ATCL kupasua anga India na China

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
2,000

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inakamilisha taratibu za kidiplomasia ili kuwezesha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kuanza safari za moja kwa moja kwenda India na China.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi, Isack Kamwelwe, wakati wa mahafali ya kwanza ya wahudumu wa ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Amesema taratibu hizo baina ya serikali ya mataifa hayo, zitakamilika karibuni. Alisema kutokana na hatua hiyo, safari hizo zinatarajiwa kuanza mwisho wa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao hasa nchini India.

Waziri huyo pia alieleza kuwepo kwa mikakati mbalimbali ya kuwezesha ndege za ATCL kwenda katika mataifa mbalimbali ikiwemo nchi za Ulaya.

Amesema katika kuhakikisha wanaliboresha zaidi shirika hilo, serikali ilitenga Sh bilioni 900 ambazo zimeelekezwa katika ununuzi wa ndege.

Amesisitiza kuwa kutokana na jitihada hizo, uwepo wa kada hiyo ya watoa huduma wa ndani ya ndege ni muhimu huku akiipongeza NIT kwa kuanzisha kozi hiyo.

"Tunatarajia hadi itakapofika mwishoni mwa mwezi wa tano ndege zetu zitaanza kuruka kwenda nchini China, pamoja na hilo serikali pia imekuwa ikiendelea na ujenzi wa viwanja mbalimbali nchini, lengo ni kuhakikisha tunaliwezesha shirika letu kukua siku hadi siku," alisema Kamwelwe.

Aidha, Kamwelwe alisema NIT ina jukumu kubwa la kuhakikisha kinazalisha wataalamu wa kutosha, watakaotoa msaada katika kuliendeleza shirika hilo na hivyo kukabiliana na uhaba uliopo nchini hivi sasa.
 
bababikko

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,393

kwa kuwa hamtaki kuwalipa konoike hii itadakiwa mumbai izuiliwe mpaka jiwe alazimishwe kulipa 61m$$$
 
Mvuvi_papa

Senior Member
Oct 25, 2012
141
225
Ndege yenyewe hiyo moja kweli itafanikisha hizo safari za mbali?. Pia hii issue ya Boeing nayo ni majanga watu wanaanza kuziogopa with preferences kwa AirBus
 
utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
2,496
2,000
KONGORE KWA SERIKALI. .
Ila mkuu ungetumia picha hii kuzima kelele za upand ule tuujuao maana hauchelew kuja na kelele kisa picha
dreamliner1%2Bpic.jpg
images.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,407
2,000
Dreamliner haiwezi kuruka mpaka ziwe mbili maana kiitifaki inabidi uwe na ndege mbili ili uweze ku cover incase moja inamushkeli au imegoma kwenda
 
iokote

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
597
1,000
Kwani hizi zilizonunukiwa zilipitia bajeti gani hizi ndege ni nje ya bajeti maana zilinunuliwa cash
Baada ya CAG kuweka wazi madudu, sidhani kama watafanya tena yale makosa waliyofanya awali.

Kwa sasa italazimishwa budget ya ndege iingie kwa hali yoyote ile ili kuficha makando kando.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,407
2,000
Baada ya CAG kuweka wazi madudu, sidhani kama watafanya tena yale makosa waliyofanya awali.

Kwa sasa italazimishwa budget ya ndege iingie kwa hali yoyote ile ili kuficha makando kando.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaishi nchi gani? CAG hajakagua ATCL pia hizo helw zinachotwa na zinapelekwa Vote 20 ambako hakuna ukaguzi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom