kufufuka kwa ATCL na uwekezaji wa ndege mpya(Kwa hili nipo na JPM mpaka dakika ya mwisho).

Jambo la kufahamu ni kuwa, uwekezaji katika usafiri wa anga unahitaji gharama kubwa, hizo ni pamoja na gharama za malipo kwa nguvu kazi na malipo kwa ukarabati na uendeshaji wa ndege na vile vinavyoambatana navyo, sio kila jambo liangaliwe kwa jicho la "ufisadi" na sio kila jambo lisifiwe kwa jina la "kubana matumizi".

Tukienda na dhana hii, tutaliuwa shirika, tutafanya kazi chini ya viwango na tutapoteza "confidence" ya wataalamu kutushauri kitaalamu maana wanaogopa kuonekana ni sehemu wa mafisadi wanaotaka kujipatia pesa kwa njia ya ukarabati au uendeshaji wa shirika letu. Ifikie mahali, katika haya mambo ya kitaalamu, tuwaachie wataalamu wetu na hao tuliowapandikiza toka "Eagle House" waendelee kufanya kazi zao nyingine ambazo haziingiliani na utaalamu moja kwa moja.

Usafiri wa anga una taratibu zake kwa hatua ya kitaifa na kimataifa, wao wenye fani zao wanaita "Standards And Recommended Practices (SARPs)", ingawa hizi hazina "legal binding force" lakini walau nchi wanachama walioziridhia wanapaswa kuzifuata ili kuweka ule mfanano wa ubora wa viwango katika level ya kidunia.

Suala la upakaji wa rangi katika ndege
Hili bila shaka hata kwa mujibu ya kanuni na sheria za TCAA linadondokea kwenye kipengele cha "Marking and Manner of Affixation (hapa wanasheria watanisahihisha). Aircraft Registration and Markings Regualations zinatoa muongozo wa namna ndege inavyopaswa kupakwa rangi inapobadilika kutoka kwa "Operator" mmoja kwenda kwa mwingine.

Kwa hiyo, ndege aliyoisema Rais, Operator wake alikuwa ni TGFA, na logo pamoja na rangi ya TGFA ni tofauti na rangi na logo ya ATCL. TGFA rangi yake ya kujitambulisha ni nyeupe na blue bahari wakati rangi ya ATCL ni nyeupe na blue, nembo ya TGFA ni bibi na bwana wakati ya ATCL ni twiga. Hivyo ATCL walitaka kuondoa rangi hii yote pamoja na logo, na kwa kweli kwa viwango vya kimataifa (the bitter reality is - Tanzania can not do such kind of a thing).

Kuipaisha ndege kwenda Afrika Kusini ambapo walau watu waliangalia unafuu wa bei kulingana na sera za sasa ilikuwa ni jambo la lazima na la kawaida sana. Sisi hatujafikia viwango hivyo, huo ndio ukweli. Hao waliosifiwa si kwamba wamefanya kile kilichotakiwa kwenda kufanywa Afrika Kusini, ila wamechomeka tu logo kwenye ubavu na sehemu za fusalage, fuel tanks, tail boom na engine cowling.

Hii ni kama Fastjet na rangi ya njano, nyeupe, nyekundu na kasuku na muito wake uliita kama "Gray bird" maana logo yake ilikuwa ni kasuku wa kijivu. South Afrika ni rangi za bendera yao na mnyama jamii ya swala(Springbok) na muito wake popote duniani huitwa kama "Springbok" kwa hiyo huwezi kui-brand South Africa bila uwepo wa hizo rangi zake, na hili ndio ATCL walikusudia kulifanya.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa kanuni hizi za usajili, nadhani zinataka marks, design pamoja symbol zishabihiane na operator. Ila kwa sababu labda TCAA, TGFA na ATCL wote ni watoto wa baba mmoja, hili si tatizo, lakini hata kama si tatizo basi isijenge picha kuwa kulikuwa na dalili ya ufisadi kwa watu wa ATCL kumbe wao walikuwa wanafuata Standards tu na ndio maana ukiangalia rangi ya mstari wa ubavuni na ule wa maandishi ya ATCL katika hiyo ndege iliyopakwa rangi, utagundua kuwa zile ni blue mbili zinazotofautiana. Ya ubavuni kwenye mstari ni blue ya TGFA na kwenye neno "Air Tanzania" ni blue ya ATCL.

