ATCL fanyeni kama Fastjet

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Ni kweli serikali inataka faida ili irudishe pesa iliyotumika kununulia ndege 8. Lakini bei ya ticket bado zipo juu sana.

Hivyo mjitahidi kufanya kama ilivyokuwa Fastjet ili kila Mtanzania afaidi.
 
Wamekusikia, watalifanyia kazi shuri lako...

Hili lipo hata kwenye bidhaa za ndani, utakuta bidhaa za ndani bei kubwa, bidhaa za nje bei ndogo...

Cc: mahondaw
 
Fast jet walikuwa wajanja ndani ya ndege wanaweka siti chache za Bei rahisi..sijui kwann ATCL hawaigi
 
Nalanda nawe kuiga jambo jema sio dhambi, igeni hapa Air Tanzania ; The Wings of Kilimanjaro 🦒🇹🇿
 
Mtapanda tu Mpende Msipende maana hakuna Tena Ndege itakayofanya Biashara ya ushindani na ATcL.
 
Ni kweli serikali inataka faida ili irudishe pesa iliyotumika kununulia ndege 8. Lakini bei ya ticket bado zipo juu sana.

Hivyo mjitahidi kufanya kama ilivyokuwa Fastjet ili kila Mtanzania afaidi.
FastJet ilikuwa ni low cost airline. Unajua maana ya low cost airline na lengo lake ni nini? Unajua ina operate namna gani? Wanachoweza kufanya ni kuanzisha kampuni tanzu ya low cost airline kwa lengo la watu wa kiwango cha chini.
 
Ni kweli serikali inataka faida ili irudishe pesa iliyotumika kununulia ndege 8. Lakini bei ya ticket bado zipo juu sana.

Hivyo mjitahidi kufanya kama ilivyokuwa Fastjet ili kila Mtanzania afaidi.

Mkuu unaweza kutueleza utaalam wako katika mambo ya Air Travel na ticketing?
 
Ni kweli serikali inataka faida ili irudishe pesa iliyotumika kununulia ndege 8. Lakini bei ya ticket bado zipo juu sana.

Hivyo mjitahidi kufanya kama ilivyokuwa Fastjet ili kila Mtanzania afaidi.
Linganisha kati ya atcl na precision
Utagundua atcl wako juu sana
Screenshot_20191215-180517_Chrome.jpeg
Screenshot_20191215-180556_Chrome.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanatakiwa wapunguze gharama. Kama kutoka Dar mpaka Mumbai ni $378 kwenda na kurudi yaani Tshs.875,070 mwendo wa masaa sita kwenda na kurudi masaa sita hivyo kwa saa moja ni Tshs.72,922 lakini Dar mpaka Mwanza kwenda na kurudi ni wastani wa Tshs. 420,000 au zaidi lakini mwendo wa saa moja kwenda na kurudi saa moja. Ukigawanya unalipa kwa masaa mawili moja kwenda na nyingine kurudi unalipa Tshs.210,000 kwa saa kwa safari ya Dar-Mza na kurudi. Hivyo bado ATCL kwa safari za ndani bado bei yao iko juu sana. Ni budi wapunguze bei zao.
 
Wamekusikia, watalifanyia kazi shuri lako...undefinedHili lipo hata kwenye bidhaa za ndani, utakuta bidhaa za ndani bei kubwa, bidhaa za nje bei ndogo...undefinedundefinedundefinedCc: mahondaw
kuna ukweli ndani yake. mitumba ya nje against nguo za viwanda vya ndani. Nawaza kwa sauti iwapo kama hati punguzo litatolewa
 
FastJet ilikuwa ni low cost airline. Unajua maana ya low cost airline na lengo lake ni nini? Unajua ina operate namna gani? Wanachoweza kufanya ni kuanzisha kampuni tanzu ya low cost airline kwa lengo la watu wa kiwango cha chini.
Nia kubwa ya serikali ni kutoa huduma kwa wananchi.habari za biashara za nini?
 
Back
Top Bottom