ATCL chukueni maamuzi magumu

ATCL chukueni maamuzi magumu

njuga

Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
24
Reaction score
16
Tarehe 10 Machi 2018 nimesafiri toka Dsm mpaka Kilimanjaro. Safari ilitakiwa ianze SAA 11:40 lakini tukaondoka SAA sita na robo usiku. Kisa ni kupata hitilafu ya kiufundi huko mwanza.

Kabla ya Bomberdier tulikuwa na cs 300 ndege iliyoweza kufanyakazi katika kipindi chote.

Lakini baada ya kupata mpya wakatelekeza ya zamani Kyle hangani. Ukiuliza eti wanasema imekaa muda mrefu ni ngumu kuiamsha kwani ni gharama.

Mheshimiwa wa Waziri Mbarawa na Mwenyekiti wa bodi ATCL fanyeni jitihada za makusudi ili huyo twiga aliyelala aamka.

Usiache mbachao kwa msala upitao.
 
Kuna kitu hakipo sawa ATCL, kila siku kuna malalamiko kuhusu hili shirika. Nadhani kuna kitu inabidi kifanyike
 
Shirika kama shirika liko sawa na wanajitahidi saana, tatizo lipo katika ushindani wa kibiashara, chuki, wivu na kutothamini vya kwetu.

Abiria wanapata matatizo katika mashirika karibu yote ya ndege hapa nchini tena yanayofanana lkn kwingine wanaona ni bahati mbaya, wavumiliwe na ni hali ya kawaida, ikitokea ATCL lalalala matatizo yote ya FASTJET,P/AIR NK yatalundikwa kwa ATCL ili lionekane limeshindwa.

Tujifanyie clinic sisi wenyewe hivi kweli tunajivunia mafanikio haya, tupo pamoja kwenye changamoto za kibiashara, wapo walioacha kazi na wanapenda kurudi lkn nafasi hakuna kundi hili linachuki.

Wapo ambao wanapenda kona, kona hawataki kuendana na wakati kujiiinua kimafunzo kwa kufuata taratibu sahihi hawa wana wivu.

Tuliunge mkono ni la KWETU.
 
Shirika kama shirika liko sawa na wanajitahidi saana, tatizo lipo katika ushindani wa kibiashara ,chuki ,wivu na kutothamini vya kwetu.

Abiria wanapata matatizo katika mashirika karibu yote ya ndege hapa nchini tena yanayofanana lkn kwingine wanaona ni bahati mbaya ,wavumiliwe na ni hali ya kawaida, ikitokea ATCL lalalala matatizo yote ya FASTJET,P/AIR NK yatalundikwa kwa ATCL ili lionekane limeshindwa.

Wapo ambao wanapenda kona,kona hawataki kuendana na wakati kujiiinua kimafunzo kwa kufuata taratibu sahihi hawa wana wivu.

Tuliunge mkono nila KWETU.
Malofa chadema ndio zao kuhujumu taifa
 
Tuliunge mkono nila KWETU.[/QUOT
Endelea kutetea shirika mfu hili mana biashara ya ushindani imeshawashinda mmebaki na kauli kama hizi unazotoa wewe kuwa matatizo yapo hadi fastjet ungekuwa unapanda hizi ndege usingetetea ujinga hapa..kiufupi ndege ni mbovu hizi mana kughairi safari na kubadilisha muda wanaotaka wao ni kitu cha kawaida kwao +huduma mbovu na wanajisifu kuwa wapo kwenye soko la ushindani..shame.
 
Malofa chadema ndio zao kuhujumu taifa
Yapo mambo ya vyama na yapo mambo serious ya kulitetea Taifa na Mali zake CCM ni chama dola kisimamie Sera zake na kikubali kukosolewa.

Huu ni ukweli usiopingika, kilikosolewa na kikajikosoa na ndio maana kiko hivi kilivyo.

Wapinzani nao ni WATZ wasikilizwe,wasipuuzwe.
 
Si umeona tatizo kubwa la kiushindani lililojaa wivu na chuki.

Mimi hata hunifahamu unasema natetea ujinga, Mimi hata hunifahamu unasema ningekuwa napanda hizo ndege.

Jifunze kutetea hoja uliyonayo. Kama ni Mtanzania mpenda haki, toa ushauri nini kifanyike
 
ATCL Hawajawahi kuwa na ndege za Bomberdier Cs 300 ila wanatarajia kuzipata siku za karibuni, unayoizungumzia nadhani itakuwa ATR iliyopakiwa kwenye Hangar. Kulikuwa na CRJ 200 ya kukodi wakati fulani lakini baada ya kuwasili zile mbili mpya haionekani kitambo sasa. ATCL ni shirika letu na binafsi ningependa kuliona likirudia enzi zake za miaka ya 80.

Hizo changamoto zipo kwenye mashirika yote yanayotoa huduma nchini lakini ndizo za kuangalia kwa makini maana zikizidi sana zitalirudisha shirika kule kubaya linakojaribu kutoka. Naamini zikifika zile nne kama ilivyopangwa shirika litakuwa na vitendea kazi vya kutosha kwa kuanzia, nitashangaa sana tu, kama mambo ya kuendesha shirika kipuuzi yatajirudia tena.
 
Nia ya kuleta Uzi huu sio kubeza ATCL kwa vile sisi ni wazalendo tunaeleza ukweli ili kujitathmini. Kama tutafufua ndege ile iliyopo hangani tutaweza kupambana na ushindani.
Nashukuru kwa hiki ulichokieleza lkn hebu nijibu hili umetaja ndege CS 300 Kuwa ni mbovu iko HANGA.

Je ndege zinazotegemewa kuja mwaka huu ni ndege aina gani?

Baada ya kuingia ATCL kwenye ushindani wa Anga nauli zimepanda au zimeshuka.?

Fedha inayokusanywa na ATCL inakwenda wapi? na kufanya nn?

Ndege kuahirishwa imetokea Mara ngapi? Na kwa sababu gani? Je majira haya ya mvua ni ajabu safari kuahirishwa sababu ya mazingira?
 
Shirika kama shirika liko sawa na wanajitahidi saana, tatizo lipo katika ushindani wa kibiashara ,chuki ,wivu na kutothamini vya kwetu.

Abiria wanapata matatizo katika mashirika karibu yote ya ndege hapa nchini tena yanayofanana lkn kwingine wanaona ni bahati mbaya ,wavumiliwe na ni hali ya kawaida, ikitokea ATCL lalalala matatizo yote ya FASTJET,P/AIR NK yatalundikwa kwa ATCL ili lionekane limeshindwa.

Tujifanyie clinic sisi wenyewe hivi kweli tunajivunia mafanikio haya, tupo pamoja kwenye changamoto za kibiashara, wapo walioacha kazi na wanapenda kurudi lkn nafasi hakuna kundi hili linachuki.

Wapo ambao wanapenda kona,kona hawataki kuendana na wakati kujiiinua kimafunzo kwa kufuata taratibu sahihi hawa wana wivu.

Tuliunge mkono nila KWETU.
Kuna changamoto nyingine ni za kipuuzi kwa mfano Ndege inamsubiri waziri aliyechelewa Airport.
 
Si umeona tatizo kubwa la kiushindani lililojaa wivu na chuki.

Mimi hata hunifahamu unasema natetea ujinga, Mimi hata hunifahamu unasema ningekuwa napanda hizo ndege.

Jifunze kutetea hoja uliyonayo. Kama ni Mtanzania mpenda haki, toa ushauri nini kifanyike
Unatetea ujinga kwa hoja za kitoto una ufinyu wa mawazo yani karne hii ya 21 mtu kama wewe unalialia kuwa shirika linaonewa wivu na kuna watu wana husda sasa katika biashara ulitaka ATCL ibaki peke yake ? Afu unataka nitoe ushauri labda uwe mgeni humu kuna mada zimeshaletwa mara nyingi kuhusu hili shirika na watu tumetoa ushauri mara nyingi tu kichekesho ni pale unapowachelewesha abiria wasafiri wengine kisa unamsubiri waziri halafu unakuja kusema wanaonewa wivu..changamsha ubongo huo.
 
Anyway kuelewa nacho ni kipaji, kama ilivyo kutukana na kukashifu, vingine vinaletwa na taswira ya MALEZI siwezi kulaumu.
 
Shirika kama shirika liko sawa na wanajitahidi saana, tatizo lipo katika ushindani wa kibiashara, chuki, wivu na kutothamini vya kwetu.

Abiria wanapata matatizo katika mashirika karibu yote ya ndege hapa nchini tena yanayofanana lkn kwingine wanaona ni bahati mbaya, wavumiliwe na ni hali ya kawaida, ikitokea ATCL lalalala matatizo yote ya FASTJET,P/AIR NK yatalundikwa kwa ATCL ili lionekane limeshindwa.

Tujifanyie clinic sisi wenyewe hivi kweli tunajivunia mafanikio haya, tupo pamoja kwenye changamoto za kibiashara, wapo walioacha kazi na wanapenda kurudi lkn nafasi hakuna kundi hili linachuki.

Wapo ambao wanapenda kona, kona hawataki kuendana na wakati kujiiinua kimafunzo kwa kufuata taratibu sahihi hawa wana wivu.

Tuliunge mkono ni la KWETU.

Nani analundika matatizo ua FastJet na PA kwa ATCL?
Naona unaishi hangani kama hiyo cs 300
 
Pia ATCL wapunguze gharama za uendeshaji kwa kutumia mawakala badala ya kuwa na ofisi kila waendako. Hakuna haja yakuwa na watumishi wengi kwenye kila ofisi
 
Back
Top Bottom