Na lengo la ATCL lilikuwa ni kukwangua ndege nzima na kupaka rangi na logo za ATCL na kuondoa zile za TGFA, kitu ambacho ni Standards za usafiri wa anga, ila sababu mwenye nazo kaamua wapake rangi juu ya rangi, basi wale walioamua kuipeleka Afrika Kusini isionekane walikuwa wezi. Ila, tuwe tu tayari kwa matokeo ya kupaka rangi juu ya rangi.

Kimsingi ndege zote za ATCL ni za TGFA, na serikali ilifanya hivyo ili tusipokwe na wanaoidai ATCL yetu.

Kuhusu Air Hostess kuwamo ndani ya ndege
Hili la Air Hostage(nadhani alimaanisha air hostess), halo halikuwa la kusemwa hadharani maana ni kama waliomfikishia Rais taarifa hizi wakidhani wameibua ufisadi ni kama tu na wao wamejiabisha.

Ndege ya aina ile inapokuwa na safari ndefu nje ya nchi kama Afrika Kusini, ni lazima ibebe hata Flight Attendants wawili, na hii ndio standard, tunapotaka mambo mazuri basi tukubali na gharama zake.

Flight Attendants ni sehemu ya "Cabin Crew", hawa zaidi ya kutugawia chai na kalimati tunaposafiri, wao pia ni wanahusika na mambo ya safety kwa cockpit crew, ndio watoa huduma ya kwanza kama rubani mmoja ataugua ghafla akiwa angani, hawa wana kazi zaidi ya ile tunayodhania, hawa kusafiri na ndege ikiwa haina abiria a safari ndefu ni moja ya hitaji muhimu la kiusalama angani, na pia hata anaongezeka injinia ambaye anapaswa kuwepo ili kutoa msaada wa tatizo la kiufundi ndege ikiwa angani.

Hivyo hawa kujumuishwa katika safari ni hitaji la kiusalama na sio ufisadi, kama tunataka mambo mazuri basi tukubali na gharama zake. Kuna incidence nyingi ambapo cabin crew wamesaidia marubani wakati wa hatari angani na kuokoa maisha ya marubani.

Hivyo, kuna wakati tusidhani kila kilicho nafuu ni faida, nafuu nyingine ni aghali. Na tusitazame kila jambo kwa mentality ya kuwa tunaibiwa ili tuweze kuwa wa kimataifa na tukidhi viwango ni lazima tukubali pia kutumia gharama.

Yote kwa yote, pongezi zimwendee Mh. Rais kwa jinsi anavyolipa nguvu shirika letu na kutufanya sasa na sisi tupatikane katika rada za usafiri wa anga duniani, naona mpaka walio USA wanatuchungulia kwenye flight radar na kutuombea mabaya. Kwenye hili la ATCL, wengi tupo na JPM mpaka tone la mwisho cha muhimu wale waliopandikizwa, wasiangalie kila jambo kwa jicho la ufisadi, tutaendesha mambo chini ya kiwango.
Usitete uhalifu wa kodi zetu. Hizo ni kuchezea kodi zetu. Kuna umuhimu gani wa kutumia zaidi Milioni 200 wakati kazi hiyo inaweza kufanyika ndani ya nchi kwa chini ya Milioni 10. Usitete ufisadi,labda kama na wewe moja wa wanufaika.
 
Mkuu kukwangua rangi ya ndege ili uipake upya inahitaji chemicals na wataalamu wa hiyo kazi. Halafu Magufuli anakuja kupiga kelele za kiki za kisiasa eti ameokoa Tshs 160 walitaka kuzifanyia ufisadi. Hivi analinganisha jinsi hiyo ndege ambavyo imepakwa rangi hapa TZ na jinsi ambavyo ingepakwa rangi nje? Anajisifia kuokoa fedha kwa kuamuru watu wapake rangi juu ya rangi kwa kutumia brashi!

Acheni kutetea upigaji wa kodi za wananchi. kama hata kubadilisha rangi hatuwezi hunger tulizo nazo za kazi sasa. Eti kwa kiwango cha kimataifa lazima rangi ipakwe nje ya nchi. Acheni upuzi wa kutetea ufisadi.
 
Je, ikichorwa tanzania na watanzania haikubali?
Je, itazuiwa kuruka tanzania kwa kuwa haijapakwa nje kwa mabeberu?
Je, inaweza kuanguka kwa kuwa imepakwa rangi na watanzania?

Mjifunze na nyie kuabana matumizi,msiwe watumwa wa fikra. Ipo siku mtasema na shell za hapa hazifai kufanya refuel hadi ziende ulaya
 
Soma tena utaelewa.
 
