ATCL kuanza safari za kwenda Afrika Kusini

ATCL kuanza safari za kwenda Afrika Kusini

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019
1075093

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) karibuni linatarajia kuzindua safari mpya za kwenda Afrika Kusini, ambapo ndege ya kwanza kuruka kwenda jijini Johannesburg itaruka Julai mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema kuwa watatangaza nauli na kuanza kutangaza safari hizo watakapoanza kuuza tiketi.

Hatua hii kubwa ya kuendelea kupanuka kwa shirika hilo inakuja ikiwa ni miezi miwili tangu lilipozindua safari mpya za kwenda Harare nchini Zimbabwe na Lusaka nchini Zambia.

Safari ya kwenda Afrika Kusini itakuwa ni safari ya tano ya kimataifa kuzinduliwa na ATCL baada ya Harare, Lusaka, Bujumbura na Entebbe.

Baada ya kuzindua safari hiyo, Matindi amesema kuwa shirika hilo litajiandaa na safari za kwenda Mumbai (India) na Guangzhou (China) ambapo maandalizi yake yamefikia katika hatua nzuri.

Ameongeza kuwa safari hizo zitazinduliwa mara tu mazungumzo na mamlaka kwenye nchi hizo yatakapokamilika.

Kwa sasa shirika hilo linalofufuka baada ya kutofanya vizuri sokoni kwa miaka mingine lina ndege nane ambazo ni, Bombardiers Q-400s tatu, Airbus (A200-300) mbili, Fokker50, Fokker28 na Boeing 787-8 Dreamliner.
 
Hii route ya dar-joburg imekua pasua kichwa sana. Kila anayejaribu kushindana na SAA kwenye hii route anachemka. Kuna wakati precision nadhani walijaribu wakashindwa..fastjet walijaribu wakashindwa..kulula/british airways walijaribu wakashindwa. Ngoja tuone kama air tanzania wataweza. Kukiwa na ushindani angalau bei itashuka maana saa hizi SAA anajichagulia tu nauli ya kutoza maana yupo peke yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa jamaa kila siku wanakuja na single mpya.

Mpaka 2020 October inafika, si ajabu hakuna safari itakayokuwa imeanza.
 
Zambia imeshaanza kwenda???
 
Waanzishe route ya DSM to Mogadishu itawalipa sana. Kule kwetu Ntwala tunasema ndani ntiti nje ntiti fulu nyomi
Tunashukuru lakini hatujakuelewa mku fafanua kwa luga yetu pse iwe musigazi.
 
Yeye Zitto kabwe kule bungeni anashauri MAMLAKA ya usimamizi wa ndege irudishwe wizarani ( Ya Uchukuzi) labda CAG anaogopa kukagua likiwa chini ya Ofisi ya Rais. Huyu jama sikumuelewa mchango wake Bungeni. Au anataka zirudi kabisa kwa ATCL wazungu waje wazipige bei?
 
Tatizo hili shirika halikua na business plan
Actually mimi naona kama wanaenda vizuri. Watu wengi wanalalamika kwamba hazijaanzishwa route za nje ya afrika. Lakini lamza uelewe kwamba route za nje ya afrika haziwezi kua sustainable bila kuwa na network kubwa ndani ya afrika. Yaani ni lazma mtu aweze kutoka asia au ulaya au marekani aje dar then aconnect kwenda sehemu nyingine afrika. Nadhani ndio maana matindi ameweka nguvu kubwa kwenye kujenga network kubwa ya afrika kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii route ya dar-joburg imekua pasua kichwa sana. Kila anayejaribu kushindana na SAA kwenye hii route anachemka. Kuna wakati precision nadhani walijaribu wakashindwa..fastjet walijaribu wakashindwa..kulula/british airways walijaribu wakashindwa. Ngoja tuone kama air tanzania wataweza. Kukiwa na ushindani angalau bei itashuka maana saa hizi SAA anajichagulia tu nauli ya kutoza maana yupo peke yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Wa SA asilimia kubwa wanapands SAA
 
ni vizuri kama tutafikia kwenye utekelezaji...maana matamko mazuri ya china na india yalianza mda mrefu tuu.......Lalafu kimya
 
Back
Top Bottom