1. UZITO UNAKUWA ZAIDI YA ULE ULIOKUSUDIWA.
2. RANGI INAKUWA SIO BORA, HIVYO HAIWEZI KUDUMA WALA KULETA MUONEKANO MZURI.
3. NDEGE INA SENSORS NYINGI SANA, HALI HII INAWEZA KUSABABISHA BAADHI ZIKAFUNIKWA NA RANGI NA KULETA
FAULT NYINGI AMBAZO ZINAWEZA KULETA MADHARA AU KUONGEZA GHARAMA ZA MATENGENEZO.

MENGINE WATAONGEZA WATAALAMU HIYO KUTOKA KWENYE BASIC YA KAWAIDA KABISA KWENYE ENGINEERING.
Au labda rangi hizi za kawaida zitasababisha isisome kwenye Rada. Kama itasoma basi poa twende kazi
 
Kupaka rangi ju ya rangi sio hoja lakini ungesema kwa kawaida kupaka rangi ya kitalamu kwenye ndege kama hiyo ni kiasi gani? Ubishi uko kwenye bei Tzs.200M ambayo tumeiona ni kubwa
 
Acheni kutetea upigaji wa kodi za wananchi. kama hata kubadilisha rangi hatuwezi hunger tulizo nazo za kazi sasa. Eti kwa kiwango cha kimataifa lazima rangi ipakwe nje ya nchi. Acheni upuzi wa kutetea ufisadi.
Tatizo mnabisha mambo msiyoelewa. Hivi unafikiri kupiga rangi ndege ya abiria ni sawa na kupiga rangi gari? Inawezekana tatizo lako ni lugha au mapenzi yaliyopita kwa Jiwe, au ugonjwa wa Uzalendo Induced Logic Deficiency Syndrome - UIDS.

In-service experience has taught us that even activities performed on the aircraft mainly for cosmetic reasons, like washing or painting, may have an impact on the safety of operations.

The in-service incidents described in this article illustrate the need to care-fully follow the indicated instructions available in the Aircraft Maintenance Manual, Structure Repair Manual as well as Tool and Equipment Manual.
 
Nimejaribu kufuatilia clip moja hivi JPM akijaribu kupiga mahesabu ya kusafirisha ndege nje ya nchi na gharama za kufanyia shughuli zote hapa hap nchini ()..
Niliyojifunza sasa ndo yakanisikitisha..
1. Washauri wake wanamuogopa sana.
2. Hawapi nafasi ya kujenga hoja ili apewe maelezo ya kitaalamu
3. Anajua kila kitu yeye
4. Anafanya maamuzi kwa kukurupuka
5. Yeye ni bora gharama iwe ndogo bila kuzingatia vigezo vya ubora
6. Anapenda sifa na kusifiwa
7. Hafikirii madhara ya maamuzi yake..

Hivi kweli kupaka ndege rangi ni sawa na kupaka gari la kutembelea..?
With all that air friction na weather changes up there milioni tano tu zinatosha?

Haki watakaonijibu kuwa inawezekana naomba wanipe mawasiliano ya hao wapakaji... May be naweza kuwapa yale malori wakanipakia rangi.. Price ni lazima itakuwa chini ya laki 5..
 
Nimejaribu kufuatilia clip moja hivi JPM akijaribu kupiga mahesabu ya kusafirisha ndege nje ya nchi na gharama za kufanyia shughuli zote hapa hap nchini
Niliyojifunza sasa ndo yakanisikitisha..
1. Washauri wake wanamuogopa sana.
2. Hawapi nafasi ya kujenga hoja ili apewe maelezo ya kitaalamu
3. Anajua kila kitu yeye
4. Anafanya maamuzi kwa kukurupuka
5. Yeye ni bora gharama iwe ndogo bila kuzingatia vigezo vya ubora
6. Anapenda sifa na kusifiwa
7. Hafikirii madhara ya maamuzi yake..

Hivi kweli kupaka ndege rangi ni sawa na kupaka gari la kutembelea..?
With all that air friction na weather changes up there milioni tano tu zinatosha?

Haki watakaonijibu kuwa inawezekana naomba wanipe mawasiliano ya hao wapakaji... May be naweza kuwapa yale malori wakanipakia rangi.. Price ni lazima itakuwa chini ya laki 5..
Tatizo watu hawajajifunza juu ya Magufuli kujifanya anajua kila kitu kwa gua ya uzalendo. Kalivuruga la korosho na kuleta hasara kubwa. Sasa anaingilia ndege.

Nadhani siku ndege hizi zikianguka watu wakafa ndio watajua ni jinsi gani kuingilia kisiasa vitu vya kitaalamu kunavyoweza kuleta madhara. Ndege sio korosho bwana.
 
1. UZITO UNAKUWA ZAIDI YA ULE ULIOKUSUDIWA.
2. RANGI INAKUWA SIO BORA, HIVYO HAIWEZI KUDUMA WALA KULETA MUONEKANO MZURI.
3. NDEGE INA SENSORS NYINGI SANA, HALI HII INAWEZA KUSABABISHA BAADHI ZIKAFUNIKWA NA RANGI NA KULETA
FAULT NYINGI AMBAZO ZINAWEZA KULETA MADHARA AU KUONGEZA GHARAMA ZA MATENGENEZO.

MENGINE WATAONGEZA WATAALAMU HIYO KUTOKA KWENYE BASIC YA KAWAIDA KABISA KWENYE ENGINEERING.

Mie aomba unisaidie kitu kimoja ile niongeze ufahamu wangu. Swali kubwa ambalo limekuwa likinisumbua upi haswa ni umri wa ukomo kwa ndege kufanya kazi. Majibu mengi niliyoyapata baada ya pekua pekua yangu ni kwamba inategemea na masaa yaliyotumika, na aina ya ndege. Labda unisaidie majibu ya maswali haya:

(i) Je, kwa mujibu wa watengenezaji wa ndege hizi husika, je, zilitakiwa kuwa zimeruka masaa mangapi kabla ya kuonekana kwamba hazifai kuruka tena?

(ii) Je, hizi za kwetu, zimesharuka masaa mangapi?

(iii) Je, ni kiwango gani cha fatigue kunaweza kuongezeka kwa kuandika maandishi ‘Air Tanzania‘ na kuchora twiga kwenye ndege ya fokker 50? Kwani ni uzito kiasi gani wa rangi iliyotumika?

(iii) Je, kwa kuandika maandishi ‘Air Tanzania‘ na kuchora twiga kwenye ndege ya fokker 50, ni sensors gani zinaweza kuhitilafiwa?

Natanguliza shukrani.
 
Tatizo mnabisha mabo msiyoelewa. Hivi unafikiri kupiga rangi ndege ya abiria ni sawa na kupiga rangi gari? Inawezekana tatizo lako ni lugha au mapenzi yaliyopita kwa Jiwe, au ugonjwa wa Uzalendo Induced Logic Deficiency Syndrome - UIDS.

In-service experience has taught us that even activities performed on the aircraft mainly for cosmetic reasons, like washing or painting, may have an impact on the safety of operations.

The in-service incidents described in this article illustrate the need to care-fully follow the indicated instructions available in the Aircraft Maintenance Manual, Structure Repair Manual as well as Tool and Equipment Manual.
Sina mapenzi na mtu yoyote na sina tatizo la lugha, nina uchungu na matumizi mabaya ya kodi zetu. hayo ni matumizi mabaya ya kodi zetu na kutokuwa na huruma na Watanzania.
 
Vema sana. Sasa katika masuala ya usalama, hasa wa ndege, suala la kubana matumizi halipaswi kuingia hata kidogo. Hakuna mtu anayepinga kuokoa kodi za watu, lakini isiwe kwa kufanya maamuzi ya kisiasa kwenye suala la usalama, utaingia gharama kubwa hata zaidi, kama sio kupoteza maisha ya watu gharama ambayo haikadiriki.

Wewe unaambiwa, kuna ndege ilianguka kwa kuoshwa vibaya tu, na leo unaenda mbali kusema acha mafundi rangi wetu wapake ndege rangi. Na ukiambiwa ndege zikaoshwe nje kutokana na ajali ya Air France, utakataa?

Na pia watu wanatakiwa kuelewa kwamba haya mambo ya Magufuri kuingiza uamuzi wa kisiasa kwenye mambo ya kitaalamu ya ndege, IATA wanaweza kutupiga marufuku hizo ndege tukaziendeshe viwanja vya ikulu. Haya mambo balozi wa nchi za nje wanayasikia. Unaweza kukuta hata hizo Dreamliner haziruhusiwi kuruka nje ya Tanzania kwa kuwa watu wasiojua wanajifanya wajuaji wa aircaft management
 
Back
Top Bottom